Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

 »  Home  »  Blogs  »  Mbatia aziasa SACCOS Kilimanjaro
Marshy Abdu
Insured by Mafia Islanders You hit me!! We hit you!!! 

View all blogs by Marshy Abdu...
Mbatia aziasa SACCOS Kilimanjaro
By Marshy Abdu | Published  09/3/2007
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia, ameviasa vyama vya wanawake vya kuweka na kukopa (SAACOS) kujenga uaminifu na umakini katika kuendesha vikundi hivyo.

Mbatia alitoa changamoto hiyo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wanawake cha akiba na mikopo, Soki SACCOS, kilichopo Kata ya Mji Mpya.

Alisema kuwa, ni ndoto kwa vikundi hivyo kupiga hatua kimaendeleo iwapo hapatakuwa na kuaminiana na kuongeza kuwa hiyo ndiyo nguzo kuu ya kujikomboa kiuchumi.

Hata hivyo, Mbatia, ambaye alichangia sh 500,000 kwa kikundi hicho, alivitahadharisha vikundi kama hicho kuwa waangalifu katika utunzaji wa kumbukumbu na ukaguzi wa hesabu.

Alisema kuwa, utunzaji na ukaguzi wa vitabu ni mhimu na kutoa wito kwa wanachama wa SACCOS kufuatilia kwa umakini mienendo ya utendaji kazi wa viongozi wao.

Akifungua mkutano huo, Mbatia alivitaka vikundi vyote, vikiwamo vya aina hiyo, kuzingatia kanuni na taratibu zinazozimamia masuala ya biashara na kuongeza kuwa, biashara bila daftari, hupotea bila habari.

Alishauri wanachama wa SACCOS kuwa na elimu ya ujasiriamali ili waende sambamba na mabadiliko ya kiuchumi na kwamba bila elimu hiyo ya ujasiriamali, itakuwa ni kazi bure na hivyo kushindwa kufikia malengo.

Kikundi hicho cha wanawake chenye wanachama 53, wakiwamo wanaume wawili, kina jumla ya hisa zenye thamani ya sh milioni 1.3 na akiba ya sh milioni 8.4.

Post a comment about this blog
Add comment
Comments


Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
No popular authors found.