Katika kuangalia namna Rais Jakaya Kikwete alivyoshupalia suala la filamu ya Darwin's nightmare, mtu yeyote mwenye akili anashangaa ni kwanini Rais anapoteze muda wake na wa taifa,heshima na mengine kama hayo kujiingiza kwenye kutafuta majibu ya maswali ambayo yaliishajibiwa.
Tarehe 11 Septemba ni siku ya wamarekani pamoja na dunia nzima kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi maarufu kama 9/11. Dunia nzima hasa marafiki wa Marekani wanaungana na wamarekani kwa hali na mali.
Safu hii mara nyingi hujadili mambo mbali mbali bila kuacha nyuma suala zima la dini na mila zetu. Leo pasina kupitwa na wakati tumejikita kwenye kuijadili alama mojawapo kuu na kongwe ya mojawapo ya dini mojawapo kongwe. Tutajitahidi kuonyesha chanzo hata upogo urongo unaozunguka uwepo,ujio,utumizi na maana nzima ya alama hii ya msalaba.
What is going on in Tanzania with regards to power rationing annoys and sickens. If anything, what TANESCO is maliciously doing to our people begs more questions than answers.
Jana tarehe 19 Septemba, marais wa Marekani George W. Bush na mwenzake wa Iran, Mahamoud Ahamadnajad, walihutubia mkutano wa baraza la umoja wa mataifa jijini New York.
Hivi karibuni mameya wa majiji ya Madrid nchini Hispania na Milano nchini Italia wamepania kuangalia upya suala zima la ushiriki na viwango katika mashindano ya mitindo na mavazi kwenye majiji yao.
Katika kutafakari mambo na hali inavyoendelea nchini Irak,safu hii imeonelea ijaribu kutoa mpambano wa kimatukio baina ya wababe wawili waliosababisha mauaji makubwa na udhalilishaji wa kutisha katika kitatange kinachoendelea nchini humo.