Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Makali mgawo wa umeme yaongezeka
Makali mgawo wa umeme yaongezeka
By Habari Tanzania | Published  09/15/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Kulwa Karedia

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hakutakuwa na umeme nyakati za mchana kwa wiki nzima.

Kutokana na mabadiliko hayo, Ijumaa na Jumapili ambazo zilikuwa na umeme siku nzima, sasa hazitakuwa na umeme.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Adriaan van der Merwe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana alisema kuwa, hatua hiyo inatokana na idhini ya serikali ya kufanya mabadiliko ya mgawo wa umeme kwa nchi nzima.

Alisema kutokana na mabadiliko hayo, umeme utazimwa kuanzia saa 1.00 asubuhi na kurejeshwa saa 1.00 usiku kila siku.

Tangu TANESCO ilipotangaza kuwapo kwa mgawo wa umeme nchi nzima, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wateja wakidai kuwa wamekuwa wakipoteza muda wa kuzalisha tofauti na ilivyokuwa awali.

Mgawo huu ulianza baada ya kuharibika kwa mtambo wa Kampuni ya Songas inayozalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.

Mtambo huo ulioharibika Agosti 23, mwaka huu tayari umepelekwa nchini Uholanzi kwa matengenezo yatakayochukua wiki nane ambapo gharama ya matengenezo hayo inayolipwa na Songas ilitarajiwa kufikia dola bilioni moja.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.