Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

 »  Home  »  Blogs  »  Ikulu yamjibu Mbowe
Marshy Abdu
Insured by Mafia Islanders You hit me!! We hit you!!! 

View all blogs by Marshy Abdu...
Ikulu yamjibu Mbowe
By Marshy Abdu | Published  07/24/2007


OFISI ya Rais (Ikulu), imekanusha madai ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyoyatoa mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mkutano wa hadhara Sirari, wilayani Tarime.

Ikulu katika taarifa yake kwa gazeti hili jana, ilisema Rais Kikwete alikwenda katika Wilaya ya Serengeti kwa ajili ya mapumziko ya kawaida na si kwa lengo la kuhujumu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime uliofanyika jana.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Maura Mwingira, alisema kwamba mapumziko hayo ya Rais huko Serengeti yalikuwa katika ratiba kwa muda mrefu na hayakuwa na uhusiano wowote na uchaguzi huo wa Tarime ambao umehusisha mvutano mkubwa kisiasa kati ya CCM na CHADEMA.

“Tumeshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA katika gazetini lenu la leo inayohusisha mapumziko ya kawaida ya Rais huko Serengeti, kilomita zaidi ya 300 kutoka Tarime na kufanyika kwa uchaguzi wa halmashauri,” alisema Mwingira.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Sirari mwishoni mwa wiki, Mbowe alisema kuwa ameshangazwa na ziara hiyo ya Rais Kikwete kutotangazwa na vyombo vya habari na kudai kuwa, ana hofu ya chama chake kuhujumiwa madiwani wake wanaotarajia kuchuana katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya.

Mbowe alisema: “Viongozi wa juu wa taifa wa CCM wamekuwa wakifuatilia na kuwavuruga wanachama wa vyama vya upinzani, hata katika chaguzi ndogo, kwa kuvihujumu vyama hivyo, kwa kuwarubuni wanachama wao kuhama vyama kama walivyotuhujumu Kigoma.”

Alisema hadi kufikia hiyo juzi, CHADEMA ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kiti hicho ikiwa na madiwani 15, CUF wawili na CCM 13 katika Jimbo la Tarime, ukilinganisha na Jimbo la Rorya lenye madiwani 22 wa CCM na watano wa upinzani.

Alisema kuwa iwapo CHADEMA itashinda katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, itashirikiana na CCM kuhakikisha wanakuwa mfano mwema katika kudhibiti fedha zinazotolewa na serikali na wafadhili katika kuwaletea wananchi maendeleo, hususan barabara, maji, shule, zahanati na kusaidia vikundi vya wajasiriamali katika Wilaya ya Tarime.

Kama moja ya mkakakti wa kuhakikisha wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi huo, chama hicho kiliwachukua madiwani wake wote 15, pamoja na wawili wa CUF, na kuwapeleka katika semina inayofanyika mjini Musoma.

Post a comment about this blog
Add comment
Comments


Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Nthelezi Nesaa
  4. Linda Garner
  5. Marshy Abdu
No popular authors found.