Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

 »  Home  »  Blogs  »  Wengine CCM kuwekwa kitimoto leo
Marshy Abdu
Insured by Mafia Islanders You hit me!! We hit you!!! 

View all blogs by Marshy Abdu...
Wengine CCM kuwekwa kitimoto leo
By Marshy Abdu | Published  09/3/2007
 


LILE sakata wa wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha kukamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa litachukua sura mpya leo baada ya viongozi wengine wa chama hicho kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho.

Wakati hayo yakitokea, bado haieleweki ni lini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) ambayo ndiyo iliyowatia mbaroni wabunge hao na wapambe wao akiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) mkoani Arusha, watafikishwa mahakamani kukabili tuhuma hizo.

Alipotafutwa kwa simu aelezee hatima ya wabunge hao na wenzao, Kamanda wa TAKUKURU mkoani humo, Ali Mfuru, hakuweza kupatikana kwani simu yake haikupatikana wakati wote.

Hata hivyo, habari zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa CCM ambao hawakupenda kutajwa majina yao kwa kuwa si wasemaji, zilieleza kuwa viongozi wengine waliokamatwa na TAKUKURU wakihusishwa na tuhuma hizo, nao watahojiwa leo.

Tayari wabunge hao, Elisa Mollel (Arumeru Magharibi) na Michael Lekule Laizer (Longido) walishahojiwa na habari zinasema kuwa walitakiwa kuandika barua ya kujiondoa katika nafasi wanazowania.

Wakati Mollel, ambaye hivi sasa ni mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoani humo anawania ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Laizer yeye anausaka uenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, wabunge hao wametoa taarifa wakikataa kujitoa wakidai kuwa kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kukiri kuwa wanahusika na tuhuma hizo wakati si kweli.

Viongozi ambao walikamatwa ni pamoja na mwenyekiti huyo wa UVCCM, Daniel Ole Porokwa, ambaye alikutwa na sh 436,500 ambazo TAKUKURU inadai kuwa zilikuwa zinagawiwa kwa wajumbe walioalikwa katika kikao hicho.

Viongozi wengine ni John Palangyo ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Nkoaranga na mjumbe wa Mkutano wa CCM wilaya na mkoa, Danieli Losioyo, mwakilishi kutoka Arumeru na Abrahanu Kaaya mwenyekiti Kijiji cha Maroroni na mjumbe wa halmashauri ya CCM wilayani Arumeru.

Wengine ni Emmanueli Laizer, mwenyekiti wa kata ya Longido, Ndewirwa Soori Mbise, Afisa Mtendaji wa Kata ya Nkoaranga na mjumbe wa kutano mkuu wa CCM wa mkoa na taifa, Charles Akyoo, Katibu Kata ya Usa River na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wa wilaya na mkoa, Abubakar Shekalage, Katibu Mwenezi Kata ya Usa River na mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya na mkoa na dereva wa gari namba T 428 APE, Abdi Mushi. Gari ambalo linasadikiwa ni la Mbunge wa Longido.

Watuhumiwa hao walikamatwa katikati ya wiki iliyopita katika mji mdogo wa Usa River wilayani Arumeru, katika hoteli ya Rotterdam, wakati wanapanga kukutana na baadhi ya wajumbe ili kuwashawishi wawachague kwa kuwapa rushwa.

Taarifa ya TAKUKURU ilieleza kuwa Porokwa yeye ndiye alikutwa amekabidhiwa fedha kiasi cha sh 436,500 zinazosadikia kuwa ndizo zilikuwa zitumike kuwapa wajumbe hao walioalikwa mahali hapo.

Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa ilizuka purukushani kubwa na mapigano baada ya wabunge hao na wapambe wao kuvamiwa na maofisa wa Takukuru waliokuwa wameweka mtego.

Hata hivyo, hatua ya CCM mkoani Arusha kuwahoji viongozi hao ni tofauti na msimamo uliowahi kutolewa hicho hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu wa chama, Jaka Mwanbi, kuwa haitajishughulisha na wananchama na viongozi wake ambao watanaswa na TAKUKURU kwa tuhuma za kuhijusisha na rushwa.

Post a comment about this blog
Add comment
Comments


Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
No popular authors found.