Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Serikali yajikanganya filamu ya utumwa
Serikali yajikanganya filamu ya utumwa
By Habari Tanzania | Published  09/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na David Frank, Arusha

WIZARA ya Nishati na Madini Kanda ya Kaskazini, imekana kutoa kibali kwa waandaaji wa filamu ya ‘Watumwa wa Vito’ ambayo inawahusisha watoto wadogo katika uchimbaji wa madini ya tanzanite.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Ofisa Mfawidhi wa Madini Kanda ya Kaskazini, John Nayopa, alisema waandaaji wa filamu hiyo walifika ofisini kwake, lakini aliwanyima kibali.

Hata hivyo, watengenezaji wa filamu hiyo walipata kibali cha serikali kutoka Idara ya Habari (MAELEZO), Ofisi ya Waziri Mkuu wakati huo.

“Mimi niliwakataza kwenda Mererani. Leo nashangaa kuona picha hizi… huu ni uhuni, na una athari kubwa," alisema Nayopa.

Alisema watu hao walikuwa wanataka kwenda kwenye machimbo ya tanzanite Mererani, lakini baada ya kuzuiwa kupiga picha ndipo walirejea ofisini mwake.

“Sisi tumejiwekea utaratibu, huwezi kwenda tu kupiga picha kwenye migodi bila idhini yetu," alisema Nayopa.

Filamu hiyo ambayo ilitarajiwa kuzinduliwa jana Jijini New York, Marekani, imeandaliwa na Shirika la Habari la Kimataifa la IRIN kwa msaada wa mashirika mengine ya UNICEF na ILO.

Filamu hiyo inaonyesha jinsi haki za watoto zinavyokiukwa sambamba na jinsi wanavyotumikishwa vibaya.

Waliofika nchini kuandaa filamu hiyo ni William Rondolph aliyekuwa na pasi ya kusafiria namba 205538707 na Jandries Groenendik aliyekuwa na pasi namba NF 6412034.

Imebainika kuwa aliyewapa kibali ni Ofisa Habari Mkoa wa Arusha, Richard Mwangulube, kwa maelekezo ya mkuu wake, John Hokororo aliyekuwa makao makuu.

Akizungumzia filamu hiyo, Mratibu wa Shirika la Good Hope, Harry Mushi, alisema: "Mimi nilikuwa Mererani nikapigiwa simu na ILO na ofisa habari kuwa niwasaidie hawa na nilifanya kazi hiyo, lakini nashangaa walichokionesha ni mapungufu pekee."


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.