Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

 »  Home  »  Blogs  »  ole zito akidhurika
Marshy Abdu
Insured by Mafia Islanders You hit me!! We hit you!!! 

View all blogs by Marshy Abdu...
ole zito akidhurika
By Marshy Abdu | Published  09/3/2007
VIONGOZI wakuu wa vyama vinne vya upinzani vinavyoshirikiana, jana walianza kwa kishindo vuguvugu la mabadiliko makubwa yajayo kitaifa katika medani ya siasa.

Viongozi hao, Freeman Mbowe, ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Wilfred Lwakatare na wawakilishi wa NCCR-Mageuzi mkoani Mwanza.

Wengine ni Mbunge machachari wa CHADEMA aliyesimamishwa shughuli za Bunge kwa miezi mitano, Kabwe Zitto na Lucy Owenya, Mbunge wa CHADEMA (Viti Maalumu).

Walianza ziara ya mikoa 12 kwa kupaa kwa helikopta na kuhutubia katika wilaya za Magu, Ukerewe na hatimaye Jiji la Mwanza, ndani ya siku moja.

Akizungumza katika mikutano hiyo mitatu, Mbowe, kwa sasa maarufu zaidi kwa jina la ‘Kamanda wa Anga’ alisema ziara yao hiyo ya mikoa 12 ina lengo la kuamsha chuki dhidi ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na mwenendo usiofaa wa viongozi.

Mbowe, alisema mwendo wa mambo ndani ya serikali ni uthibitisho kwamba, hivi sasa baadhi ya mawaziri katika serikali ya JKT wanapaswa ama kujiuzulu, kufukuzwa kazi na wengine kutupwa gerezani kutokana na kujihusisha na vitendo vya kuhujumu uchumi wa taifa.

Mbowe ambaye alikuwa akizungumzia tukio la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto la kusimamishwa shughuli za Bunge kwa miezi mitano na lile la Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa kuiondoa bungeni hoja yake kuhusu kashfa ya Benki Kuu (BoT), alisema tangu muda huo wabunge hao wawili wa CHADEMA wamekuwa wakipokea vitisho dhidi ya maisha yao.

Alisema kutokana na hali hiyo, amelazimika kumwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP, Said Mwema akimtaka aimarishe ulinzi wa wabunge hao ambao walisema wanatishiwa kutokana na kutetea masilahi ya taifa.

“Nimempelekea IGP Mwema barua nikimwambia iwapo Jeshi la Polisi linaweza kuwalinda mawaziri ambao miongoni mwao wamo wezi, ni kwa nini lishindwe kuwalinda wabunge hawa wawili ambao wanapata vitisho kwa sababu za kutetea rasilimali za taifa…” alisema Mbowe.

Mbali ya hilo, Mbowe alimtaka Rais Jakaya Kikwete kutambua kwamba iwapo Zitto au Slaa watadhurika, basi nchi hii itakuwa katika hatari ya kulipuka.

“Namwambia Rais Kikwete akidhurika Zitto au Slaa, nchi hii tutaiwasha moto…wakati umefika kwa Watanzania kuamka na kufanya kile ambacho kwa Kiingereza kinaitwa ‘Civil disobedience’ (uasi wa wananchi),” alisema.

Aliwaeleza wananchi waliofurika katika viwanja vya Nyakabungo katikati ya Jiji la Mwanza ambao walikuwa wakimshangilia mara kwa mara kwamba, ziara ya vyama vyao hivyo vinne kuzunguka mikoa 12, pamoja na masuala mengine, italenga kupandikiza chuki dhidi ya serikali na chama tawala.

Aidha, Mbowe aliwageukia wananchi, akawalaumu kwa kuwadharau viongozi wa upinzani na kuendelea kukichagua Chama Cha Mapinduzi ambacho matokeo yake kimeliacha jukumu la kuwatumikia.

Alisema jukumu la kuleta mabadiliko katika nchi ni la wananchi wenyewe, na wala si la viongozi wa upinzani peke yao, kama ambavyo imekuwa ikionekana na watu wengi.

Alisema, hivi sasa viongozi wa serikali wanaofahamu kwamba si waadilifu kwa taifa lao, wamekuwa wakisisitiza haja ya kuendeleza amani na utulivu kama mbinu ya kujihami na uwezekano wa kulipuka kwa hasira za wananchi.

Hata hivyo, alisema siku zinakuja ambazo Watanzania watalazimika kupigana kutetea haki zao, ambao katika siku hizo, wakuu wa wilaya, watashangaa watakapoona watu wakivamia ofisi zao na kudai haki wanazopokonywa.

Post a comment about this blog
Add comment
Comments


Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
No popular authors found.