kawaida imekuwa mara nyingi ikisababisha athari kubwa katika jamii zetu tunamoishi.
Hii ni kutokana na tabia iliyozoeleka miongoni mwetu kuwa kawaida ni moja na sehemu muhimu katika kufikia maamuzi ya kutekeleza wajibu fulani.
Katika suala la mahari kuna aina mbili ya sababu zinazojenga dhana hasi dhidi ya jukumu hilo la waunganao.
Ni dhahiri kuwa katika jukumu la mahari, kuna malipo yatokanayo na desturi/mila za kikabila sambamba na uhali wa kifamilia.
Maoni yangu katika hili ni kwamba heri kufikia muafaka wa kuoana bila gharama za upande a binti kwani kwa gharama hizo kumekuwepo na vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake mara baada ya kuolewa na waume zao kwa kigezo na kisingizio cha gharama kubwa ya mahari.
Imani yangu ni kuwa wapo vijana wa kiume ambao wao hukerwa na malipo hayo ya mahari na kuona kama ni adhabu au malipo ya manunuzi ya mke, fikara ambazo ni potofu.
La msingi kwa jimii ni kubadilika na kufikia uamuzi wa kuachana na desturi/mila zinazokandamiza haki za kila mmoja katika suala la wawili kujenga familia moja(MkeMme).
Mwisho