Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Nthelezi Nesaa  »  Documentary ya Sept 11
Documentary ya Sept 11
By Nthelezi Nesaa | Published  09/13/2006 | Nthelezi Nesaa | Rating:
Na Mwanahabari wa HabariTanzania.com, Canada.
Tarehe 11 Septemba ni siku ya wamarekani pamoja na dunia nzima kuwakumbuka wahanga wa mashambulizi maarufu kama 9/11. Dunia nzima hasa marafiki wa Marekani wanaungana na wamarekani kwa hali na mali.
 
 Tarehe 12 Septemba documentary inayoitwa The secret of 9/11 History. Nchini Canada inaonyeshwa na kituo maarufu cha CBC.
 
 Katika documentary hiyo kuna masuala mengi yamejitokeza kuhusiana na tukio zima la Septemba 11.
 
 Muhimu kati ya hayo ni uzembe wa serikali nzima ya Marekani katika siku ya tukio hilo.
 
 Kwa mfano katika mahojiano na baadhi ya washauri wa kiusalama. Wanakiri kuwa kuna uzembe mkubwa ulitokea. Kama vile kuruhusu watekelezaji kumi na sita wa mashambulio ya Septemba 11 kupita kwenye mamlaka za uhamiaji za Marekani miezi kumi na nane kabla ya tukio wakiwa na nyaraka ama za kughushi au zisizokamilika.
 
 Pia kuna siri imefichuka kuwa ndege mbili za kijeshi zilizotumwa kudungua ndege yeyote iliyokuwa inaelekea Washington siku hiyo hazikuwa zimepewa amri ya kufanya hivyo ukiachia mbali kuelekezwa vibaya. Kwani zilipewa ramani isiyo kiasi cha kujikuta kilimeta takriban 250 kutoka New York.
 
 Tatu, ndege iliyokuwa imepewa amri ya kushambulia au kutungua ndege yeyote ya kibiashara iliyokuwa inaelekea jijini Washington haikuwa na silaha.
 
 Nne haijulikani ni nani alitoa amri ya kutungua ndege. Kwani kisheria amri ya kufanya hivyo imo mikononi mwa Rais. Wakati huo huo utafiti, kwa mujibu wa documentary hiyo unaonyesha kuwa mawasiliano yalikatika baina ya Limousine ya Rais na White house pamoja na kwenye Air Force one. Hata kumbukumbu za mawasiliano za Ikulu kwa siku hiyo zinaonyesha kuwa hakukuwa na amri toka kwa Rais siku hiyo.
 
 Tano, kwenye makao makuu ya usalama wa anga wa Marekani siku ya tukio kulikuwa na mtu mmoja tu ofisini na ambaye kisheria hakuwa na mamlaka ya kutoa taarifa kwa majeshi ya Marekani juu ya kuchukua hatua.
 
 Sita, pia documentary inasema kuwa jeshi la Marekani lilitaarifiwa kuhusu kutokea kwa mashambulizi zikiwa zimechelewa. Kwani ndege ya kijeshi ya Marekani iliyotumwa kuangalia hali ya usalama wa jiji la New York ilipita juu ya kituo cha biashara cha dunia (WTC) mnara wa mwisho ukianguka.
 
 Saba, kuna ushahidi kuwa Rais George W. Bush alionywa na makachero wa serikali wa kupambana na ugaidi miezi mitatu kabla ya tukio na hakuchukua hatua.
 
 Pia mamlaka ya usalama wa anga ya Marekani ilishatoa tamko na taarifa ya maandishi kwa mashirika ya uchukuzi wa anga na serikali lakini serikali bado ilikalia taarifa hizo.
 
 Hali hii imesababisha watu waanze kusema kuwa mashambulio ya Septemba 11 yana mkono wa serikali. Maana hata taarifa za serikali kuwa ndege iliyoanguka Pennslivania ikielekea New York ambapo serikali inasema kuwa kuna simu zilisikika toka kwenye ndege si za kweli. Maana wataalam wameruka juu ya eneo hili kiasi cha mita 30,000 ambazo ndege hiyo ilikuwa na kugundua kuwa simu haziwezi kupokea signal kwenye urefu huu. Hii imeamsha maswali ya ni kwanini serikali iliamua kudanganya ili iweje?
 
 Kimsingi kuna mikanganyiko mingi kuhusiana na uzembe na utendaji wa serikali nzima ya Marekani kuhusiana na mashambulio ya Septemba 11.

Nthelezi Nesaa
 Canada
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.