Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwimbaji aliyefia kanisani
Mwimbaji aliyefia kanisani
By Habari Tanzania | Published  09/16/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Utata wa kifo cha Bwana Shemndolwa Kihiyo, 55, aliyekuwa muimbaji wa kwaya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, KKKT usharika wa Manzese na ambaye alidondoka ghafla kanisani kabla ya kufariki umeondolewa na hivyo kufuta hisia potofu zilizoanza kujitokeza.

Francis Kihiyo ambaye ni mmoja kati ya watoto wa marehemu, amezungumza kwa niaba ya familia yao akisema kuwa hakuna mkono wa mtu katika kifo hicho na badala yake, msiba huo umetokana na mapenzi ya Muumba.

Kuhusiana na tukio lenyewe, Francis anasimulia hivi: ’’Masaa saba kabla ya kifo chake, mimi mwenyewe nilikuwa naye. Wala hakuwa na dalili zozote mbaya kiafya.’’

Anasema ’’ Hata hivyo, alishawahi kudondoka siku za nyuma akiwa kwenye kazi za kanisa kama katika tukiuo hili, lakini hilo la kuanguka awali lilitokea maeneo ya Ubungo na ilikuja kubainika kuwa kuanguka kwake huko kulitokana na kusumbuliwa kwake na shinikizo la damu.’’

Akisimulia zaidi, Francis ambaye anadai walielezwa kila kilichojiri na wanakwaya wengine waliokuwa na baba yake kanisani kabla ya kukumbwa na umauti, anasema kifo chenyewe kilikuwa hivi: ’’Aliacha ghafla kuimba, akamstua mwenzie kwa kumshika bega, akanyoosha mikono yake akionyesha dalili za kutaka kukaa, lakini ghafla akaanguka chini na kubamiza paji la uso’’’.

Amesema baada ya kitendo hicho, wenzake walianza kumpepea huku baadhi yao wakiharakisha kusaka gari la kumuwahisha hospitali.

Hata hivyo hawakuwahi kwani walipofika Muhimbili waliambia Mola kishamtwaa kitambo.

Kifo hicho kilitokea wiki hii katika kanisa hilo la KKKT Manzese na kuthibitishwa pia na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni , Jamal Rwambow.

Alisema kifo hicho kilitokea mishale ya saa 2:30 usiku wakati marehemu akiimba na wenzie kwaya za kumsifu Bwana.

Kabla ya kusimulia zaidi juu ya namna kifo hicho kilivyomkuta baba yao mpendwa, Francis amesema: ’’Naamini kuwa siku za baba kuishi duniani zilikuwa zimekwisha. Yote hayo ni mapenzi ya Mungu ambaye hutoa na kutwaa kwa mapenzi yake.’’

Kuhusiana na shughuli za mazishi, Francis ameeleza kuwa walitarajia kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda kwao Bumbuli, Lushoto na kumlaza kwenye nyumba ya milele.

Taarifa za Kipolisi kuhusiana na marehemu zinasema kuwa hakuna anayeshikiliwa kutokana na kifo hicho cha ghafla na kwamba marehemu aliyekuwa akiishi maeneo ya Shule ya Msingi Tandale ameacha mke, watoto sita na wajukuu saba.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.