Lengo la utoaji wa misaada hiyo kwa taasisi mbalimbali hususani zile za kielimu ni kama njia ya shukurani kwa Watanzania ambao ndio wanamiliki asilimia sabini ya hisa za benki ya CRDB.
Watu wanane wanaosadikiwa kuwa majambazi yakiwa na silaha yameyateka kwa muda wa saa saba, machimbo ya dhahabu ya Nyakahula, wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Wateka nyara wa mtoto Humudy Aboubakary (3) pichani mkazi wa Magomeni Makurumla na Uweje, jijini Dar es Salaam ambao bado wanaendelea kumshikilia mtoto huyo, sasa wamempiga picha ..
Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema kuwa Serikali itahakikisha kwamba hakuna mtu atakayekufa njaa kwenye maeneo yote yaliyokumbwa na mafuriko mkoani Kilimanjaro
Yanga ya Dar es Salaam ambayo ni moja ya timu tatu za Bara na yenye jukumu la kwanza kubakisha nyumbani Kombe la Kagame la klabu bingwa ya soka ya Afrika Mashariki na Kati kutokana na kuwa mshindi wa ligi kuu ya Bara mwaka jana, jana ilianza kwa kwa wasiwasi michuano hiyo na kuambulia sare ya 0-0 mbele ya St. George ya Ethiopia
Serikali imeliagiza Shirikisho la Soka, TFF, kuziondoa kwenye orodha ya wanachama wake klabu za Simba na Yanga endapo hazifanya marekebisho ya katiba zake ili zifanane na ya shirikisho hilo.
Wachezaji wa timu ya Moro United ya Morogoro wametakiwa kujituma zaidi kwenye mazoezi na uwanjani na hatimaye kuongeza kiwango cha uchezaji ili wachaguliwe kwa wingi katika timu ya taifa, Taifa Stars.
Timu za netiboli za Zanzibar mwaka huu hazikusajili wachezaji kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya ligi kuu itakayoanza Juni kwenye uwanja wa Gymkhana, imeelezwa.