Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Nthelezi Nesaa  »  The Darwin's Nightmare
The Darwin's Nightmare
By Nthelezi Nesaa | Published  09/12/2006 | Nthelezi Nesaa | Rating:
Na Mwanahabari wa HabariTanzania.com, Canada

Katika kuangalia namna Rais Jakaya Kikwete alivyoshupalia suala la filamu ya Darwin's nightmare, mtu yeyote mwenye akili anashangaa ni kwanini Rais anapoteze muda wake na wa taifa,heshima na mengine kama hayo kujiingiza kwenye kutafuta majibu ya maswali ambayo yaliishajibiwa.

Documentary hii nzuri ilitengenezwa na mtenezaji filamu Hubert Sauper ambaye anajulikana kwa umaarufu wake kutengeneza filamu za kusisimua ili kujipatia riziki yake.

Kwanza filamu inayomuhangaisha Rais haikutengenezwa jana wala juzi. Ina muda mrefu kwani ilitengenezwa akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje. Hivyo kama kweli alikuwa na nia ya kuitetea hadhi ya nchi yake kama anavyotaka aonekane baada ya kuwa rais, tunadhani angefanya hivyo muda mfupi baada ya filamu kutoka kwani ilikuwa kwenye eneo lake la utendaji kazi kama waziri wa mambo ya nchi za nje.

Si mpya kwa sababu baadhi ya vyombo vingi vya habari hasa magazeti vilishaelezea kilichomo humo. Hata waandishi wengi wa humo nchini wameishaandika sema kutokana na katabia kabaya ka jamii kusahau mapema machapisho,usishangae sakata hili kuonekana kama kitu kipya.

Pia ifahamike kuwa hasara au taathira inazopata Tanzania na watanzania kutokana na madhara ya kadhia hii,yavilinganishwa yale yanayosababishwa na matatizo ambayo yako ofisini mwake na asifanye kitu,tena kwa kuwauliza wananchi,tunadhani suala la documentary litaonekana kama upuuzi Fulani.

Kwa mfano sifa ya Tanzania ni nini na ina maana gani ikilinganisha na madhara yatokanayo na sera nzima ya ubinafsishaji kama ilivyotekelezwa kijambazi na kibububusa na serikali iliyopita?

Hatuoni kama Darwin's Nightmare, kwa mfano ina madhara sawa na IPTL,Net Group Problems, Makampuni ya madini yanayoipa serikali mrahaba wa asilimia tatu ilhali kwa madini kama hayo hayo Nchi kama Botswana inapata zaidi.

Hatuoni kama madhara yatokanayo na filamu hii yanaweza kulinganishwa na madhara yanayotokana na hujuma zinazofanywa na makampuni ya uwindaji na utalii huko mbugani.

Kimsingi filamu hii inaongelea sehemu ndogo ya nchi yetu tofauti na madhara tajwa hapo juu yanayoikabili nchi yetu.

Tunadhani Rais angeshughulikia masuala yanayoingia akilini mwa wananchi kwanza ya kupambana na uoza uliopita kiasi alioukuta ofisini mwake badala ya kufanya waingereza waitacho "witch-hunt and white wash"

Hatuoni madhara yatokanayo na filamu tajwa maana inachosema ni ukweli kwani kama ni kuwepo kwa unyonyaji wa kiuchumi upo pale mwanza. Nani kasahau kuwa hata zile kashfa zilizowafukuzisha kazi akina Profesa Joseph Mbilinyi, Kilontsi Mpologomyi na Dr. Juma Ngasongwa inatokea huku.

Japo siyo hoja katika mjadala huu, hata yakitakiwa maelezo kwa mfano ni kwanini wale waliokuwa wanaonekana kuwa mangapi na mizigo kwa serikali iliyopita amewarudisha maofisini tena kwenye idara nyeti, tunadhani jibu litakuwa gumu. Haya kimsingi ndiyo mambo ya maana ya kuweza kumshughulisha Rais ili awape majibu watanzania na siyo ubabe.

Ukifuatilia filamu ya The Darwin's Nightmare, utakuta kuwa mtengenezaji licha ya kuonyesha umaskini wa waswahili wa pale mwanza, alitaka mataifa makubwa ambayo ndiyo wanunuzi wakubwa wa sangara waone ni kwa kiasi gani wanachangia katika jinai hii ya umaskini kwa kununua kitu ambacho nadhani tafsiri ya haraka ni haramu.

Hapa mtengeneza filamu licha ya kuwa mkweli, alikuwa makini kutaka kuwashawishi wanunuzi wa sangara kujua ukweli kuwa hawana haja ya kutumia pesa nyingi kiasi hicho kununua kitu ambacho kimezalishwa kwa bei nafuu hata kwenye mazingira machafu.

Anayekana kuwa kilichosemwa na mtengeneza filamu si ukweli, ajiulize jina mapanki kwa mfano limetungwa na nani? Ni wananchi wenyewe. Je lina maana nzuri kiuchumi na kijamii?

Hivyo kimsingi mtengenezaji wa filamu hakuwa na nia mbaya kama watawala wetu wanavyoiangalia. Hivi kwa mfano mtu akionyesha mayatima walioko Makete na mateso wanayo yapata utasema ameidhalilisha nchi?

Juzi hapa Canada Televisheni ya CBC, usiku ilionyesha picha ya waathirka wa ukimwi huko nchini Zambia. Kwa bahati nzuri documentary hii ilitengenezwa na mtengenezaji filamu na mwandishi mashuhuri Sorius Somirwa, kutoka Afrika Magharibi.

Ni aibu na uchungu ukiangalia watu kwanza walivyo maskini na wajinga ukiachia mbali mateso wanayopewa na ukimwi. Ukiwalinganisha kwa mfano na aliyekuwa Rais wao Fredrick Chiluba, picha yao ni aibu kwa Zambia lakini ni ukweli.

Je kwa mfano wenye viwanda Mwanza hawanyonyi wananchi wanaoshughulika kwenye industry ya uvuvi?

Hilo tuache, ukija suala la umalaya. Ni kweli kuwa si jambo la kutia chuku kuwa nchini Tanzania na Kenya wanaharakati wa ukimwi wanapata kibarua kigumu kupambana na ongezeko la waathirika wa ukimwi kwenye visiwa vilivyomo kwenye ziwa Nyanza.

Visiwa vimevuta hisia za wanaharakati wa ukimwi kutokana na ukweli kuwa kuna umalaya wa kupindukia kwenye visiwa hivyo.

Filamu ikisema kuna umalaya Mwanza tunadhani siyo kutukana wala kuidhalilisha Mwanza wala Tanzania. Ni hali halisi na ni ukweli mtupu.

Hivi kwa mfano mtu akisema kuwa maeneo ya Kinondoni na Ohio jijini Dar es salaam na Kwa Macheni yanaongoza kwa vitendo vya kimalaya atakuwa anaaibisha jiji na nchi?

Je kwa mfano mtu akitoa documentary kuonyesha watanzania japo si wote, walivyopoteza utu kiasi cha kufanyia ngono kwenye makaburi ya Kinondoni bila aibu wala utu, atakuwa anaidhalilisha nchi na jiji.

Au hata mtu akitoa documentary kuonyesha ubomu wa wasomi wa kitanzania kutokana na kukithiri kwa wizi wa mitihani ataambiwa anaihujumu nchi? Ni nani anahujumu nchi kati ya yule anayetenda na yule anayeandika. Hii ni sawa na kulaumu chombo cha habari kwa kuandika uchafu wako wakati hutaki kujilaumu kwa kufanya uchafu huo.

Tunadhani Rais hapa aachane na masuala madogo ashughulikie masuala ya muhimu na nyeti kwa faida anwai ya wananchi badala ya sifa za juu juu.

Tumalizie kwa kumshauri Ndugu Rais arejee kuiangalia na kufikiria upya juu ya filamu husika,hatuna shaka ataungana nasi kuwa kinachoelezwa mle siyo uongo bali ukweli.

Kwa madai ya Mwanza kupitisha silaha, jibu la ukweli na uongo ni upi laweza kutolewa na swali fupi tu.

Je unapobinafsisha hata mamlaka za kusimamia bandari na viwanja vya ndege unategemea nini kuhusu hili?

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by mtemi)
    Rating
    kusema kweli huyo anatetea sera yake na anajua mwenzie alifanya nini sasa wanalindana. hajui mapanki maana yake nini au hataki kuelewa
     
  • Comment #2 (Posted by Eng. Magafu, F.F)
    Rating
    very good comments. It a time to change for our leaders.
     
  • Comment #3 (Posted by Kamaliza Jumanne)
    Rating
    Hongera mtandao wa habaritanzania kwa kupata waandishi waliokwenda shule. Nimefurahi kusoma mchango wa huyo mwandishi Nthelezi Nesaa. Tofauti na watu waliopofuka wakidhani ni uzalendo,mwandishi amesema ukweli tena ukweli mtupu. Huu ni mfano wa kuigwa hasa linapoangaliwa suala la ukweli.
    Nchi nyingi changa zimebaki nyuma kutokana na kuogopa kusema ukweli. Au mwenzetu huyu kwa vile yuko huko kulikoendelea ndiyo ameamua aanzishe huu utamaduni mpya?
    Hongera mwandishi na mtandao tena
     
  • Comment #4 (Posted by an unknown user)
    Rating
    pricise to my opinion
     
  • Comment #5 (Posted by Raymond)
    Rating
    Umekong'ori nyoyo za watu baba
     
  • Comment #6 (Posted by jo)
    Rating
    Huu ni ukweli usiopingika na nadhani Pres wetu hana jipya zaidi ya kushabikia vitu ambavyo ni vya kweli usio pingika. Anatakiwa apasue kchwa kwa kuangalia lini huu mgawo wa umeme uataisha, lini tutafaidi maliasili zetu ( madini na wanyama pori ), lini titaacha kubinafsisha mipaka yetu ( bandari / maziwa ) na mambo mengine mengi makubwa ambayo akipita barabani kama matanzania halisi anatikiwa kuona kila kitu ni jukumu lake, mfano akikuta njaa eneo fulani ajue huo ni mzigo wake ambao anaweza akaulizwa siku moja akiomba kura kwa kipindi kijacho au kwa maanani..... This is serious, atuwezi kupotosha jamii kwa ukweli usifichika na hii ni sawa sawa na mtu amejisaidia haja kubwa bila kunawa vizuri halafu mabwana afya ( inzi ) wanamfuata kwa wingi kutokana na kuwakaribisha kwenye chakula chao halafu unasema kwa kirahisi tu ya kuwa nimenawa vizuri wakati inzi na watu wanakuona hujanawa vya kutosha, sorry nimetumia mfano mabaya lakini ukitaka ujumbe ufike kwa sisi watz tumia maneno machafu / matusi ndiyo utaeleweka vizuri. Thanks and keep it up my brother from Canada.
     
  • Comment #7 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Filamu hii haina kitu kipya.

    Kabla ya sangara, umalaya, ufukara,uvutaji wa bangi nk ulikuwepo Mwanza, kama ilivyo sehemu nyingi nchini (hata nje ya Tz) ambapo kuna mzunguko mkubwa wa fedha na tofauti za vipato katika jamii. Hata Dar kulikuwa na sehemu kama Maggots, Skyway ambapo umalaya uliendeshwa hata zaidi ya yale aliyoonyesha "Bw. Nightmare"; ukienda dampo la Vingunguti utakuta watu wenye akili zao timamu wakitafuta kitu chochote cha ku-salvage kutoka kwenye taka zilizotupwa... wakati Dar hakuna Sangara!!

    Tatizo ni introduction ya sangara, ambao wamepunguza population ya samaki wadogo kama Sato, Ningu nk, ambao ndio chakula kikuu na pia chanzo cha fedha kwa wavuvi wadogo wadogo around Ziwa Victoria.

    Kuhusu shutuma za uwanja wa ndege Mwanza kutumika kama transit point ya silaha, nadhani hapo ndio serikali inatakiwa kufanya uchunguzi zaidi.

    Darwin's Nightmare ni sensetionalization ya mambo ambayo yamekuwepo Mwanza na sehemu nyingi duniani kabla ya kuwepo kwa Sangara (Mwanza)
     
  • Comment #8 (Posted by Jayjay)
    Rating
    kichwa kilichoandika hii makala si tu kimeenda shule bali kina uzalendo wa kweli.Mimi nafikiri JahKaya si mjinga kukurupuka na issue hii ya Mapanki ni kwamba serikali hii from where I am standing inafanya kazi nzuri lakini pia inapenda kuSpin mambo kama Mzee Blair wamegundua umuhimu wa kuwa kwenye front page kila siku ukitoa mkwala(threats) huu na ule.Sasa issue hii wameona vilaza wengi wa Bongo imewagusa ndio maana wameing'ang'ania miaka mitano ndio itakuwa kipimo cha kazi yao.
     
  • Comment #9 (Posted by Fatma)
    Rating
    Thank you for this impressive article. It has been to our leaders' advantage to hide the truth about our dear country. I think we all need to wake up and live in the current world standards. We still people starving in TZ although we have "kasi mpya"
     
  • Comment #10 (Posted by Fransisca Masika)
    Rating
    Makala yako haina maana hata kidogo,,Umeiona hiyo documentary kweli wewe???inatudhalilisha.yaani amewatumia watu wajinga wasiojua hata Lugha,,masikini wa mwisho katika nchi hii,alitakiwa achanganye hali,,inaonyesha ubaya tu wa Tanzania.kwani hamna vizuri???umesikia kiingereza cha walioshirikishwa??mi naona nia ilikuwa ya kutudhalilisha zaidi badala ya kutusaidia.Ukiiangalia kwa makini ina vitu vya ujinga ujinga tu,,sijui watoto wenye mguu mmoja,chokoraa eti na wasichana wanaofanya ngono na marubani wa ndege.it does not make any sense.Nashangaa kwanini na wewe umeizungumzia.Hata nchi za dunia ya kwanza nahisi hawaijui,HAIELEWEKI kwa ufupi.mh Jakaya Anyamaze na wewe pia unyamaze,huu ni upuuzi wa kuuandikia makala.nilipoiona kwa mara ya kwanza kidogo mimba itoke kwa hasira.Nahisi walioshiriki kama walipewa kitu kikubwa sana ni chakula kama malipo ya kushiriki kwao,,wakaona masifa kuchukuliwa na video wakidhani watakuwa maarufu kumbe upuuzi na kujidhalilisha na kiingereza chao kibovu.
    asante

     
  • Comment #11 (Posted by Adelard)
    Rating
    Kwa kweli hii ni moja kati ya makala nzuri kabisa mwaka huu. Tena ni kweli tupu na haipingiki. Endeleeni kumfungua macho kikwete kwani anataka kutufunga macho kwa kuongelea mambo yasiyo na msingi.

    Nadhani sikuzijazo hatokuwepo mtu wakuhoji wanayoyafanya. Kwani elimu yenyewe hawataki kutupa. Mikopo ndio usiseme
     
  • Comment #12 (Posted by Jida)
    Rating
    Hapa mwandishi nakusifu maana umesema mambo ya kweli na hii ndiyo inafanyika nchini hapa. Kitu kinachoniuma sana ni wananchi wengi kuwa mbumbumbu sana kiasi kwamba kiongozi wa nchi akitokea kulalamikia jambo hata kama lina ukweli akalisemea uongo kidogo wanamuunga mkono bila kuchambua ukweli. Wanasiasa wa Tanzania wamezidi sana kwa kusema uongo na hii imetufikisha hapa tulipo, katika dimbwi la umasikini.Fikiri wanasiasa uchwara wa Mwanza walivyo organise maandamano kupinga hata ukweli huu ili mradi waonekane wanam support Rais wao na watu kwa kutojua wakaingi katika lakini cha ajabu mapanki ni kweli wanakula.Shida ni elimu kuwa duni tu si kingine.
     
  • Comment #13 (Posted by Genevieve)
    Rating
    First and fore most thanks to Habari Tanzania.com.
    President Kikwete, this should kindly come to your attention. Its your high time you get back to you cracking table and get the resollunion of every negative movement parteining Tanzania. As am writting a line here some one is watching the "CHILD LABOUR AT MERERANI FILM" Really, in General where are we heading too?? do you know how much this people from over seas might talk behind you when you go there for official/presidential duties?? In general we are really suffring. Again say thanks to God the Darwin's nightmare film was launched as one of Tanzania wekness has been revealled its only for you as a president to find the resollutions positively and Not negatively. My beloved young sisters and brothers are really suffering at Mererani yet we people who are staying in urban areas end up boosting yet forgetting the tears of our fellow siblings who are suffering out there. Really shall God ever forgive us?? Not the poor people who provide this jobs to the kids they are the so named Tycoons of Tanzania who owns Migodi there yet their children pursuing their academic studies out of the country.
    Papa Kikwete, its only when we accept the realities thats when we will find peace.
    Have a honorable day.
    An BAE Student- Genevieve
     
  • Comment #14 (Posted by Julius Mganga)
    Rating
    Well written and analysed
     
  • Comment #15 (Posted by DELLA)
    Rating
    hey we uko wapi??
    unastahili zawadi mwankwetu khaa
    mi nashangaa ni kwanini watu hawataki kukubali ukweli??jamani wa tz tubadilike na tukubali ukweli!!!!kwanza tuanzie na hao ma rais sijui viongozi watajua wenyewe!!mi nachoka!
     
  • Comment #16 (Posted by anonymous)
    Rating
    sentesi ya mwisho imemaliza kila kitu
     
  • Comment #17 (Posted by Bwana M ikaeli)
    Rating
    Bwana M ikaeli

    Salaam na pole na kazi mimi ni mtanzania ambae kwa sasa nafanyia
    shughuli zangu nchini Afrika kusini sijaelewa hasa maana ya hii mail
    kuhusu ile senema ambayo mimi naamini ni yakishenzi na huyu muandishi
    wenu alie huko Canada nacho jaribu kusema hapa ni nini ni kuwa raisi
    angekaa kimya au. Mi namuunga mkono amuheshimiwa raisi na kama kweli
    tuna uzalendo na nchi yetu nadhani tulitakiwa tuwe na raisi wetu. Huyu
    bwana ambae yuko Canada sijui kama amesha wahi kufika huko mwanza ambako
    ndio kuliko lengwa na hayo yaliyomo yote hayana ukweli wowote.
    Mheshimiwa raisi alikuja juu hasa kwa ile kashfa ya kuingiza siraha ile
    ni ishu kubwa ambayo inaweza pelekea kutokea vita kati yanchi na nchi.

    Naomba tuwe makini kabla ya kuanza kupinga kila jambo ambalo viongozi
    wetu wanafanya. Na tuwe wazarendo hata tukiacha kufikilia raisi kasema
    nini lakini sisi kama watanzania tunahaki zote za kuisimamia na kutetea
    nchi yetu.

    Mungu ibariki Tanzania

    Asante.
     
  • Comment #18 (Posted by washawasha)
    Rating
    rais acha utoto na huo mpira sisi tunataka maendeleo wewe kupitia real madrid ukiwa safarini kuelekea Cuba sisi haitusaidii ki2,barabara bora,huduma nzuri kwa jamii hospitali,mashule,maji safi,umeme ndio tunavyovitaka
     
  • Comment #19 (Posted by joseph mashauri)
    Rating
    Ndugu wananchi fungueni macho,mimi ni mwana ccm ,lakini naona watanzania tuna rais mzuri machoni ,tatizo anapenda kuvipa attention mambo amayo anaamini yanavutia hisia za watu,mfano hii ya mapanki,kuzunguka misibani,mahospitalini,mpirani,masokoni, yaani ilimradi ni yale mambo ambayo mwananchi wa kawaida ataona anajali well ni vizuri lakini tungefurahi zaidi angepoteza muda wake kutekelrza sera za ajira,tena inayoendelea kuathiriwa na mgao wa umeme .,kutekeleza miradi endelevu ya umeme,uchumi ,kwa nini tunaambiwa shilingi inashuka kwa ajili tuna exports kidogo ilhali dhahabu inasafirishwa kama udongo kwenye makontena kila siku wambeya wanasema projection za kweli za mauzo ya madini nje kwa mwaka zisizoripotiwa kwa wadanganyika{watanganyika ni dola billion 10 tunaambulia 3% ya zinazoripotiwa na 200,000 kwa halmashauri,,mh mkono aligoma kuzipokea ..hawa ndio watu wanaoona mbali.. kama mauzo ya nje yangeripotiwa yote maskini shilingi yetu ingekuwa imara zaidi ya majirani zetu,,,hilo ndilo moja ya mambo ambayo JK hajaona haja ya kuyapa attention,,,elimu yetu duni na wana vyuo wasiokua na uhakika wa kikopo,,,tena wa familia masikini,,nani wa kuwatetea,,wakati watoto wa wakubwa wanaosoma academies na kununua mitihani ndio wanaopata divition one ,na kunufaika na mikopo wasiyohitaji,,matunda yake ni kupata madaktari na wataaluma wasio na wito na wasiojali masikiniangalia utu wa madaktari siku hizi ulivyoshuka ,wasnabakia kugoma na miziki juu, ndio haya ndio mambo ambayo rais wetu hayaoni anaona mepesi ya kuchota umaarufu kwa asilimia 80% ya wananchi ambao hawawezi kuchambua mambo kwani sanasana wana elimu ya msingi na wanaishi vijijini ,.hawakuelewi ukiwapa uchambuzi,,na wle wasomi wachache wanaona lakini wanasema mtumikie kafiri upate ujira wako,,,si ndio ,sasa je utakula wapi!!
    nawapongeza erndeleeni kuelimisha watu ,,rais wetu hana jipya amebakia kurudia rudia manenoyule mwimbaji wa salamu mjomba anasema ;maneno mengi hayajengi gorofa!!! si utani ana maneno matamu kama sura yake rais wetu.

    jamani tujielekeze kuleta mapinduzi ya kiuchumi ,jana vijana 400,000 wamemaliza la saba ,masikini watakao endelea seko hawazidi laki ,,,laki tatu wankuja uwaja wa fisi na kwingineko kutumikia utumwa wa ngono ndio,,,hatuna muda wa kuwafikiria ..
    ajira milioni moja kwa mwaka ziko wapi ,,sekta ya kilimo ingeboreshwa na tupate masoko tungeweza mfano viiwanda vyetu vinaagiza mawese nje ,ngano ,shayiri wakati tunayo ardhi hilo ni soko tosha lakini wapi ,,hakuna ajira ,,jana lowassa kaenda kigoma kakuta matrekta saba 7 mkoa mzima ,,tena moja bovu,,suluhisho kamuagiza co simbakalila ,mkuu wa mkoa aendeshe mkoa kijeshi,,wananchi wadanganyika wakapiga makofii..alamsiki!!!!!!!!!!!!!!!

     
  • Comment #20 (Posted by Leonard Akaro)
    Rating
    Nchi yetu ni ya demokrasia. Tutumie uhuru tulio nao kupeana habari bila aibu ali mradi tuwe na nia njema na Taifa Letu. Hingereni sana
     
  • Comment #21 (Posted by Jabir Idrissa)
    Rating
    Muandishi amejitahidi kuzidi kuweka wazi mambo ya kuchekesha yanayoikumba nchi yetu. kwa hakika amefanikiwa kumfundisha utendaji kazi Rais JK. ni kweli badala ya Rais kumkasirikia H. Sauper, apange mikakati ya kuondokana na hayo machafu yaliyoelezwa na wananchi wenyewe wa Mwanza na kanda ya Ziwa. Ukweli ni ukweli na utabaki kuwa ukweli hata kama kutakuwa na vitisho vya mtutu wa bunduki. Maandishi yapo Ukutani, hayafutiki.
    Tunapaswa kuendelea kufichua kwa upana zaidi machafu yanayotendeka nchini petu. Wala tusiogope kutishwa na mtu kama Rais. tukiyaachia machafu bila ya kuyasema, historia itaja kutuhukumu.
    Masalaam.
     
  • Comment #22 (Posted by Mwinyi)
    Rating
    Mheshimiwa asione soni kutaka ushauri wa kitaalamu hata kutoka kwa wapinzani kama vile Prof. Lipumba kwa matatizo makubwa yanayoikabili nchi (Umeme, Inflation, UKIMWI,uharibifu wa mazingira, Elimu mikopo ya vyuo vikuu,corruption n.k, n.k). Matatizo haya yanatatulika kwa sharti kuwa tuwe wakweli na serious with issues and not cheap party platform politics.
     
  • Comment #23 (Posted by guydon)
    Rating
    That's 100% TRUE I have been to Mwanza and Musoma, I have seen through my two eyes people they are doing like the articles saying.
     
  • Comment #24 (Posted by mbise)
    Rating
    Ilimradi huyu mtegeneza filamu hii alichokisema ni ukkweli mtupu basi hana hatia. Na kwetu sisi tuachane naye na tukazane oh sorry neno tukazane si zuri tujitahidi kurekebisha hayo maswala yaliyojitokeza kwenye hii filamu bila kumfuata mtengenezaji. Yako mambo mengi ya kushughulikia yenye immediate impact kwa uchumi wa tanzania eg madini, ememe, utalii nk.
     
  • Comment #25 (Posted by mrs issa)
    Rating
    the article is very good na huyo alietoa hiyo documentary was very right kwa nini afiche ni vizuri atoe ukweli labda itasaidia kuibadili tz sasa...na rais asipoteze muda sasa apiganie kuiweka sawa ili hata hao watu wakija kuiaangalie wakute mabadiliko
     
  • Comment #26 (Posted by naomi)
    Rating
    Ukweli huuma na kuukubali inakuwa vigumu,anapaswa kukubali ili arekebishe makosa yaliyokuwepo na yanayo endelea. Nchi nyingi ambazo ni maskini wanaacha ukweli uwe wazi ili wapate msaada lakini tukika na shida zetu wenyewe ati kwsababu ya aibu,WALE WASIO JIWEZA WATASAIDIWA NA NANI ILIHALI VIONGOZI WANAONA AIBU KUWEKA WAZI MAMBO YANAYO ENDELEA? Wanainch ni watu muhimu,they are the ones that elect you and you promise so much that you wil do for them but after you get what you want you forget them and you leave them SUFFERING. Kuhusu mapanki, ni ukweli mtupu. Tuachane na hayo, wanafunzi wengi sasa wana elekea kumaliza shule, wata kwenda wapi wakati ajira walizo ahidi hakuna. Ina huzunisha sana kuona majambazi wanakuwa wengi,wasichana wadogo wana jiuza ovyo ili kupata riziki. WANANCHI WANAKUFA NJAA LAKINI CHAKULA KINAUZWA NCHI ZA NJE, ukikaa chini ufikirie kitu cha kujivunia nchini unashindwa useme nini kwa sababu ni shida tupu.
     
  • Comment #27 (Posted by Fun Safaris)
    Rating
    Thanks again to Habari Tanzania.
    I was just going through the comments which have been submitted by my fellow Tanzanians so far.
    Where is this BAE Student Genevieve?? for sure i was touched by her words. As she said "Papa Kikwete, its only when we accept the realities thats when we will find peace". I wish if the all the Tanzanians had the same feeling as for that student. My questions are, where do we belong??? where are we heading to?? Room for the changes is still there as it is still early.


     
  • Comment #28 (Posted by Genevieve)
    Rating
    My appreciation again goes to Habari Tanzania.com.
    Its till when we all get to hear our beloved president has made some changes thats when we will settle our Mind. Am a typical Tanzanian but taking my studies out of the country, normally during the one's country partriotism debates arise here i dont get peace at all, all the students do provoke me as per the Darwin's night mare film, some even extend their tongues and tell me "besides your studies here, we guess you also enjoy the fresh food which the school provide as we know Tanzanians are dying there of hunger- or else some feed on the rotten bones of nile perches" For heaveny sake, i have lost my peace of Mind completely. can any Tanzanian help me out there?? In the same school which iam, am schoolinh with one of the Tanzania minister- she was boosting there before that her Dad is a minister of..........I swear this to you now she has swallow her pride completely.
    I want to assure president Kikwete and the Tanzania Government that we want peace while we are out here. We are being undermined, we feel as if we belong to unknown planet apart from this earth. We are really working hard with lots of determination only to make a good tomorrow for our country- But how will this tomorrow be without the help of our leaders?? Please i dont mean to be a pollitician but all i know at the end of each dark tunnel there must be a light- kindly pass us through to this light for we are already fedup with this darkness which we have been for so many years.
    BAE STUDENT- GENEVIEVE
     
  • Comment #29 (Posted by Mohamed Sleyim)
    Rating
    Ni kweli kwamba Mh.JK amelishupalia suala la kudhalilishwa kwa Watanzania ndani ya flm ya Darwin's Nightmare,ikiwa ni sehemu moja tu ya mengi anayojihusisha nayo katika kunyoosha maovu yaliyofanyika katika kipindi cha nyuma.Sioni sababu ya kumshambulia Rais kwani serikali yake inajishughulisha na kuboresha maisha ya Mtanzania.Katika kipindi kifupi JK ameshughulikia na kwa kweli serikali yake inaendelea kukaa pamoja na wadau mbalimabali katika sekta za madini ili kupata mrabaha wa maana,anajituma katika kuboresha maisha ya wakulima na wafugaji kama unafuatilia hotuba zake,na anafanya mengi katika kuleta maendeleo ya wananchi.Nataka kumuelewesha mwandishi wa makala kuwa hapa Sauper pamoja na kutafuta rizki na sifa za tuzo za filam hakutakiwa kuongopa kuwa Tanzania ni mahali panapotumika kusafirisha silaha kwa madhumini ya kuendeleza vita.Hapa hatuna Charles Taylor au Savimbi.JK kuudhika na kitu kama hicho ni halali kabisa.Ukahaba hauko Mwanza tu,lakini degree ya ukahaba iliyoko Mwanza kwa namna yoyote ile haiwezi kulinganishwa na huko Majuu.Kumwambia Rais kuwa ameacha baadhi ya watu wabovu waliokuwa katika Serikali iliyopita nadni ya cabinet yake ni kauli ya kubahatisha na haina ukweli ndani yake.Katika kuteua baraza la mawaziri Rais alifuata vigezo na sifa za wale alowateua.Haikutosha aliwapa miezi sita kuonyesha utendaji wao ama sivyo wasje kumlaumu.JK,hawa wanaokupima kwa kigezo cha Darwins Nightmare nadhani ni vijana ambao hawajakomaa bado,wana haraka ya kuona matokeo ya uongozi wako katika muda mfupi sana,jambo ambalo katika uongozi si rahisi.JK,endelea na juhudi zako sisi wenye macho tunaziona.
     
  • Comment #30 (Posted by Peter Lwegasira)
    Rating
    Nthelezi Nesaa ni kati ya watu wengi wenye nia nzuri na nchi yetu. Nakumbuka nilisoma mahojiano ya Sauper na mwandishi wa makala katika gazeti la Mwananchi mara tu baada ya swala hili la filamu kujitokeza tena. Yeye alisema hivi "Kwa anayesema ile filamu inaonyesha uongo au inaonyesha ukweli, sharti awe ameiangalia mwenyewe na siyo kusimuliwa na mtu mwingine" Tuwe wakweli. Je tumeiangalia kwa macho yetu mawili au tumesimuliwa na kusoma kwenye magazeti tu?

    Jibu la swali la mwisho la Nthelezi Nesaa linatuonyesha kuwa kuna baadhi ya vitu lazima viendelee kusimamiwa na serikali moja kwa moja. Hili siyo swala geni na madhara ya kutokufanya hivyo ni makubwa. Serikali ya sasa isisubiri yatokee. Tuna imani nayo kwamba inaweza.

    Peter
     
  • Comment #31 (Posted by Eng Msafiri)
    Rating
    sauper did commendable job
     
  • Comment #32 (Posted by mashaka)
    Rating
    Kweli wajinga ndiyo waliwao. naona kuna watu wanamshutumu mwandishi na mtengeneza makala! Kweli mwenye mapenzi haoni. Badala ya kumpongeza mwandishi Ntelezi nesaa kwa kutoa mchango ambao si rahisi kuuona kwenye vijarida vyetu, watu wanamshutumu. tunampa tafu aendelee kuwapa vidonge vyao.
    Jakaya anaanza kuonyesha rangi yake halisi na urembo wake kwa kasi mpya nguvu mpya na ari mpya.
     
  • Comment #33 (Posted by lilian)
    Rating
    ukweli rais ashughulikie mambo yenye kukatisha watanzania tamaa na si kuvalia njuga jambo ambalo ni la siku nyingi na la kweli.ahsanteni kwa kuwaonyesha watz ukweli.
     
  • Comment #34 (Posted by grace)
    Rating
    its very true,keep on
     
  • Comment #35 (Posted by Steven Ndosi)
    Rating
    I appreciate this "makala" it tells a lot of truth and tanzanians should wake up. There are so many "keros" which our leaders should look at instead of wasting time on things that are very open and real.
     
  • Comment #36 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Ninapenda kwanza nimpe hongera mh. Rais kikwete kwa kazi anayofanya. Ninafahamu wazi kuwa kila mtu anao uhuru wa kusema na kutoa maoni yake, ila haya maoni ya kukushambulia wewe Rais kuhusu kipengele cha TZ kutumika kama sehemu ya kupitishia silaha umefanya vema. Huyo anayelichanganya swala hili na minofu ya samaki kuzalishwa sehemu chafu ana anachanganya mambo mawili na anachanganya vichwa vya wa-Tz. Mimi sitegemei wewe kuleta mabadiliko lukuki ktk uongozi wako kwa muda huu mfupi ila kwa jinsi ulivyokwisha kuanza kufuatilia mambo yote makubwa na madogo nina imani jahazi litasogea kwani sii rahisi lifike ktk kipindi kifupi cha uongozi wako utakokaa kadiru Mungu atakavyokujalia. Wale wanaotaka uangalie mambo makubwa makubwa tuu ya nchi usahau hayo madogo anakudanganya, kiaongozi anayeona mbali ana uwezo wa kufanya mambo yote pamoja wazungu wanasema "intergration" ndio kiongozi anayejishughulisha na matunda yanaonekana. Songa mbele mh. Kikwete usife moyo na lawama ndogo ndogo songa mbele daima kwani kama raia pia unayo maoni yako kuhusu mambo mabaya dhidi ya nchi na mimi naheshimu kauli yako ya kupinga kuwa TZ niantumika kama sehemu ya kupitishia silaha za kivita kwa mataifa jirani. Hiyo ni kashifa hata kama hukuijibu ukiwa waziri wa mambo ya nje naridhika na kuwajibika kwako kuijibu ukiwa kama rais kwani hata kama ungeijibu wakati ule ukiwa kama waziri hawa watu wangekupinga pia kwani hawaoni baya hapo hata sasa pamoja na muda wote huo waliokuwa nao kutafakari hili swala. Jamani tuache kuandika mambo tushitukapo toka usingizini.








     
  • Comment #37 (Posted by cecy)
    Rating
    jamani rais aangalie vizuri hii picha yaliyoonyeshwa yote ni kweli kama wale kina mama walivyowachafu na mavunza wanafanya kazi kwa shida sana!!! kwani wenye kiwanda hawaoni hayo!! Je wanamazigira wanasemaje??? rais peke yake hawezi kufanya kazi watu wamefumbia macho wenye kazi zao !!!! mambo ya ten percent yaho!!!!hayataisha rushwaaaa!!!!!!!!!!!!!
     
  • Comment #38 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Hey! hongera bwana eebwana hii ni kipindi cha mabadiliko. umeelezee vizuri. nimesoma leo ila naomba nikupe hongera zako.
    A town.
     
  • Comment #39 (Posted by an unknown user)
    Rating
    UKWELI UNAUMA NA LAKUFANYA SIO KUKANUSHA BALI NI KUTAFUTA NJIA YA KUTATUA MATATIZO KWANI AIBU TUBU.
     
  • Comment #40 (Posted by Dungunyi)
    Rating
    There are more serious things for the President of the country to deal with. Not this. I think we have to adhere to Mwl Nyerere that "Rasilimali zetu zitabaki kuwa chini ya Ardhi yetu mpaka pale tutakapokuwa tayari kuzivuna sisi wenyewe kwa maslahi ya taifa letu" rather than bosting ouselves that TRA has boosted monthly tax collection to 229 bil shs a month. Do we real know how much they harvest from our resources? The country leaders should understand that they turn investment policy to harvesting policy not unknowingly but for their own benefits.
     
  • Comment #41 (Posted by sambe)
    Rating
    huenda bw. jk ameghafilika kwamba suala hilo angeweza kulikabidhi kwa wizara husika nae akashughulikia ambayo yana umuhimu zaidi ya hilo.

    kwani si afadli huko mwanza wanaweza hata kuzungumziwa kulilo kule kigoma ambako kumesahauliwa kabisa utadhani sio Tanzania ni bora tu wawape mamlaka yao wenyewe wawe na sirikali yao. Kuna bandari,reli,kuna mipaka lakini hakuna uhai mkoa mzima una madaktari wawili tu wakati madaktari wapewa ubalozi.

    Hivi bw. jk anatambua kwamba kuondosha Daktari mmoja ni sawa na kuuwa watu wangapi? ambao huyo Daktari angewahudumia?
     
  • Comment #42 (Posted by Kimbau)
    Rating
    Hongera mwandishi kwa uchambuzi wa kweli. Waandishi wetu hapa nchini hamna budi kueleza umma ukweli. Kutumbukia katika ushabiki wa kisiasa (uanamtandao) na kusahau wajibu wenu, ni kosa kubwa kwa umma wa Tanzania ambao historia haitaacha kuwasuta. Mie nimeiona hiyo filamu. Inadhalilisha lakini kwa wale wenye kufanya uchambuzi wa kina na hasa wale waliotembelea viwanda vya samaki na Mwanza yenyewe, hakuna cha kulalamika. Tufanye kazi kuondoa dosari zinazotupaka matope nje kwani utendaji unapimwa kwa vitendo na si maneno matupu. Sioni kwa mfano ni kwanini, baada ya miaka arobaini na tano ya uhuru nchi bado inatumbukia kwenye giza na bado tunaona si janga. Pia, ni kwanini tunazidi kuwa soko la viwanda vya mataifa mengine (hasa nguo na bidhaa za kilimo)? Kuoneana haya, kumepitwa na wakati. Mapinduzi ya kiuchumi Asia ya Mashariki na Uchina hayakuletwa kwa kuoneana haya. Kama vyombo vya habari vya nje vinatoa "relatively objective opinion" na sisi waandishi wa hapa nchini tumekalia kupakana samli kwa mgongo wa chupa, tutaendelea kuandikwa na kutangazwa vibaya. Tuache kuripoti tu, tufanye uchambuzi pia.
     
  • Comment #43 (Posted by Madakomulume)
    Rating
    Nimechoka kabisaaa. Yaanini kuna watu wanaweza kuunga mkono hiyo hotuba ya Kikwete? Mwe! Tanzania tuna safari ndefu. Hebu ninyi mnaodai mmezalilishwa mtueleze, watu hawali mapanki? Hao malaya hapo makoroboi hawapo? Ukimwi kwenye visiwa hakuna? Mmedhalilishwa vipi? Documentary hii imeshinda tuzo za kimataifa, mnadhani hao watoaji wa tuzo ni wababishaji kama watoa tuzo za Kilimanjaro music award?
    Badilikeni Watanzania. Rais wenu alichemka vibaya mno kwani asilimia tisini na tano ya yaliyomo humo ni ukweli usiopingika isipokuwa kwa mtu aliye na maslahi na hiyo hotuba ya Kikwete.
     
  • Comment #44 (Posted by Loota L aiser)
    Rating
    Aisee kumbe watu wengine hawavikirii kabisa. Mimi ni Maasai kutoka Monduli, Wazazi wangu ni wafugaji kidogo na wakulima pia kidogo. Sometime tunauza maziwa ya ngombe na tunajua kuwa ile ni biashara. Hivi kama mtu akija kuniambia kuwa maziwa yako ni mbovu yanatoka madudu au unaongeza maji, nisimshitaki au nisilalamike eti sitaki kupoteza muda. Je hujui kuwa biashara ni pamoja na kulinda mazingira ya ushindani? Hata kama unafanya hayo machafu je ni vema kujulika siri ya biashara yako? We mwnandishi inabidi ukasome tena maadili ya uandishi. Pia Nashauri waandishi wa habari wawe wanasoma some la uchumi na ujasiriamali ili waweze kutofautisha nyakati na biashara. Umeboa sana hapa.
     
  • Comment #45 (Posted by Anonymous)
    Rating
    What we dont see is that despite these and other good opinions from well-meaning people, nobody cares! do you really think the Pre is going to give a damn to your advise? lets face it, this country is rotten..the current 'madawa ya kulevya' issue is proof of that!
     
  • Comment #46 (Posted by Nata Kaputura)
    Rating
    It is true, but everyone has the right to put priorities. Anything undermining a person even if it is true 100% is not acceptable be in the super first world or the last third world. There are several issues worldwide that needs attention more than this one.
     
  • Comment #47 (Posted by D.K.Mwenda)
    Rating
    Sipendi japo kwa leo tu kusema alichokemea rais juu ya filamu hiyo ni sahihi au la. Sijaiona filamu, lakini kama upo ukweli wowote kwa yaliyooneshwa jibu lake ni moja tu yaani kurekebisha kisha Bw. Sauper apate tuzo ya pili na Tanzania ipate ya kwanza.
    Hata hivyo alichoandika Bw. Joseph Mashauri kuhusu vipaumbele, yafaa kuzingatiwa na wakubwa yaani UMEME, UKIMWI, INFLATION, RUSHWA, MAZINGIRA NA ELIMU.
    Rais amemudu vizuri kushughulikia UJAMBAZI. Tunasubiri kutoa BRAVO kwa japo matatu kati ya yaliyobaki.
     
  • Comment #48 (Posted by AMINAWAZIRIJUMARICHARDS)
    Rating
    All is more than true , hey hang on what about as well as prostitutes big shots too, strife for power in using the powers of darkness!will we trully reach anywhere?hk0z1v
     
  • Comment #49 (Posted by Joseph Bainomugisha)
    Rating
    Nashauri hii article itumwe na ichapishwe kwenye gazeti la RAI hapa Tanzania ili wasomaji wetu waione maana ndilo gazeti makini linaloweza kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania walio wengi.
     
  • Comment #50 (Posted by an unknown user)
    Rating
    uongozi bora unatumia mipaka yakikatiba,kiongozi anayependwa sana na watu wake na watu wa nje kumsifu ,ujue hapo kuna tatizo ,naomba sana watanzania tuelezane ukweli kabala ya nchi hii haija chukuliwa na wageni na wenyeji kutupwa baharini .nyerere huko aliko anashangaa sana ijapokuwa tunaimba kuwa ni baba wa tifa ,hongera na muendelee kuchambua mambo yote
     
  • Comment #51 (Posted by araxy)
    Rating
    Ni aibu viongozi wetu hujiingiza na maswala ya mtaani badala ya kutatua matatizo ya taifa. Angalia swala la rose garden !!!
     
  • Comment #52 (Posted by an unknown user)
    Rating
    DARWIN NIGHTMARE IS A GREAT DOCUMENTARY IF YOU CANT STOP POVERTY MHE. JK POVERTY WILL STOP YOU!!!
     
  • Comment #53 (Posted by Nyundo Mohamed)
    Rating
    Ni Documentary nzuri,imeandikwa na mtu ambaye anajua records, Inaonekana viongozi wetu wanaongea Mambo bila kujali maslahi ya wanyonge, bali kutetea maslahi yao binafsi,kwani wao ndo hufaidika kupitia manyanyaso ya wanyonge. mwisho wao utafika tu.
    hongera muandishi
     
  • Comment #54 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Kamata tano mwanangu, umepiga ikulu
     
  • Comment #55 (Posted by Joab)
    Rating
    Msanii yule alikuwa na nia ya kuandika kitakacho wagusa Watanzania na Jamii ya Dunia kuhusu Maisha ya watu walio wengi hasa Africa, Nafikiri lengo lake ni kuwa
    Maarufu, kupata fedha nyingi,Kushinda na kutoa kazi nzuri itakayo futa watanzamaji wengi kwa wakati husika.
    Riwaya nyingi zimewaudhi sana watawala,ili kuitetea nchi ni lazima Mkuu wa nchi husika atoe msisimamo wake.
    Ni vizuri rais wa nchi ameona hili.Akisema wananchi wa Tanzania wamesema, Mtanzania anayeishi Canada akisema ni yeye pekee yake kasema.Rais wa Tanzania akisema maana yake watu wa Tanzania wamesema.Nachukulia waliompigia
    kura (majority) Wamesema ndani ya miaka 5 kauli yao ni sahihi si vinginevyo.
    Yule Mzungu kwanza nia yake ni Kutufuruga,Kutuchanganya, kutudharau,Kutunyanyasa, na kama hatuwaoni Dada zetu wakifanya mambo ya kipuuzi tukawaacha pale maggot , Masenze, na Kwingineko Tanzania, hawa wako ndani ya nchi yao, wamejificha na vazi la nzuri la nchi yao ili watu wa nje wasione uji wa watu hawa. Inapofika Kichaa mmoja katoka nje ya Tanzania na Kupora nguo za hawa Wanzania ili waonekane na watu walioko nje ya nyumba yetu ni aibu yetu sisi tunaoona Nchi yetu imenyang'anjwa nguo na tunaficha nyuso zetu.
    Wale ambao ni wa nje ya nchi hii wanafurahi na kukuza hali ile.Ni upuuzi, na lazima nchi yetu itamke na kumwonye huyu mshenzi kwamba alichotoa ni Kinyume cha maadili hapa Kwetu.Rais wetu hana mpaka kwa mambo ya kisheria.Kwa kusema hajavunja wala kukosea na wala mada, si jinai, amesema, anawajibika kufanya vile
    Na kuyazungumzia yote yanayomzunguka.
    Watanzania tulinde nchi yetu kwa nguvu zote.
    Ansate
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  3. Is Tanzania a safe place to invest?
  4. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
  5. Nitaendelea kugombea nafasi za kisiasa- Balozi Karume
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Linda Garner
  4. Nthelezi Nesaa
  5. Marshy Abdu
  6. Prosper Kwigize
  7. Salehe Mmoro
  8. Ramadhan Semtawa
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.