Mkazi wa Mlandege, Iringa, Bw. Emanuel Edward Wanel, ameibuka mshindi wa kwanza wa mchezo wa Nipashe Motomoto katika droo ya tatu iliyochezwa kwa ajili ya mikoa ya kanda ya kaskazini, hivyo kujinyakulia kitita cha Sh. milioni moja.
Mchezo huo ambao ni mfululizo wa michezo ya Nipashe Motomoto inayochezwa kwenye kanda tofauti hapa nchini, ulifanyika jana kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini.
Mchezo huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu akiwemo Meya wa Manispaa ya Iringa, Bw. Amani Mwamwindi.
Aidha katikaa mchezo huo, Bw. Daud Juma Feruz, mkazi wa Mwangata, Iringa, alishika nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa Sh. 500,000.
Washindi wengine na maeneo wanayotoka ni Bw. Neviln Charles Nyange, mkazi wa Iyunga Mbeya aliyetia kibindoni Sh. 250,000 na Bi. Paulin Mwakipesile, mkazi wa Kihesa aliyepata Sh. 150,000.
Aidha, licha ya zawadi ya fedha hizo, washiriki kadhaa walijinyakulia fulana za Nipashe.
Baadhi ya washiriki waliopata kofia ni pamoja na Edwin Rwegasira Swai, Daudi Mahenge, Jakobo Sanga na bahati Emil Hamza.
Wengine waliozawadiwa fulana za Nipashe ni Michael J. Muyinga, Hassan Nassor Mkonga, Selina Kalinga, Tumaini Mawele, Samwel Mushi, Augustino Kafyulilo na Daud Sauli.