KATUNI iliyochorwa na King Kinya, katika gazeti, The Citizen la Oktoba 16 mwaka huu, juu ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri aliyofanya Rais Jakaya Kikwete, imeniacha hoi!
KATUNI ya gazeti la Newsweek la Septemba 12 mwaka jana, ilimwonyesha George W. Bush (Namba 43 White House) akipiga simu kutaka maafa ya janga la katrina, New Orleans , yakabiliwe kijeshi.
MWAKA 1831, Seneta wa New York , William L. Marcy aliwahi kusema wakati wa majadiliano katika Bunge la Congress kwamba mshindi (wa uchaguzi) huja na majahili na mafisadi!
KAMA kuna Mwanasiasa ambaye harakati na mienendo yake ya kisiasa ni utata mtupu, mafumbo na kiini macho hapa Afrika Mashariki, si mwingine bali Waziri wa zamani wa Barabara, Ujenzi na Nyumba, Raila Odinga.
SEPTEMBA 22, mwaka 2004, Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa ,alipokuwa akihojiwa na Mtayarishaji wa kipindi maarufu cha Straight Talk Africa (VoA), Dk. Shaka Ssali, aliwatetea wawekezaji wa madini kwamba wamekuwa na manufaa makubwa kwa kuleta tija katika sekta hiyo na kusadia huduma za jamii nchini.