Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakulima Igoma Mwanza waitaka serikali kuwabana wenye viwanda.
Wakulima Igoma Mwanza waitaka serikali kuwabana wenye viwanda.
By Prosper Kwigize | Published  09/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi wa HabariTanzania.com, Mwanza
Ni kutokana na kuzagaa kwa maji taka mashambani mwao
Wanafunzi wa shule ya msingi Mandela wanatumia maji taka kuoga
 

 
 Wakazi wa bonde la Igoma jijini Mwanza wamelaumu viwanda kuyaachia maji taka yanayotoka viwandani kuzagaa hali inayohatarisha afya za wakazi na wakulima wa eneo hilo.
 
 Akiongea na waandishi wa HabariTanzania.com kuhusu mazingira jijini mwanza mmoja wa wakulima na wakazi wa Igoma Bw. Mohamed Sakara ameeleza kuwa maji taka ya viwanda vya coca cola, mwatex na kiwanda cha kuyeyusha vyuma vichakavu yote huishia katika mashamba yao.
 
 Bw. Sakara amebainisha kuwa kutokana na kuzagaa kwa taka taka hizo katika mashamba yao kilimo kimekuwa kigumu mazingira yameharibika na kwamba ipo hatari ya kuibuka kwa magonjwa.
 
 Amefafanua kuwa miaka kadhaa iliyopita bonde la Igoma ilikuwa ndilo mkombozi wa kilimo cha mbogamboga hususani mchicha, kabichi na mazao ya nafaka kama mahindi na mtama.
 
 Aidha mkulima huyo amebainisha kuwepo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela ambao huogelea katika dambo la maji taka kutokana na kutokuwepo kwa kinga yoyote katrika madambo ambayo hata hivyo hayatunzwi na wenye viwanda.
 
 Mabomba ya maji machafu kutoka katika viwanda hivyo yanaonekana kutofanya kazi kutokana na kutokuwa na matunzo yoyote pamoja na kupitisha maji mengi kuliko uwezo wake
 
 Mkulima mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe ameeleza kuwa bomba la maji taka linalotuika kwa sasa lilijengwa na kiwanda cha Mwatex miaka mingi iliyopita na wakati huo hakukuwa na tatizo lolote hadi lilipoanza kutumiwa na viwanda vingine ambavyo havijajenga mabomba yao.
 
 Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa HabariTanzania.com amebaini kuwa kupasuka na kuzagaa kwa maji machafu katika bonde la Igoma na kutotumika kwa miundombinu ya maji taka kumetoka na hujuma iliyofanywa na wakulima hao ambao huhitaji maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
 
 Mmoja wa wakazi wa eneo la shule ya msingi Mandela aliyejitambulisha kwa jina la mama Kassim amekanusha kuwepo kwa watoto wanaooga maji taka hayo ingawa amesema mara nyingi watoto hao huchezea katika maeneo yenye dampo hilo.
 
 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mandela ailyehojiwa na kujitambulisha kwa jina la John Magesa anayesoma darasa la nne amekiri kuwepo kwa baadhi ya watoto wanaotumia dampo hilo kama bwawa la kuongelea hususani nyakati za masika.
 
 Juhudi za kuwapata wamiliki wa viwanda na viongozi wa jiji la Mwanza hazikuzaa matunda kutokana na kutokuwemo ofisini kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki na juhudi za kuwapata zinaendelea

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.