Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahakama yazuia ubomoaji maghorofa
Mahakama yazuia ubomoaji maghorofa
By Habari Tanzania | Published  05/24/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
.Hatima baada ya kesi ya msingi kusikilizwa
 

MAHAKAMA Kuu kitengo cha Ardhi, jana iliamuru kusimamisha ujenzi na ubomoaji wa maghorofa ya Masaki, Dar es Salaam.
 
Ubomoaji wa maghorofa hayo, mali ya Kampuni ya Empire Properties Limited, katika barabara ya Toure, unatekelezwa na Manispaa ya Kinondoni, inayoeleza kwamba kibali cha ujenzi huo ni batili.
 
Jaji Angela Kilewo wa mahakama hiyo, alisema kuwa amefikia uamuzi huo ili haki itendeke kisheria kwa pande zote mbili zinazovutana, wakati kesi ya msingi ikitarajiwa kusikilizwa Juni 7, mwaka huu.
 
Kampuni ya Empire Properties, kupitia wakili wake Kololo Bundala, iliwasilisha maombi mahakamani, ikitaka kusimamishwa kwa ubomoaji wa majengo hayo ili haki itendeke kusubiri kesi ya msingi.
 
Wakili wa manispaa, Johnson Jasan, alipinga madai hayo, kwa madai kuwa mteja wake ameingia gharama, na hivyo kuitaka mahakama kutokubaliana na madai hayo.
 
Aliomba siku saba ili apate fursa ya kwenda kupitia vielelezo vya kesi na kujenga hoja za utetezi wake, huku akisisitiza kwamba vibali vya ujenzi vya mlalamikaji si halali.
 
Jaji Angela aliamua kesi isikilizwe Juni 7, siku ambayo kesi ya msingi pia itasikilizwa.
 
Katika hali tofauti, shauri la jana lilichelewa kusikilizwa muda uliopangwa saa 5 asubuhi na kufanya ianze saa saa 8 mchana, baada ya manispaa ya Kinondoni, kudaiwa kugoma kupokea hati ya kuitwa mahakamani.
 
Muda wa kesi ulipofika saa 5, wakili Bundala aliiambia mahakama kuwa walalamikiwa-manispaa ya Kinondoni walipelekewa hati ya kuitwa mahakamani Mei 19, mwaka huu, lakini waliikataa kuipokea.
 
Kutokana na hali hiyo, Jaji Angela aliahirisha kesi hiyo hadi saa 8 mchana na kuamuru dalali wa mahakama kupeleka hati nyingine. Alisema asingeweza kutoa uamuzi hadi pande mbili zitakapokuwepo mahakamani.
 
Ubomoaji wa jengo hilo unafanywa na Manispaa ya Kinondoni, ukiwa chini ya ulinzi mkali, kwa madai kwamba ujenzi umekiuka kibali cha ujenzi na pia kuna vibali vilighushiwa.
 
Kesi nyingine kuhusu sakata la maghorofa hayo ipo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, ambapo watumishi wanne wa idara ya ujenzi wa |manispaa ya Kinondoni walifikishwa juzi kwa kughushi nyaraka na kuzificha.
 
Majengo mawili yanayobomolewa, moja inadaiwa kibali cha ujenzi kimekiukwa kwani iliruhusiwa kujenga ghorofa tatu, lakini mjenzi akaongeza ghorofa; wakati jengo lingine linadaiwa halina kibali cha ujenzi.
 
Wakati huohuo, maofisa wa manispaa jana waliachiwa baada ya kukidhi masharti ya dhamana.
 
Hakimu Mkuu Mfawidhi, Sivangirwa Mwangesi, alisema kuwa wadhamini wa washitakiwa hao waliwasilisha hati za nyumba ambazo zilikaguliwa katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kuonekana kuwa ni halali.
 
Washitakiwa hao wote kutoka idara ya Ujenzi ya Manispaa ya Kinondoni ni: Robert Sinde Warioba (46), ambaye ni Mhandisi Msaidizi, Fundi Mchundo Olympia Kundi (38), watunza kumbukumbu Joyce Mwamlima (39) na Diana Peter (44).
 
Kesi hiyo itatajwa Juni 5, mwaka huu.
 
Kutoka gazeti la Uhuru
ISSN 0876-3896 NA.19318
Na Njumai Ngota

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.