              
|
|
Ndesanjo Macha
|
| Naitwa Ndesanjo Sila Macha. Zamani nilijulikana kwa jina nililokuwa wala sijui maana yake, Gregory.
Mimi ni Mtanzania ambaye ninapigania nafasi ya lugha na maarifa ya Afrika mtandaoni. Ninajihusisha pia na juhudi za kuwezesha watu wetu kuwa na uwezo, maarifa, na mbinu za kutumia teknolojia mpya za habari na mawasiliano kwa ajili ya maendeleo ya kijamii, kitamaduni, kisiasa, kiakili, na kiuchumi.
Ninaguswa sana na dhana mpya ya uandishi wa raia ambapo kwa kutumia zana mbalimbali raia kama mimi na wewe tunaweza kuwa na vyombo vyetu vya habari bila kutumia gharama kubwa na wakati mwingine bila kutumia gharama yoyote ile. Kila mmoja wetu ana jambo la kusema. Kila mmoja wetu ana haki ya kujieleza. Hivyo zana za kutuwezesha kufanikisha msukumo tulionao binadamu wote wa kuwasiliana wa wengine na kutoa mawazo yetu ninazichukulia kwa makini sana.
Kwa kuwa demokrasia ya kweli hujengwa kwa majadiliano na juu ya msingi wa maarifa na habari, umma wenye maarifa na wenye uwezo wa kuwasiliana na kushiriki kwenye mijadala ya mustakabali wake kamwe hauwezi kukubali kuendeshwa kama gari au kuswagwa kama kondoo. Ninaamini kuwa zana hizi (blogu, wiki, n.k.) zinaweza kutumia kutawanya maarifa na kujenga mawasiliano ya moja kwa moja miongoni mwa raia bila kupitia katika mfumo wa vyombo vikubwa vya habari (ambavyo huwa ninaviita “vyombo vya uongo”) ambavyo malengo yake ni kuzalisha faida kwa ajili ya wamiliki na wenye hisa.
|
Articles by this Author
»
Yaliyoamuliwa Kwenye Mkutano wa Wanablogu wa Tanzania
»
Tanzanian bloggers’ virtual conference
|
Tanzanian bloggers held their first virtual conference on November 18th, 2006. The aim of the conference was to discuss various steps to be taken to make the community more effective and expand its reach. Most bloggers feel that there is an opportunity for blogs to be a tool for critical national dialogue and social development.
|
»
Tuwaokoe haraka Keko, Kurasini Mbagala na Vijibweni.
|
Ukikiliza kisa kizima cha tukio lililotokea mwishoni mwa mwaka jana kuhusu wananchi wa Vijibweni huko Kigamboni kupinga ujenzi wa mradi wa gesi,kama huzingatii unaweza kuchukulia suala hili kama suala dogo la kawaida na la kupita.
|
|
|