Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

 »  Home  »  Blogs  »  Sura mbili za Gaddafi, Umoja wa Mataifa na Afrika
Marshy Abdu
Insured by Mafia Islanders You hit me!! We hit you!!! 

View all blogs by Marshy Abdu...
Sura mbili za Gaddafi, Umoja wa Mataifa na Afrika
By Marshy Abdu | Published  07/16/2007

UHARAKISHAJI unaoonyeshwa na kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, kutaka utekelezaji wa mpango wake wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ya Afrika (USAFRIKA), una tafsiri mbili tofauti.

Kuna wanaomwona Gaddafi kama shujaa na mzalendo wa kweli wa Bara la Afrika, lakini kuna wanaotilia shaka msimamo wake, wakiamini ana ajenda ya siri.

Kwamba, baada miaka 40 ya kujaribu kulazimisha Libya kuungana na Sudan pamoja na kuutwaa ukanda wa Auziu kutoka Chad huku akifadhili mipango ya kuzorotesha nchi za Liberia, Uganda na kwingineko, je, tunapaswa tuwe na imani na malengo yake?

Lazima tuwe na shaka na mradi huu, haitakuwa ajabu kuyameza mataifa ya weusi ambayo mengi hayavutiwi na nia yake.

Katika hotuba yake mwaka 2005, aliutaka Umoja wa Afrika (AU) kuteua Waziri wa Ulinzi, Biashara na wengineo kama kipaumbele.

Aidha, alitaka kuwapo kwa jeshi la Afrika na kuzitaka nchi za Afrika kuwania kuteuliwa kuwa makao makuu ya vyombo mbalimbali vya AU/USAfrika.

Uharakisho huu unatia shaka kwa kiasi kikubwa. Ni wazi nchi za Kiarabu zenye utajiri kutokana na mafuta na huku zikiungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu, zitazimeza nchi maskini za weusi na hivyo kutoa nafasi ya utawala wa Kiarabu katika USAfrika.

Kama ilivyo kwa Umoja wa Mataifa kutawaliwa na genge la mabeberu ambako vyombo vyake muhimu ndiko viliko, huku Marekani ikiwa na Benki ya Dunia, IMF Washington na UN New York na Ulaya ikiwa na UNESCO, Mashirika wakala ya meli yakiwa London na mashirika mengine muhimu Geneva.

Iwapo dhana ya Gaddafi ya kutaka nchi zishindane kuweka makao makuu ya vyombo hivyo ingeruhusiwa, USAfrika kitakuwa chombo cha ukoloni wa Kiarabu na kitaimarisha madaraka ya Waarabu dhidi ya weusi.

Ulinzi ni kitu cha mwisho kufikiriwa katika vitu vinavyotaka kuunganishwa na kuwa huru kiutawala. Mfano mzuri baada ya mchakato wa miaka 50 wa kutaka kuwa taifa moja, nchi za Ulaya bado hazijateua Waziri wa ulinzi.

Ajabu, Gaddafi anayelindwa kwa asilimia 100 na askari wa kike, wakati mwingine akiambatana hata na walinzi binafsi 200, anakimbilia hilo hapa Afrika. Inatia shaka mno.

Hatari ya ukoloni wa Kiarabu inaonekana waziwazi nchini Mauritania na Sudan na linapaswa liwe fundisho.

Kisingizio cha kuwapo kwa fursa kubwa ya kunufaika kiuchumi iwapo Afrika itakuwa nchi moja hakina msingi.

Ukubwa wa Bara la Afrika si kigezo cha kuweza kuwa na nguvu kiuchumi.

Iwapo hiyo ni kweli, Japan, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uswisi na nchi nyingi za Ulaya zisingekuwa hapo zilipo bila kusahau baadhi ya nchi za Asia.

Aidha, mabara ya Atlantiki na Australia yenye utawala mmoja, yangekuwa na nguvu kiuchumi duniani iwapo ukubwa ungekuwa kigezo.

Kauli ya Gaddafi wakati wa mkutano wa Umoja wa nchi za Kiarabu nchini Jordan mwaka 2001; “Theluthi moja ya jamii ya Kiarabu inayoishi nje ya Afrika inapaswa ihamie kwenye theluthi mbili iliyopo barani Afrika na kujiunga na AU ambayo ni nafasi pekee tuliyo nayo,” inapaswa ichukuliwe kwa uzito mkubwa kwa jinsi inavyoonyesha yeye na Waarabu wenzake walivyo na ajenda dhidi ya Waafrika weusi mara tutakapoingia katika mtego wa USAfrika.

Waafrika weusi wana mambo mengi ya kuzingatia na kilicho muhimu ni kuingia katika majadiliano ya hatua kwa hatua kabla ya kukubaliana pendekezo hilo.

Waafrika weusi wanapaswa wasikubali tena ujinga wa viongozi wao mwaka 1973, wakati OAU ilipojipanga mstari nyuma ya Waarabu juu ya vikwazo vya mafuta kwa matumaini ya kupata upendeleo wa mafuta, bila kuwapo kwa makubaliano ya kueleweka ya maandishi hali iliyowafanya wasiambulie kitu baada ya Waarabu kuhujumu msaada wa uungwaji mkono waliopewa na weusi.

Kwa sababu hiyo na nyinginezo, tunashuhudia USAfrika kuwa mpango mpya wa ukoloni wa Kiarabu Waarabu na mpango wa kujipanua ndani ya mipaka ya Waafrika weusi, kila rais wa taifa jeusi la Afrika ndani ya AU anapaswa aukatae mpango huu. Wanapaswa waahirishe uamuzi wowote kwa miaka mitano zaidi ili kutoa nafasi ya mjadala mkubwa juu ya suala hili kuchukua nafasi miongoni mwa wananchi kuamua.

Wananchi ndio wanaopaswa kuwaambia marais wao nini cha kufanya, hiyo ni kwa mujibu wa demokrasia badala ya kujichukulia uamuzi kivyao huku wakipingwa na sauti ya wengi.

Tunapaswa tujifunze somo lililotokea EU ambako mchakato wa hatua kwa hatua ulichukua nafasi huku wananchi wakipewa nafasi ya kuamua.

Iwapo USAfrika itakubaliwa hivi sasa, Gaddafi na Waarabu wote watawacheka weusi kuwa ni mambumbumbu, ambao wameweza kuwalaghai kwa mara nyingine.

Tusisahau mawazo ya Waarabu dhidi ya weusi karne nyingi sasa, hebu tuangalie kauli hizi hususani kutoka kwa Obn Khaldun, Inb Sena na Osama bin Laden.

Ibn Khaldun anawaona weusi kama, watu wasio na staha, wakurupukaji, wenye kutaharuki na wenye mhemko mkubwa na kwamba; “wanaelezwa kila mahali kuwa watu wapumbavu”.

Al Dimashqi alikuwa na haya ya kusema; “Ikweta imejazwa na jamii za weusi ambao wanaweza kuhesabiwa kama wanyama wasiostaarabika. Rangi ya uso na nywele zao zimeungua na kimaadili na kimwili si wa kawaida. Bongo zao zimechemka kutokana na joto la jua.”

Ibn al Faqih al Hamadhani anafuata mkumbo huo huo wa kuwatukana weusi (zanj) kwamba; “wametengenezwa vibaya hadi kuungua kiasi cha kwamba mtoto huzaliwa kati ya weusi na uvundo mkali huku mioyo yao ikiwa pungufu.”

Ibn Khaldun anaongeza kwamba weusi ni binadamu tu wanapolinganishwa na wanyama mwitu. Aidha, ibn anasema kuwa weusi kiasili wamezaliwa kutumikia kama watumwa.

“Waafrika wote weusi ni malaya na taifa zima la wanaume wa Kiafrika wamezaliwa kuwa watumwa. Watu wake ni kama panya wanaopekua ardhi.”

Post a comment about this blog
Add comment
Comments


Your Favorite Articles

View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
No popular authors found.