Ni mwandishi wa habari za Kikanda, Kitaifa na Kimataifa.
Ni mtangazaji wa Radio Kwizera mkoa wa Kagera na Kigomaa, (Kigoma Press Club) napatikana kwa anuani hii, pkwigize@habaritanzania.com, au pkwigize@yahoo.com, mpigie simu na. 0784676888 au 0754077478.
Tuijenge dunia yenye mawasiliano makini,na Tanzania inayoheshimu vipaji.
Shirika la mazingira na haki za binadamu la REDESO wilayani Kibondo limetoa msaada wa ujenzi wa nyumba kwa mzee mmoja aliyetelekezwa na mwanae na kumwacha bila makazi.
Shirika la kidini nchini linalohudumia wakimbizi TCRS limeanzisha ofisi zake nchini Burundi ili kuwasaidia warundi na wakimbizi watakaorejea nchini mwao kutoka nchini Tanzania.
Jumla ya migogoro 62 imewasilishwa kwa kamati maalumu ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi wilayani Kibondo mkoani Kigoma katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kuanza kazi kwa kamati hiyo.
Mwananfunzi mmoja wa shule ya sekondari Maragalasi wilayani Kibondo amefanikiwa kuunganisha mitambo na kurusha matangazo ya radio katika eneo la Kibondo mjini.
Serikali imeahidi kutoa kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa wahanga wa ajali ya gari la mizigo iliyotokea wilayani Biharamlo na kupelekea vifo vya watu 29 wakiwemo wakazi 12 wa wilaya ya Kibondo.
Kijana mmoja Mtondo Gabriel mkazi wa kijiji cha Rusohoko wilayani Kibondo anasakwa na shirika la REDESO kitendo cha utetezi na uzuiaji wa unyanyasaji wa kijinsia kwa kosa la kuwatelekeza baba yake na mkewe mwenye watoto wane.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Maragalasi wilayani Kibondo ambaye mtandao huu ulitangaza kufanikisha kwake kuunganisha mitambo ya redio na kurusha matangazo amejitokeza hadharani kuomba misaada.
Watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia na kupora fedha tasilimu shilingi laki tatu na nusu pamoja na vitu mbalimbali katika kambi ya Kanemba wilayani Kibondo.