Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Mambo yazidi kuwa magumu kwa Bush.
http://www.habaritanzania.com/articles/990/1/Mambo-yazidi-kuwa-magumu-kwa-Bush.
By Nthelezi Nesaa
Published on 09/15/2006
 
Rais wa Marekani bwana George W. Bush anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya chama chake cha Republican kuanza kumgeuka na kumpinga wazi wazi.

Na Mwanahabari wa HabariTanzania.com, Canada

Rais wa Marekani bwana George W. Bush anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya chama chake cha Republican kuanza kumgeuka na kumpinga wazi wazi.

Hii imetokea wiki hii ambapo waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje chini ya utawala wa Bush,Generali mwenye nyota nne, Collins Powell kumtandika barua Rais Bush akipinga sera nzima ya ukamataji na kuhoji watuhumiwa wa ugaidi.

Collins amerejea tena kuhimiza kupinga kwake zoezi zima la kuzuilia watuhumiwa wa ugaidi kwenye kambi ya Guantanamo. Hii ni kutokana na kufanya hivyo kuvunja ibara ya tatu ya Mkataba wa Geneva (Geneva convention) ambao unasema kuwa wahalifu au watuhumiwa watendewe kibinadamu.

Wakati barua hiyo ya Powell vumbi lake halijatua,Bush alipata pigo jingine baada ya wabunge vikaka wa chama chake kumpinga wazi wazi wakiongozwa na Senata John McCain ambaye ni shujaa wa zamani wa vita.

Pamoja na mtoto wa nyumbani kama wanavyomuita waziri wa sasa wa mambo ya kigeni, Dr. Condolezza Rice, kuja na barua ya kujibu barua ya Powell, Bush alibaki hana la kufanya baada ya maseneta kujibu mapigo baada ya Bush kutoka kukutana nao Capitol Hill ili kuwanyamazisha na wasinyamaze.

Wakati sakata hilo likiendelea, vyombo vya habari vimegundua kuwa Marekani imeamu kuwasajili jeshini wasenge,wahalifu sugu wa zamani hata watoro wa shule ili kupata watu wa kwenda mstari wa mbele hasa nchini Afghanistan.

Hii ni baada ya nchi 34 zilizoombwa na Marekani kuchangia majeshi ili kuzima hujuma za watalebani zinazozidi kuongezeka kukataa kufanya hivyo wakihofia usalama wa majeshi yake.

Wakati nchi hizo zikikataa, baadhi ya washirika wa Marekani wanaanza kufikiri upya mantiki na madhara ya vita inayoendelea nchini Afghanistan hata Irak.

Kwani mshirika wa karibu wa Marekani yaani Canada, kwa sasa inapambana na upinzani mkubwa toka wananchi na vyama vya upinzani unaoongozwa na kiongozi wa upinzani Jack Layton.

Bw. Layton anasema wazi kuwa waziri mkuu wa Canada Bw. Stephen Harper anaonekana kuburuzwa na Bush.
Upinzani huu umetokea baada ya Canada kupoteza wanajeshi wengi mwaka huu kwenye mapigano huko Afghanistan.
Canada ilianza kuisaidia Marekani nchini humo tangu mwaka 2002.

Marekani kwa sasa inakabiliwa na hasara kubwa kutokana na vita nchini Afghanistan na Irak. Kwani kupitia kipindi cha Cafferty File kinachorushwa na CNN, takwimu zinafichua kuwa hadi sasa askari zaidi ya 2,000 wameishauawa katika Iraq na Afghanistan huku wengine zaidi ya 4,000 wakiwa wamepoteza viungo vyao.