Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Nthelezi Nesaa  »  Je msalaba siyo alama ya upagani?
Je msalaba siyo alama ya upagani?
By Nthelezi Nesaa | Published  09/15/2006 | Nthelezi Nesaa | Rating:
Na Mwanahabari wa HabariTanzania.com, Canada
Safu hii mara nyingi hujadili mambo mbali mbali bila kuacha nyuma suala zima la dini na mila zetu. Leo pasina kupitwa na wakati tumejikita kwenye kuijadili alama mojawapo kuu na kongwe ya mojawapo ya dini mojawapo kongwe. Tutajitahidi kuonyesha chanzo hata upogo urongo unaozunguka uwepo,ujio,utumizi na maana nzima ya alama hii ya msalaba.
 
 Kama ilivyo alama ya nyota na mwezi, msalaba ni alama kuu na muhimu ya dini ya kikristo. Msalaba ni sawa na bendera ya nchi kwa ukristo. Hivyo ni alama muhimu na yenye thamani kubwa. Je inastahiki kupata heshima na umuhimu huu ? Hilo ndilo swali kuu la kushughulika nalo leo.
 
 Twende kazini. Ushahidi wa kwanza kuwa msalaba una chimbuko na maana kwenye dini za awali za kipagani unapatika kwenye katiba yenyewe ya ukristo yaani biblia wanayoiita wao takatifu. Soma waebrania 12 ;2 kwa ufafanuzi zaidi.
 Pia kuonyesha ujio na uwepo wa msalaba na mkanganyiko wa jamii ya waumini inayoifuata biblia, waweza kusoma 1 wakorintho1 ;17 na 18 ambapo mitume wanatukuza tendo lililofanyika kwenye msalaba na siyo msalaba kama ilivyo sasa.
 
 Kabla ya kwenda mbali lazima tukiri kuwa uchambuzi wetu utaonyesha jinsi msalaba ulivyokuwepo kama alama ya dini za kipagani hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu mwenyewe. Tutajaribu kufanya hivyo ili kuonyesha upagani ulivyopaganisha ukristo huku na ukristo ukikiristisha upagani na kufanya ndoa ya mashaka inayoendelea hadi leo tunaandika.
 
 Katika kamusi ya Expository of new tastment words, yaani kamusi fafanuzi ya maneno ya agano jipya, inasema kuwa msalaba kama alama ya kipagani ilianzia kule Ukaldayo ( ambapo pia ndiko chimbuko la Ibrahimu). Kamusi hii inasema kuwa wapagani wa eneo hili waliitumia alama ya msalaba kama heshima yao kwa muungu wao wa kipagani aliyeitwa Tammuz ambaye kimsingi ni Nimrodi muwindaji na mwanzilishi wa himaya ya Babeli iliyolaaniwa kuliko hata firauni.
 
 Tammuz kwa ufupi aliitwa « Tau » akitumia alama ya T kama alama yake kuu au sahihi tuseme. Alama hii ya T kama ishara ya Tammuz pia ilitumika si ukaldayo tu bali hata misri na asia wakati ule ikizingatiwa kuwa Tammuz aliweza kuabudia karibia maeneo hayo yote wakati wa himaya yake.
 
 Msalaba pia unaweza kupatikana katika jamii za kimisri za kipagani za hapo mwanzo. Ushahidi huu unapatikana kule kwenye jengo la Amenopolis IV kule Tabes nchini misri. Msalaba huu unajulikana maarufu kama « Msalaba wa Misr au Msalaba wa tau. Hii ni kutokana na baadhi ya kazi za wanahistoria maarufu wa zama zile. Msalaba huu ulikuwa na mduara upande wa kichwani ukiashiria alama ya Tammuz akiwa kama muungu jua hapo baadaye.
 
 Pia katika maeneo ya Ufoenike,China na Mexco inapatikana dhana nzima ya matumizi ya kidini ya msalaba kama alama yao kuu. Ikumbukwe kuwa yote hii ni kabla ya kuzaliwa kwa Yesu hivyo kabla ya ukristo tulio naos asa.
 
 Jamiii nyingine unapopatikana msalaba kama alama shufaa ni maeneo kuanzia nchi ya Niger ya sasa hadi mto Nile. Kwani ngao za mashujaa wa eneo hili zilichorwa alama hii kama ishara ya utaua na ukuu.
 
 Ushahidi madhubuti waweza kupatikana pia nchini Mexco ambako msalaba maarufu wa Palengue unapatikana. Kwa anayetaka ushahidi zaidi juu ya hili aweza kusoama kwenye “The catholic encyclopidia “ ambayo licha ya kuuita msalaba wa Palengue inauita msalaba wa kabla ya ukrist wa Palengue.
 Msalaba huu nchini uliitwa pia Tota ama baba kama ambavyo baadaye uliitwa kwenye biblia. Soma Yeremia 2 ;27 hii imebainika kuwa upotofu mkubwa kuanzia lugha hata matumizi ya neno baba kumaanisha msalaba.
 
 Nchini Misri inapatikana pia michoro ya au picha ya Muungu Amon akiwa ameshikilia msalaba wa Tau.
 Pia kwenye hekalu la serapis kule Alexandria lilibeba alama ya msalaba.
 
 Hata kwenye vita bain aya Alexander Mkuu (Alexander the great),na waajemi, waajemi walibeba msalaba kama alama yao ya ushindi. Pia hapa ikumbukwe kuwa utumizi wa alama ya msalaba kwenye vita ilianzishwa na akina Nebkadneza na wenzake kama alama ya ushindi.
 
 Kwa ufupi angalau msomaji anaweza kuona utamaduni huu wa kuutukuza na kuutumia msalaba ulikotoka kuwa ni kwenye dini za kipagani za kale. Hiki ndicho tulichomaanisha tuliposema kuwa upagani umepaganisha ukristo na ukristo umekristisha upagani na kufanya ndoa kuu ya urongo na mashaka.
 
 Hebu tuhame twende nchini Italia ambako ndiko chimbuko hasa la ukristo chini ya himaya ya kiroma. Mwaka 46 kabla ya kuzaliwa Yesu, kunapatikana sarafu za muungu jupiter zikiwa na alama ya msalaba ambao kwa wapagani wa kiitaliano ulitumika kama hirizi au sihiri kama unavyotumiwa na baadhi ya madhehebu ya kikristo kwa sasa.
 
 Hata ukiangalia sarafu aliyoletewa Yesu alipe kodi ilikuwa na Maandishi Partem max yaani baba mkuu ambaye alikuwa ni kaizari, ilikuwa na alama ya msalaba. Hilo leo siyo mjadala wetu hivyo tutalitumia kwenye ushahidi huu tu.
 
 Hata kule Ugiriki ulichorwa msalaba kwenye vibanio na nembo ukiwa ni alama ya mfalme wao aliyefanana sana na Tammuz.
 
 Tusiwachoshe na rejea na ubukuzi na uchokonozi. Hebu tujiulize swali rahisi. Je msalaba hadi hapa ni alama ya Kimungu au kimiungu ? je inaingia akilini hadi leo mtu kuendelea kuutukuza na kuuvaa shingoni ikiwa ni kama kinga au hirizi kwake ? je kama mtu atategemea kulindwa na msalaba huyo Mungu atafanya kazi gani jamani !
 
 Je inaingia akilini kuendelea kuutumia msalaba kwenye mahekalu ya Mungu,nyumba zetu,makaburi yetu,kuuchora kwenye vipaji vya uso kila mtu aingiapo kanisani na mengine kama hayo ? Je ni nani mwehu huyo awezaye kuivaa shingoni bastola iliyotumika kumuua mpendwa wake kama kinga ? kama hata akili nyepesi ingetumika basi bastola ingeogopewa kiasi cha kutisha kwani ndiyo iliyouchukua uhai wa mpendwa wako. Je ni nini mantiki ya wakristo kuvalishwa kongwa bila makosa ?
 
 Je inaingia akilini kwa mtu ambaye amejua maana na chimbuko la msalaba kuendelea kuivaa hiyo kongwa na alama ya laana ? kazi kwenu. Je anayefanya hivyo anaendelea kuwa mkristo wa kweli au mpagani wa kawaida tu hata akijiita mkristo ?
 
 Hatulengi kudhalilisha imani za wenzetu wala kuwaonyesha kama majuha lakini ni ujuha kutumia alama ya kipagani ambao kimsingi ndiye adui mkubwa wa dini. Tunaandika haya kwa kuzingatia ushauri wa bure lakini wa maana wa Yesu. Alisema kuwa mkiitafuta kweli itawawa huru kweli kweli. Kama hivyo ndivyo kwanini nasi tusiwaweke huru kweli kweli ?
 
 Kwa taarifa yako msomaji msalaba umekuwa nongwa kwa wakatoliki hasa. Kwani huchora alama ya msalaba kila waingiapo kanisani,kunywa au kula,wakati wa kulala wakati wa kuamka n.k Pia msalaba huchorwa kwenye mwili wa mtu tangu siku ya kuzaliwa (kubatizwa) hadi kuzikwa huku kaburi lake likiubeba milele !
 
 Kwa waroma msalaba uko kila mahali. Kwenye meza,makanisa,hata tumbo la kanisa limejengwa kwa ishara ya msalaba, hata kwenye vikombe wanavyotumia kanisani hufunikwa kwa kitambaa chenye alama ya msalaba. Kwa taarifa yako ni kwamba padre hufanya alama ya msalaba mara 16 wakati akiendesha misa huku akiongeza mara 30 za kuibariki altare!
 
 Kama kweli msalaba ni alama ya laana na ya kipagani huku ni kufanya nini kama siyo kuwalaani waumini hata madhabahu yao . Je hapa kunaweza kuepukika kwa mabalaa na majanga yanayolikumba kanisa kama vile ulawiti na uzinzi wa mapadre wake?
 
 Imekuwa ni jadi kw mkatoliki kujilaani kwa kila afanyalo. Hali wala hanywi bila kujitia alama hii ya laana.
 
 Hata tukiambwa kuwa msalaba unatumiwa kama alama ya kusulubiwa kwa Yesu ambaye ni alama ya ukombozi wa kinjozi, bado haiingii akilini kwani zana na nyenzo hii ilianza kutumika kabla ya kuzaliwa na kusulubiwa kwake. Je ni wapi ukiachi siku ya kusulubiwa ulipoona Yesu na wanafunzi wake wakiongozana na msalaba kwenye shughuli zao za kueneza injili?
 
 Tuhitimishe. Huko Misri, Ugiriki , Syria na Karthago,Palestina na Roma msalaba pia ulitumika kuwaadhibia wahalifu waliokuwa wametenda maovu makubwa kama alama ya kulaaniwa kwao.
 
 Kimsingi msalaba na matumizi yake vimepotoshwa sana kama ilivyo kwa dhana kuu ya ubaba. Soma Matayo 23;9 hadi 11. tukiache magube ya kanisa ,hili liko wazi kuwa msalaba hauna uhusiano na ukristo wala dini aliyoileta Yesu. Huenda tukikubali kusema kuwa Ukristo siyo dini aliyoleta Yesu twaweza kuyakumbatia na kuyakubali matumizi ya msalaba kwa raha bila ubishi.
 
 Lakini si kosa la kanisa. Kwani kama hadi leo halijamjua Yesu mwenyewe litajuaje upogo na najisi ya msalaba kwa kazi ya Mungu? someni Matayo 6 ;8, Matayo 10 ;34, Matayo 13 ;55 na 56 na Matayo 27 ;46,Marko 10 ;17 kwa ushahidi wa haraka na kwa ufupi ndipo utagundua upogo na magube yak anisa katika matumizi ya dhana mbali mbali.
 
 Tuhitimishe kwa kukaribisha hoja juu ya kuyavinjari haya tunayoletewa bila kuhoji. Huu ndiyo wakati muafaka wa kuhoji na kuhoji na kuhoji hadi kweli ipatikane ili ituweke huru kweli kweli.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by P.Mamu)
    Rating
    Naendelea kutafakari hoja hii.Kimsingi kuna mantiki katika argument yako.
     
  • Comment #2 (Posted by kirenga)
    Rating
    TFADHALI MAMBO ULIOANDIKA NI SAHIHI, LAKINI KWA NINI MAASKOFU,MAPADRI,WACHUNGAJI,NA WAINJILISTI AWAAMBII WAUMINI UKWELI ILI WAWEZE KUJUA KWELI.
     
  • Comment #3 (Posted by an unknown user)
    Rating
    good point, but all major religion have paganic influences on them.
     
  • Comment #4 (Posted by Madakomulume)
    Rating
    Nina mashaka na lengo la makala yako. Inawezekana huna dini na kwa sababu hiyo unajaribu kuchambua kitu usichokijua. Au u mpizani wa dini hasa ukatoliki kwa sababu zako mwenyewe. Yote hayo tukiyaacha ninachoweza kukwambia hapa kwanza ni kuwa Yesu hakuwa mwanzilishi wa Ukrisyo wala hakuhubiri Ukristo. Yeye alihubiri habari njema. Kwa mantiki hiyo kitu cha kuzingitia kwa Wakristo ni hicho; je wanaishi habari njema? Siyo suala la wametumia nini kuabudu. Pili Unafahamu lugha ya kwanza kabisa ya Biblia ni ipi? Rejea tena vifungu vya biblia ulivyotoa na ikiwezekana uombe msaada wa wanatheolojia wakusaidie kufafanua.
     
  • Comment #5 (Posted by mwambata kiambata)
    Rating
    Hongera kwa uchambuzi. Lakini sehemu nyingine umechemsha na kuonyesha chuki ya wazi kwa Ukristo; hasa kwa Ukatoliki. Yesu alikuja kuleta habari njema na akasema mkaihubiri kwa mataifa yote. Yesu hakuhubiri ukristo kama alivyotangulia kusema Madakomulume. Labda nikuambie kuwa kila kitu kina msingi wake au mwanzo wake. Baada ya msingi hujengwa jengo na watu wakiishi ndani ya jengo hilo ndo huitwa nyumba. Na mtu huweza kuamua kuipamba au kuweka alama mbalimbali katika nyumba yake ili itambulike kwa urahisi. Angalia magari kama ferrari Ukiona gari lenye alama ya farasi tu hata kama haijaandikwa Ferrari utajua tu ndo lenyewe.
    Na hata katika hatua mbalimbali za viumbe hai kuna msingi wake. Kwa ufupi (kwa kuwa wewe ni mchambuzi mahiri) angalia hatua zote ulizopitia hadi kufikia kuitwa Nthelezi Nesaa. Au mwenzetu ulikurupuka tu na kuwa mtu mzima hivyo? Ghafla bin Vuuh! Agalia hatua zote anazopitia nzi au mbu hadi kuwa mdudu kamili. Zote zina msingi wake. Hivyo hivyo na "Ukristo" au "Upagani" au "Dini za Jadi" wote una msingi wake. Na msingi mkubwa au chimbuko za dini zote ni kumtafuta "Mkuu wa Viumbe Vyote ... vinavyoonekana na visivyoonekana kwa macho". Na polepole jengo la imani hujengwa. Na watu wakishaingia katika jengo hilo au imani hiyo ndiyo huitwa DINI. Na kisha watu huweza kuzipamba nyumba zao kwa alama mbalimbali au rangi mbalimbali ali mradi kutofautisha na nyingine kama alivyoamua Tau kutumia alama ya T.Kama kwa magari mbalimbali yenye alama za kutambilisha ni la kampuni gani. Lakini kampuni haiweki nembo bila kuwa na maana au msingi fulani. Na Wakristo (Watoto wa mwenye jengo) waliamua kutumia alama hiyo kama alama yao ya kidini. Na pole pole hatua kwa hatua wakaipa MAANA KUU au "Patrem Max" katika maisha yao. Na kwa taarifa yako, kama Kristo angesulubiwa katika jiwe na kupigwa kwa mawe hadi kufa. "Wafuasi" wake leo hii wangevaa au kutumia alama ya JIWE badala ya msalaba. Katika makala yako moja(sikumbuki ipi) uliandika kuwa wewe ni binti yake mpendwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu J.K. Nyerere. Mwalimu, (kwa mfano) alipoamua kuunda Chama cha Mapinduzi alama iliyotumika ni ya Jembe na Nyundo nyenye rangi ya njano na bendera ya kijani. Hii ni alama ya kukitambulisha Chama. Na kama alama hizi zingetumika kama ipasavyo yaani kuzipa maana(kama ulivyopewa msalaba mkuu) kwa watoto wa mwenye nyumba (yaani wanachama) kwa kiasi fulani ari ya kuleta maendeleo kwa kutumia Jembe (wakulima) na Nyundo(wafanyakazi) ingetufikisha mbali kimaendeleo. Ni kweli pengine utaniambia mbona msalaba ulitumika vibaya kwa nyakati fulani. Sintakuzuia kuwaza upendavyo kwani ndo "demokrasia mawazo". Ni hitimishe kwa kukupongeza tena ila angalia changamoto zako ziliwe za chuki bali zisaidie kufungua watu macho ili waweze kuwa "Huru" kimawazo wakishaujua msingi na "Ukweli" wa msalaba kwao waaminio (Watoto wa mwenye jengo)!
     
  • Comment #6 (Posted by Julius George)
    Rating
    This story is excellent in that it provides a sincere insight re.the essence of Msalaba, giving vivid references for an open minded person it wil be very easy to understanbd and take the right decision in this world before we die and regret irreversibly!! Congrats Nesaa keep enlight6ening us with your educative topics...
     
  • Comment #7 (Posted by Martin Elisante(Nalindwa na damu ya Yesu))
    Rating
    Siko tayari kuvumilia kweli ya Mungu iliyonyooka inavyo pindishwa namna hii.Neno la Mungu(Biblia) inasema "msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi lakini kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu".Kuangikwa msalabani ilikuwa kitendo cha aibu na adhabu waliopatiwa wahalifu katika jamii ya kiyahudi.Kwasababu Yesu Kristo yeye ambaye hakuwa na dhambi wala uovu haukuonekana ndani yake, mwokozi wa ulimwengu aliyezaliwa katika jamii ya kiyahudi ilimpasa kufa kifo cha aibu ili azichukue dhambi za ulimwengu.Nasema Yesu Kristo alishachukua dhambi zetu leo hii sisi tunaokoka kwa kuliamini jina lake "YESU" pekeyake. Mimi ni mkristo na nimesikitishwa sana na jinsi watu wasivyokuwa na maneno ya Mungu ndani yao na kuchukuliwa na upepo wa kila aina wa mafundisho potofu na roho zidanganyazo zilizoandikwa kwenye Biblia zinafanya kazi ndaniyao. Wakristo wenzangu someni maandiko ndio kweli Mungu ilipo, msisubirie kasisi ama mtu fulani ndio awasomee na ninyi mnahoji uhalali.Hata YESU mwenyewe aliwaambia masadukayo mnapotea kwa kutoyafahamu maandiko. Mwisho namtaka mwandishi ajielezee kwamba yeye yuko upande gani kwasababu hakuna katikati aidha kwa Yesu ama kwa yule bwana mwingine kwa kujua ama kwa kutokujua.
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.