Mara kadhaa sasa Rais Kikwete na viongozi wenzake wa ngazi za juu wamekuwa wakishikilia picha ya kuchora ya simba wakiwatishia wahalifu. Kwanini wahalifu hawatatishiki?
Makala hii ilitoka kwenye gazeti la "Kulikoni" siku ya Jumatatu Octoba 22, 2007. Niliandika makala hii kufuatia kuendelea kwa Rais mstaafu Mkapa kuwa bubu kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili. Kwanini yuko kimya?
Kuna michezo mingi ya kitoto ambayo ukikaa chini kufikiria inakuwa kama methali yenye maana. Baadhi ya michezo hiyo bado tunawaona watoto wetu wakiicheza leo hii sehemu mbalimbali nchini. Na kuna nyimbo nyingi za michezo ya kitoto ambayo watoto wetu nao huiimba siku hizi wakicheza kila jua lichwapo na giza liingiapo. Mojawapo ya nyimbo ambazo bado nazikumbuka za toka utotoni ni ule wa “Kakuku ka mama Rhoda”. Sijui ni nani alianzisha wimbo au ni kwanini waliutunga, lakini kwa vyovyote vile huyo mtu alikuwa na lake kwani kuku wa jirani alikuwa anakula mpunga wa mtu huyo na kila akitaka kukafukuza basi mama Rhoda alikuwa “anamkataza.”
Taifa letu linapitia wakati mgumu na wa majaribu ya kisiasa. Kiini cha ugumu wa wakati huu ni mgongano wa fikra unaondelea kati ya watawala na watawaliwa, viongozi na wale wanaoongozwa.
Wakati akitoa hoja ya kulihairisha Bunge tarehe 18 August mwaka huu, Waziri Mkuu Mh. Edward Lowassa alihoji kwa kejeli kuwa watu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali wao "wamefanya nini kulisaidia taifa letu?". Hii ni sehemu ya pili ya majibu yangu ya swali hilo.