Filamu mpya kwa jina la Gem Slaves: Tanzanite's child labour imezinduliwa wiki hii Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Filamu hiyo inaonyeshwa jinsi watoto wanavyotumikishwa katika machimbo ya tanzanite Mererani na watoto hao kutokwenda shule na kufanya kibarua kama “NYOKA” jina ambalo utumiwa katika migodi hiyo.
Filamu hiyo inaanza kwa kuwaonyesha watoto wanne wapo chini ya migodi wakitafuta mawe. Moja wa hao watoto Wilson Peter ( Miaka 12) anasema “tunatelemka mgodini, tukifika chini tunaanza kuchekecha mchanga, muda mwingine hatupati madini njaa inatuuma hata tunalazimika kurudi nyumbani.”
Mtoto huyo anaendelea kusimulia “Tukishamaliza kula tunarudi tena kuchekecha changa mitaani, ukifika muda wa saa kumi na mbili jioni tunarudi nyumbani. Muda wa jioni ukifika, tunabadilisha nguo tunavaa za nyumbani badala ya kuendelea na zile ambazo tunazivaa wakati wa kuchekecha mchanga. Tukishavaa nguo za nyumbani tunakwenda kuchota maji ya kutumia nyumbani, na tunamsaidia mama kazi. Usiku ukifika tunakwenda kulala.”
Filamu hiyo inaendelea kuelezea Mererani kama sehemu moja tuu duniani yanayopatikana madini ya Tanzanite na kwamba kila mwaka madini hayo huingiza fedha nyingi sawa na dola milioni 300 za kimarekani.
Wananchi wanaozunguka migodi hiyo bado wanaishi katika maisha ya kimasikini ya chini ya dola moja kwa siku. Filamu hiyo inaendelea kuelezea kwamba kila mwaka maelfu ya watu wanakwenda Mererani kutafuta hayo madini na Watoto ndio wanaofanya kazi kubwa.
Filamu hiyo inaendelea kusimulia zaidi ya wachimbaji elfu thelathini huenda chini zaidi ya mita 300 bila vyombo vyovyote vya usalama na bila msharahara wenye uhakika. Kila siku wachimbaji wadogo 4000 wa miaka kati ya 14-24 wanahatarisha maisha yao katika migodi hiyo isiyo na vyombo madhubuti, pia watoto hao hupata mlo mmoja kwa siku.
Filamu hiyo inasema, watu wanapoona tanzanite madukani wanaiona imependeza sana ila hawajui inapatikana vipi mpaka ikafikia rangi na mng’aro mzuri ilionao.
Wilson Peter ( Miaka 12) anasema anajua kwamba kunahatari anapokuwa ndani ya migodi na kwamba anaweza kuangukiwa na miamba mikubwa (gema), kupata ugonjwa wa kifua au kuteleza na kuanguka kwenye mashimo yaliyo na kina kirefu cha kutisha.
Mtoto huyo anasema haoni vizuri na busara kwa watoto kufanya kazi migodini kwasababu huwa wanatumwa tumwa ovyo kwenda nje ya shimo, kuleta soda, kuchukuwa tindo ya umeme (jack hummer) na yeye bado ni mtoto.
Mtoto mwingine Mutasi anasema yeye alikua akifanya kazi kama nyoka, akaacha kutoka ana na ugonjwa alioupata wa kifua na siku nyingine anashindwa kula chakula cha mchana. Aliacha yeye peke yake akawacha wenzake zaidi ya 50 bado wakiendelea kufanya hiyo kazi mpaka sasa.
Alikutana na fundi moja aliyekuja katika mgodi kutengeneza mashine na huyo mtoto akamueleza fundi tatizo lake. Fundi akamua kumfundisha jinsi ya kuwa fundi wa magari. Sasa anajifunza kazi za karakana na baadaye akisha kuwa mkubwa anategemea kufungua karakana yake na kufundisha watoto wenzake kama yeye alivyofundishwa.
Mama Peter ( Mama wa Wilson Peter) anasema “kwa kweli wanavyochekecha mchanga huko migodini hatufurahi, ila wanachekecha kutokana na shida iliyopo hapa . Maana watakapopata shilingi 200 au 300 wanaleta nyumbani, wananitupia hapa nami inaniwezesha kuendelea kuwalea. Na mimi nikihangaika kuuza mboga inawasaidia kuendelea kuishi”
Mama Peter anasema “Ndio maana tunawaruhusu, wakisema wanakwenda kuchekecha hatuwanyimi maana kila mtoto anabahati yake. Kwa kweli wanavyohangaika tunawahurumia lakini kutokana na shida tuliyonayo hapa inabidi tuwavumilie, tuwalee katika hii mbaya.”
Mwisho kabisa Wilson anasema “ Kama nikiwa Rais wa Tanzania sitaruhusu watoto kwenda kufanya kazi migodini na wale ambao watakamatwa wakitumikisha watoto migodini watahukumiwa kifungo”
Comments
Comment #1
(Posted by Avi Maly) Rating
I like the kids self expression in Swahili language. Can you make this film available in US and UK? If in Tanzania, where can I buy this film in DVD format?
Thanks so much for exposing of what is happening in develpoing world.
Avi Maly
Comment #2
(Posted by Steven Ndosi) Rating
Its a good teaching document in Child and human Rights Advocacy Courses. It reveals the truth about Mererani where many people think whoever goes there should become a millionaire.
Welldone
Comment #3
(Posted by gard mbigo) Rating
Hii ni kumnyika mtoto haki yake ya kupata Elimu ambapo ni kosa kubwa sana.
Comment #4
(Posted by Lwendo G.G.) Rating
AIBU!! Tumendamwa na filamu zinazotoa ukweli kuhusu Tanzania. Hatutakiwi kukasirika bali inatupasa kurekebisha.Tulisema vibaya sana na tukajikosha kuhusu Darwin's Nightmares, sasa kuhusu hili tutasema nini??
Waziri Msabaha Upo????
Comment #5
(Posted by Hope Gabone) Rating
Ni habari ya kusikitisha!
Huu ni ukweli ambao watanzania inabidi tuukubali, utumikishwaji wa watoto kwa njia yoyote ile ni hatari si kwasababu tu ya kwamba unahatarisha maisha yao ila pia kwasababu unakinzana na unapelekea watoto kukosa haki zao za kimsingi kama vile Elimu, kucheza, kupumzika, upendo na mengine mengi.
Ingawa watu wengi husema kuwa si rahisi kuzuia utumikishwaji kwa kuwa watoto husaidia familia zao, lakini ukilinganisha thamani ya shilingi 300/200 anayopata mtoto na kupeleka nyumbani na athari za kimwili na kiakili anazopata bado unaona hakuna uwiano wa athari na faida!
Kwa hiyo pamoja na kuwa familia nyingi masikini zitategemea hivyo vijipesa kidogo sababu ya umasikini, bado uwezekano wa umasikini huo kuisha haupo kabisa bali ndio matatizo huongezeka kwasababu familia itabidi zigharamie matibabu ambayo yako juu, vifo vingi vitatokea hivyo kupoteza rasilimali na matatizo mengine mengi!
Ni kweli Tanzania inabidi ifike mahali ithamanishe zaidi utu na maendeleo ya kila mtoto binafsi badala ya maendeleo ya familia nzima yanayotegemewa kutoka katika vijisente vinavyopatikana!
TAFAKARI...
Comment #6
(Posted by an unknown user) Rating
THIS IS BULL SHEET STORY, NOW IS TOO MUCH, YAANI WAZUNGU WATUCHUKUE PICHA KWENDA KUONYESHA KWAO, WATENGENEZE PESA SISI TUMEKAA TUU... HAWANA LOLOTE SANA TUNATAKA KURUDISHA UKOLONI HAPA TANZANIA.. KWANI HAO WANZUNGU WATUSAIDIA NINI!! WAKO WANGAPI HAPA NCHINI, ZAIDI YA HAPO WANATUNYANYASA TUU, HAWANA LOLOTE... HATA INGEZINDULIWA WAPI HAITOSAIDIA, KWANZA HAO NDIO MASHETANI WAKUBWA NA WALA TUSIWATETEMEKEE. HAPA NCHINI WANAKUJA KUTUSABAI TU WALA HAWANA LOLOTE. WHAT KIND OF THE GAME THIS PEOPLE PLAYING TO US?? WE SHPOULD THINK WISELY SIO KILA KITU WAZUNGU
Comment #7
(Posted by boe) Rating
kwakweli hii siyo haki kabisa yapaswa serekali iingilie hili jambo watoto wanateseka sana hawatapa elimu na omba omba hawataisha hapa tanzania !!!
Comment #8
(Posted by BONIFACE SHOO) Rating
Child labour sio kitu kizuri hata kidogo. lakini chanzo chake ni nini? ni vizuri sasa tukatibu chanzo cha shida badala ya kuhangaika na dalili.Umaskini uliokithiri upo kwa kila jamii hapa nchini mwetu.serikali yetu inafanya juhudi za kuondoa au kupunguza umaskini huo,lakini sisi kama wananchi (maskini) tunafanya nini? ukiangalia jamii nyingine zinakalia kucheza bao kutwa nzima,umaskini utaishaje? watoto nao wanaiga au wanaenda kutafuta maisha ile wapate kula!! Hizi ni alama za nyakati,zinapaswa kusomwa na wanadhimu na kutafsiriwa ipasavyo. wenzetu wa India wanafunga shule wakati wa mavuno ili watoto wawasaidie wazazi kuvuna. Child labour ikipangiliwa vizuri inaweza kusaidia kuondoa umaskini.Shida yetu ni umaskini,serikali peke yake haiwezi kuutoa,lazima ianzie kwa mtu mmoja mmoja.Tuliwahi kuambiwa kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe. Shule zipo (hata kama ni duni)mzazi anaachia mtoto akachimbe madini ili awe tajiri,tunailaumu serikali, sio sahihi.Hata kama serikali inawajibika lakini uwajibikaji huo uanzie kwa mzazi!! Sisi tulifanya kazi lakini tulisoma pia kwa sababu wazazi walitusimamia na serikali ilitupa shule hizo hizo za hali duni.Iweje leo? Filamu ni nzuri kila mmoja achukue nafasi yake ya kujiangalia na kujisafisha.Mzazi asimamie watoto na serikali isimamie sheria zake, hicho ni kioo tumepewa. samahani kwa wale nitakaowakera na maoni yangu binafsi.
Comment #9
(Posted by said) Rating
insikitisha lakini ni hali halisi.ni vyema kwa serikali kuimarisha na kusimamia suala zima la utumikishwaji watoto likomeshwe.hata hivyo serikali pekee haiwezi pasipo watanzania kuona ubaya wa jambo hilo .ndipo zinapokuja NGOs nyingi zinatumbua fedha za wafadhili bila kufanya kazi zilizokusudiwa
Comment #10
(Posted by ahmed noor) Rating
I cannot beleive that this kind of thing is happenning in Tanzania. But I also think that this exposure will make the Kikwete Gov't act very fast and very deligently as he is probably the best President Tanzania has ever had.
Comment #11
(Posted by akmsuya) Rating
Hao matajiri wanaowafanyisha kazi watoto hao wachukuliwe hatua au kiwekwe kiwango maalum cha malipo kwa kazi wanayofanya ukizingatia maneno ya yule mama kuwa japo watoto hao wanapata shida lakini hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.Inauma sana kuona watoto wadogo kama hao wanatumikishwa kwa kazi ngumu kiasi hicho.Naishauri serikali imiliki migodi hiyo na iajiri raia nakuwalipa mshahara kiwango kinachostahili.na si watoto wadogo wawe watu wazima.
Comment #12
(Posted by Klaus Collin) Rating
Hii ni sehemu tu ya ICE BERG, hali halisi ni mbaya zaidi. Kwa wale wanaotembea sehemu mbali mbali hapa nchini, mtakubaliana nami kuwa kwenye shughuli zote ambazo ni "labour intesive" e.g mashamba ya kibiashara (chai, kahawa, kakao) hali ni viyo hiyo. Kama wengine walivyo shauri, jambo hili yatupasa kubadilika. Tushughulikie ATTITUDE aspect of ourselves, and be more accountable for our lives, our nation and our future. Sorry for my Kiswa-nglish.
Comment #13
(Posted by Fabian Mesanga) Rating
Haya serikali ya Mheshimiwa Kikwete iseme tena kwamba huu ni uongo. Tatizo letu sisi watanzania tu hodari sana kuelezea ya wengine na kukataa au kukanusha yote ambayo hayatupambi. Hiyo picha/video inaonyesha ambavyo serikali haina taarifa kwamba kuna watoto wengi kiasi hicho mererani wananyonywa na kudhalilishwa. Tafadhali serikali iamke na kuwaokoa hao watoto ili wapate kuhudhuria shule kama watoto wengine na sasa kwamba elimu ni bure shule ya msingi. Tusikae kutafuta mchawi kwanza tunusuru maisha ya hao watoto. Kama tume itaundwa kama tulivyozoea basi iwe ya kutafuta namna ya kuwasaidia hao watoto na si vingenevyo.
Comment #14
(Posted by an unknown user) Rating
Sote tunaosoma na kuchangia katika hii article ni wangapi tunao watoto walioko katika utumikishwaji wa aina hii ama yoyote ile? Na je, ni nani anawajibika moja kwa moja kwa mtoto wake? Ni mzazi ama ni serikali? Na je sisi wenyewe tumekulia katika mazingira yapi? wazazi wetu walikuwa wakitulea vipi? Kwa kutwambia serikali itatusomesha au itatulisha? What is your basic role (as a parent or guradian) to your child(ren)? Samahani kwa wale ambao hawajapata watoto wa kulea.
Comment #15
(Posted by an unknown user) Rating
Sote tunaosoma na kuchangia katika hii article ni wangapi tunao watoto walioko katika utumikishwaji wa aina hii ama yoyote ile? Na je, ni nani anawajibika moja kwa moja kwa mtoto wake? Ni mzazi ama ni serikali? Na je sisi wenyewe tumekulia katika mazingira yapi? wazazi wetu walikuwa wakitulea vipi? Kwa kutwambia serikali itatusomesha au itatulisha? What is your basic role (as a parent or guradian) to your child(ren)? Samahani kwa wale ambao hawajapata watoto wa kulea.
Comment #16
(Posted by Chris Mwasambili) Rating
Imenifungua macho kuhusu child labour Tanzania na kunipa changamoto
Comment #17
(Posted by mwanagenzi) Rating
these are genuine problems facing our society as tanzanians, will the president, his excellency jk complain about this?that the un is deliberately tarning the good image of tanzania.
mr president you were misinformed abou the mapanki documentary, and you jumped into it while forgeting these serious underlying causes of poverty.think twice, we have trusted you to run Tanzania Inc, we expect profits.
Comment #18
(Posted by E.G.M) Rating
am not sure if this iz true. i think we need to work on this. if it's true, shame on us. On my opinion, serikali inatakiwa kuangalia kama huu mkanda ni wa kweli au ni usanii. Na pili, kuangalia kama hicho kitu kipo kweli huko mererani.a
Comment #19
(Posted by an unknown user) Rating
Watanzania tusiwe watu wa kukataa kuambiwa ukweli siku zote. Yaliyoonyeshwa na hii filamu ni ya kweli au uongo? Kama ni kweli tusifikirie hao wazungu ni pimbi kiasi hicho kuwa wataegemea kwa yale yaliyoonyeshwa na hii filamu tu, watkuja fanya uchunguzi na wakidhibitisha ni kweli wanaweza hata kuweka vizuizi kwenye ununuzi wa Tanzanite. Lakini kwa upande mwingine hii Tanzanite inalinufaishaje taifa kwa ujumla na vijiji vya Mererani? Lazima hatua za msingi zichukuliwe maendeleo yaonekane huko Mererani sio tu wanaachiwa mahandaki pasipo maendeleo ya aina yeyote yale. It is time to think positively and not negatively as we used to. UKIKOSOLEWA UMESAIDIWA SANA KWANI UNAPEWA MWANGA WA NINI MAPUNGUFU YAKO
Comment #20
(Posted by Emillian Rwejuna) Rating
The Govt need to look into this issue very seriously.
Comment #21
(Posted by Nuru A. Mabrouk) Rating
My comment is, Tanzania government is very rich, it supposed to make sure that all children go to school and any one who hire childred sentenced to jail
Comment #22
(Posted by EUSTACE MANG'ONDI) Rating
Trully,despite the fact that Darwin's night mere was very sad and really happening,this one is even more sad since it involve childrens who are below 18.
As the matter of fact,the employers due to this couse are suppose to be jailed,and the sentence is accompanied by corporal punishment.
Mush as I can Understand,there are rules and regulations (Local Laws)that governs the conduct of employers in Mining businesses.
I think let this to be the Challenge to the President of Tanzania,Mr.JM Kikwete as I am sure that he knows what is taking place out there.
Mr.Kikwete,these suffering Childrens are now crying for the help particularly Wilson in refering to his statement he said 'if he could one day becoms a President'.
I look forward ro hearing from the proper authorities soon.
Thanks very much.
Comment #23
(Posted by an unknown user) Rating
This is a good advocacy for child rights, but why should wazungu come and take those pictures, they will be making money in the name of development and helping Tanzania kids, there are many many problems in our country, some even worse than this, haya watanzania, lets wake up and conduct this advocay sisi wenyewe. NGO's za Kitanzania sio mnakula hela kwa manufaa yenu tu hii ni kazi yenu, kuhamasisha jamii inluding serikali kwa yale yanayotokea, jamani mpaka lini tutategemea wazungu na hao makabaila wa kitanzania ambao mko merarani na mnatumikisha watoto, aibu zenu, mnaweza kufanyia watoto wenu huo unyama, where is the media in Tanzania, Televesion mbona hamuendi huku mkaonyesha watanzania unyama unaotokea huko badala ya kutuonyesha picha za viongozi wakifanya uzinduzi, hatutaki kuona mazuri tu kwenye TV tunataka kuona uozo uliopo nchini kwetu pia ili tuwaamshe watanzania na tuwasaidie watoto wanaonyanyasika.
Comment #24
(Posted by Wakwetu Harisi) Rating
Jamani, lets not comment when you have not had an oppotunity to watch and listen to the film. Yes, the kid are being exploited, but who is responsible for that, its me and you Tanzanian. The film just shows the truth. Jamani Tuache lawama tuuuu lets do something. Just ask yourself how many children have you helped today to avoid going to such jobs. Its not that they like it social economic enviroment around them that forces them to do such jobs. listen to the lady from ILO. Ameleza vizuri. Tufanye kazi tukuze uchumi then we can adress such issues prudently. - SOrry for language mixup.
Comment #25
(Posted by Genevieve) Rating
I Guess Sir God has a reason to reveal all this during this Kikwete's period. Our Beloved President God has extended his love to you through his/your people. You may ask yourself why it never happened during Mkapa period?? during Nyerere's period?? during Mwingi's period?? does it mean perches were not exporten from Tanzania by then?? with this i mean the Darwin's Sagga. child labour was in its high rank kwanza by then. Kindly manuver the worst to the right!!It really sounds so sad when we export this nile perches, Tanzanite minerals yet the people sarrounding are dying of Hunger- Pls Take note that- THE BEND OF THE ROAD IS NOT THE END OF THE ROAD- The corner ballis now on your hand papa kikwete.
Genevieve from Arusha
Comment #26
(Posted by Beji) Rating
Let the film do the business, but if on the ground its true that these kids are doing the job, then Gov response should be to stop kids doing the job not 'making noise about the movie'
Comment #27
(Posted by CHAWENE JOHN) Rating
This situation is very dangerous for the childrens' Life,and is not fair.
This is the right time for the goverment to solve out this situation inorder to Save the childrens life.
Comment #28
(Posted by kuboko) Rating
Hapo kuna maendeleo didimizi, kwa Taifa, wanaofaidi wako Taiwani viwandani, kunakochongwa Tanzanite. Urithi wa watoto hao utakuwa mashimo yaliyo na mijoka au makaburi ya waliofukiwa.
Comment #29
(Posted by Bernard Rabiel) Rating
Ni kweli watoto wametumikishwa. Ni jambo lisilo jema. Historia inaonyesha kuwa hata nchi kama Uingereza kulikuwa na kutumikisha watoto haswa wakati wa mapinduzi ya viwanda.
Tanzania si nchi ya tofauti katika mapito haya ya kiuchumi.
Inaelekea waliotengeneza taarifa hii hawajui hata historia yao! tuwasemehe!Katika maendeleo na mabidiliko ya kiuchumi na kijamii masuala haya ya kutumikisha watoto yanakuwepo kama wakati mfumo wa nchi unapokuwa katika misukosuko ya kujiunda katika mfumo ulio imara.
Nawashauri walioandaa taarifa hii wajifunze dalili za nyakati ambazo hata wao walizipitia. Mbona huko kwao wanaume wanaoana na hali kadhalika wanawake kwa wanawakewal hawashangai? Kwao wanaona ni jambo la kawaida sie tunaona ni ajabu.Natambua tukiwauliza kuhusu ilo watasema tutambue jinsi ya kusoma nyakati! Basi na wao watambue kusoma nyakati! Hatutabaki huko katka kutumikisha watoto ni mapito tu!
Comment #30
(Posted by Mwanakwaya) Rating
Uchumi ndio tatizo! tunaposema hawa watoto wasifanyishwe kazi, swali: Je Serikali iko tayari kuwasomesha? Sasa hivi kama huna pesa huweza kusomesha mtoto! Angalia hii familia ya Mererani kwamba huyu mama anategemea kipato cha mtoto ndicho kilishe familia, je unafikiri huyu mama atakubali kufa chaa kisa mtoto hatakiwi afanye kazi? Mungu atusaidie Tanzania ili tuondokane na umaskini.
Comment #31
(Posted by Titi) Rating
Marehemu Baba wa Taifa alisema ... hayaozi. Alitaka wazawa wapate kwanza uwezo wa kuyachimba. Lakini.....???? Kikwete, Darwin sawa, na hii je?
Comment #32
(Posted by VF) Rating
I think the first question I would ask my self is 'what is the purpose of the film. Is it just to show how children are being miss used? Is it to show how people near such big investments are not benefiting anyhow but the Gov. does? Is it to enspire parent to care for their children instead of vice versa? Is it to ban the Tanzanite and other mining projects? Is it only at the Tanzanite mining where child labour is practised? Is it happening only in Tanzania or other countries have better ways of doing it? It's whos responsibility to ensure the safety of such kind of work, the Government or Investors? Is there any kind of contract within the Government and Investors which guides the safety of employees and local society? And lastly, is ther solution recommended? Because to my belief, pointing a problem without offering solution is as good as nothing!
Comment #33
(Posted by Pendo) Rating
It's time my fellow Tanzanians to take action. We shouldn't blame the government on everything that is happening, because we play part in making those terrible things happen. We can save these children if we all act responsible. Report to the concerned authority if u come across anyone who is employing our younger brothers and sisters. Chase these kids off the streets to school or to their homes. We should not just sit and blame the government for not stopping child labour. How will the government know if we don't report?? It's impossible for the government to go to each household everyday to ask where the kids are. You take action and I take action. These are our kids and they affect us all. Let's find a place in our hearts for our children. Blessings to you all!
Comment #34
(Posted by an unknown user) Rating
The beneficiary of the film must pay the children and Tanzanians who participated in making the film.
The Minister responsible mining should make sure that child labour at Mines is strictly prohibited and the subjects be punished accordingly and compensation be made.
The government of Tanzania should make sure that compansation to subjects is well guided because the films make in Tanzania never pay the Tanzanians e.g Masai, Wasukuma in Mapanki Film, Tourists Films etc. Let them bertay our country but also they must pay for those who are used to make such beutful business of defarmation of our country!.
President Kikwete, don'nt worry collect the money from those film makers in terms of compansation to yuor people and then taxes on those compansation. It is a good taxable business though is paining to view it! Hurry up to catch them before they run away!
Comment #35
(Posted by unknown) Rating
1.Sinema hii itasaidia serikali kujikosoa kwa kufshughulikia ajira za watoto katika madini.
2. Waliopata huo utajiri wawafidie hao watoto na serikali inafahamu fika walipata nini kwa sababu exports zipo. Investments za matajiri wa madini zinafahaamika na taratibu za ilegal incomes zinajulikana kwa hiyo sheria ichukue mkondo wake.
3. Mtengenezaji wa senema lazima awalipe Watanzania walioshiriki kutengeneza senema hiyo. Hata ile ya mapanki Mwanza. Nafikiri walioshiriki kuzitengeneza watakuwa matajiri hasa Eliza wa mapanki na yule mchora picha na kadhalika. Watanzania tutulize ball kwa kuhakikisha kuwa mapato ya senema hizo japo zatdhalilisha nchi lakini zinakipato duniani. Serikali kupitia balozi zetu ifuatiliae haki ya Wataznaia inayoliwa na watengeneza senema hasa za utalii pia. Wamasai wanauzwa nje kwa njia ya postcards, picha, senema na dideo bila ridhaa ama mikataba yenye kuwapa kipato.
3. Mheshimiwa Kikwete utakapoenda Marekani utetee haki hiyo ya Watanzania wanaodhalilishwa na wageni kwa njia ya kuwatumia kutengeneza filamu za mabilioni ya dola bila wao kupata hata sumuni wala peni.
5. Waziri wa Mali asili na utalii, Madini, Sheria na Manbo ya Katiba, Habari na Utangazaji na vyama vya wanasheria amkeni mutetee Watanzania waliotumiwa bila kujijua kuwatengenezea mabilioni watengeneza senema dhalimu.
6. TRA hebu kusanya hapo hako kakodi ijapo kadogo basi kama royalty, nk. wakati compansations hizo za mabilioni zitakapolipwa Watanzania waliotumika kutengeneza utajiri huo wa ajabu.
7. BUNGE TUNGENI SHERIA KALI YA FIDIA KWA MTANZANIA ATAKAEKUWA ANATUMIWA BILA RIDHAA YAKE KUTENGENEZA PICHA, SENEMA, VIDEO AMA TAARIFA YOYOTE YA KUZWA, KUONYESHWA AMA KUPELEKWA NJE. FIDIA IWE MABILIONI KAMA NI NJE YA NCHI. WAKORA WATAKOMA KUCHEZEA HII NCHI.
Mwisho, pole sana Mh. Kikwete, Loasa, Bunge na Watanzania wote. Tuamke kwa njia ya sheria nzuri bungeni.
Comment #36
(Posted by Jeba) Rating
This may be true, lakini kisiwe kitu cha kututisha sana, hili ni tatizo kama tatizo la ukimwi, njaa na matatizo mengine yaliyopo nchini. Na hili tatizo halipo Tanzania tu, lipo nchi kibao. Hawa wazungu wasitake kututetemesha wala nini, matatizo yetu ya ndani ya nchi tutayashugulikia wenyewe kwa nafasi yetu na uwezo wetu, wasitake kutumia pesa zao kutuchafulia sura yetu nzuri dunianiili tuonekane ni watu wabaya sana. Pumbavu zao.
Comment #37
(Posted by an unknown user) Rating
Kuna mazingira mengi yanayofanya watoto hawa waamue kwenda migodini. kwanza ni uyatima. kwamba wanakosa mahitaji ya muhimu kwani walezi wao hawana uwezo. pili ni kwamba wazazi na walezi wengi hawajatambua umuhimu wa elimu. Kwa hiyo wao kwa hawa watoto kwenda au kutokwenda shule sio issue muhimu. Kwa hiyo hawa wazazi na walezi waelimishwe juu ya umuhimu wa watoto wao kusoma.Tatu, Walezi na wazazi kuwa bizee na mambo mengine na uangalizi wa watoto unachukuliwa kama ziada. watoto wapewe kipaumbele kwanza. Kwa sasa si sahihi kulalamika juu ya filamu hii, ila ni kufanya haya yanayotokea yasitokee sehemu nyingine.
Comment #38
(Posted by John) Rating
I think it is way past due for our government to step up and protect her belongings. It is just ugly to see and hear such things. I am sure more videos are on their way to reveal these sorts of things. Therefore Mr. Mrisho get ready, as this is just the beginning. I am sure your government is aware of all aforementioned yet is not doing anything. This is so sad and very practical for poor countries not to step up to the plate and take care of their responsibilities.
Mr. President, while it is very normal for presidents in our country to finish their terms with very little accomplishment, I am kindly asking you and your members of Parliament to step up and wear the shoes given to you few months ago and go to work.
Mr.Mrisho and your members of parliament, can you imagine if this was your house (Back Yard) and as wealthier as you are, your kids are dying hungry in the mines despite of what their parents are worth. That is how it feels, these kids are born few miles away from Tanzanite, a stone only found in Tanzania yet they are starving, their families depend on them. Education is not a primary achievement to these kids, what do you expect from them when our generation is gone, you will have no educated people to help future citizens.
As a citizen of this peaceful and a Lay back country, I am begging you to act upon these videos and do what you promised us when you were campaigning for presidency and even after you became president. I know most of us feel that you have just been a president for less than a year and, you should not be hold responsible as much. Well, I tell you what Mr. President, irregardless of how long you have had this position; you and your members of parliament have been in this government for so long that none of these is news to you. So please act now and now only not tomorrow.
Thank you.
Citizen Muungwana.
Comment #39
(Posted by alois) Rating
it's absolutetly true; manifestation of highest grade of selfshness attitude,clear exhibition of uncalled relationship of men and their Creator,and the Creator of every thing, Tanzanite inclusive,the unusefullness of either ministry of childrens' wellfare......
Comment #40
(Posted by Fred Mwakikono) Rating
The news is verry much true but the problem is that the Tanzanian likes politics they will oppose while we all know that it is still happening even today
Comment #41
(Posted by ruth meena) Rating
Viongozi wetu walipoona filamu ya " Mapanki" walipiga kelele kwamba tumedhalilishwa, watanzania, je case hii ambayo ni ndogo tu ukilinganisha na athari za mfumo wa ubeberu uliyojikita katika utandawazi watasemaje. Tanzanite inayochimbwa hapa kwetu tanzania iwe inachimbwa na wakubwa au wadogo inawaashia nini watanzania. Afadhali Samaki watanzania wanabaki na vichwa!!!!! machimbo je? Watanzania tufike mahali tuseme, imetosha!! ruth meena
Comment #42
(Posted by Oliver Kishebuka) Rating
This film was very informative as i knew somehow, somewhere ther is child labour but it never occured to me to what extent this was and how these childrens' future is ruined and their lives and helath put at risk.
The price of that stone is very high and its very unfair for those kids as they get paid peanuts for risking their lives to makes others rich.
Comment #43
(Posted by an unknown user) Rating
Kweli hii si haki kwa watoto wa Kitanzania ambao wana haki ya kupata elimu na kuishi kama watoto. Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya vikielekezwa huku mabadiliko yanawezekana.
Comment #44
(Posted by Joshua) Rating
Yawezekana ni kweli yanatokea, cha kushangaza kwa nini hawaanzi kumaliza ya kwao kwanza ndio waende nyumba za wenzao? yanayofanyiwa watoto marekani hasa weusi mbona makubwa kuliko ya Merelani, binadamu utajikomboa mwenyewe na familia yako wala sio donor au Serikali wote hao wako katika ulaji tu, msomaji angalia mwanao asije akafikia hapo na wa jirani yako kwa njia hiyo ushauri utasambaa na tutajikomboa.
Comment #45
(Posted by asha) Rating
kwali hinasikitisha kuona haya mambo maana fedha tunapewa ili kuwasaidia watoto wasome kumbe wakubwa wanakula na kufurahisha watoto wao. sasa wameenda wenyewe na kuona vituko.je mko tayari kwetoa hizo fedha?msijineemeshe wenyewe huku wakijawafadhili mnaonyeshamjini tu.
Comment #46
(Posted by Noah kubilu) Rating
Filamu hii pamoja na ile ya Darwin Nightmare zina ujumbe mmoja mkuu ambao ni mstakabari wa matumizi ya mali asili ya nchi hii kwa manufaa ya wananchi na hasa wale ulioko katika maeneo ambapo mali ya asili hizi zinapatikana.Kama ni kweli kwamba kila mwaka pato la tanzanite ni 300m, iweje wananchi wanaoishi maeneo ya mererani waishi katika ummaskini mkubwa kiasi hicho? Nani ananufaika na mapato haya.Kiasi gani cha mapato kinarudi mererani kujenga shule, hospitali , barabara n.k?.Inaonekanan kuna ufisadi mkubwa katika nchi yetu juu ya swala la matumizi ya mali asili.Tunahitaji mjadala wa kitaifa ili kuweka bayana hatima ya mali asili zetu- vinginevyo wajanja wachache ndani na nje nchi wateendelea kuikamua nchi hii na siku tukianza kuongea kwa sauti mmoja hakutakuwa na kitu.KIZAZI CHETU KINALAANA KIMESHINDWA KUONGEA HATA PALE PANAPOKUWA NA UFISADI WA WAZIWAZI.MUNGU ATUSAMEHE
Comment #47
(Posted by Honory Lyimo) Rating
Hali hii sio nzuri. watoto ni wadogo mno. inaonyesha wazi kuwa bado tu maskini sana hapa Tanzania na tunahitaji mwamko katika shule za msingi. wazazi wa watoto hao yawezekana hawana uwezo wa kuwapeleka shule, japokuwa inasemekana shule za msingi hulipa pesa kidogo tu (kuchangia) sio kila mmoja anauwezo huo. hivi karibuni tu nilikuwa likizo na nimetembelea sehemu nyingi sana katika mkoa wa kilimanjaro, ukienda sehemu za rombo inaonekana kuna shule nyingi sana za msingi na secondari, lakini sehemu nyingine shule ziko mbali sana na watoto hutembea hata kilometa zaidi ya 10 kwenda na kurudi!! zamani vyama vya ushirika vilikuwa na mafungu ya shule, nakumbuka hata uniform za shule zilikuwa zinagawiwa kwa kila mwanafunzi bure.
naomba serikali itazame upya kuhusu shule za msingi achilia mbali zile za private ili kuhakikisha watoto wadogo kama hao wanaenda kwanza shule ili waweze kuwa na angalau elimu ya kuweza kutambua haki zao.
Comment #48
(Posted by jean) Rating
Tanzania imebarikiwa wakati mwingine nafikiri ni bustani ya Eden? tuna mali asilia nyingi tuzitumie tupasue mapori moja tujenga viwanda vya kusindika mazao tujenge shule maalumu kwa watoto wote wasio na uwezo,makazi na yatima hii inawezekana. tutumie vizuri mbuga za wanyama,hifadhi za uwindaji,madini kama dhahabu,tanzanite,almasi na aina zote zilizopo,makaa ya mawe,gesi mpaka mafuta tunayo Mungu atupe nini?ziwa kubwa duniani victoria,ziwa kina kirefu duniani tanganyika,mlima kilimanjaro,misitu kila kona. tunaweza ila tunahitaji kuwajibika kwa manufaa ya vizazi vijavyo na sio kuchumia tumbo.hata wageni wanafaidi sana njii hii.
Comment #49
(Posted by Renee) Rating
AS A MOTHER, MY HEART GOES OUT TO THESE KIDS WHOSE PARENTS HAVE FAILED TO PROTECT THEM FROM SUCH HARSHNESS. AS A PARENT I AM ANGERED BY PARENTS WHO SUBJECT THEIR CHILDREN TO LABOUR AND IN PARTICULAR UNDER SUCH DANGEROUS ENVIRONS. AS A CITIZEN I AM LIVID THAT MY GOVERNMENT HAS FAILED TO PROTECT THESE CHILDREN, THE VERY FUTURE OF OUR COUNTRY. AS AN INDIVIDUAL I HANG MY HEAD IN SHAME FOR NOT BEING ABLE TO HELP CHANGE THE PLIGHT OF THESE AND OTHER CHILDREN. I PRAY THE ALMIGHTY PROTECT THEM AND ENLIGHTEN THEIR PARENTS AND ENABLE THE GOVERNMENT TO INTERVENE.
Comment #50
(Posted by Mhache p.) Rating
Ni jambo la kusikitiha sana kuona jinsi watanzania tunavyodhalilishwa na wageni wanaoingia nchini kwa vibali halisi na kuja kutuchukua filamu zisizokuwa na heshima kwetu na kwa nchi yetu kwa ujumla . Tunaomba vyombo vinavyohusika vichunguze ujio wa watu kama hawa na madhumuni ya wao kuingia sehemu kama hizo na kuchukua habari.
Comment #51
(Posted by Mhache p.) Rating
Ni jambo la kusikitiha sana kuona jinsi watanzania tunavyodhalilishwa na wageni wanaoingia nchini kwa vibali halisi na kuja kutuchukua filamu zisizokuwa na heshima kwetu na kwa nchi yetu kwa ujumla . Tunaomba vyombo vinavyohusika vichunguze ujio wa watu kama hawa na madhumuni ya wao kuingia sehemu kama hizo na kuchukua habari.
Comment #52
(Posted by Bernard Desderius) Rating
Its a series of explosions to our goverment....i have read it thrice in order to believe it...i feel very sorry for the youngboys to be in a such death awaiting situation if its true,i never thought this could be happening in our lovely country(Tanzania).This is very serious and touchig,the government should punnish the owners of the miners in which this is found true and if possible these sections in which these young boys are working should be given to other orginisation/stakeholders to to re-supervise!Sorry for the Tanzanians...!
Comment #53
(Posted by Mmachinga) Rating
Kikwete, would you comment on this after the Darwin's nightmare? Inauma lakini ni ukweli, dawa sio kuwatukana wazungu ila ni kurekebisha mifumo yetu. Wananchi hawana rasilimali na filamu hizi ni dadlili mbaya kwetu inafaa tuzinduke usingizini. Maandamano hayatasaidia kutatua matatizo yetu. Ni kweli tunakula mapanki kwani uongo? Uzalendo ni sawa lakini ukweli ukoje
Comment #54
(Posted by Ali Kalufya) Rating
I guess this film exposes a bigger problem: "How much of Tanzanian resources actually end up helping Tanzania(ns)". This has to do with contracting and dealing with foreign investers (pls read: harvesters). Many countries get developed from use of local resources e.g. USA (ref: Gold rush), Arabia, Iran, Iraq(!)(Oil), South Africa (Diamonds, etc), HOW ABOUT US? I guess a hard look is needed to how much foreigners are harvesting vis-a-vis how much they return to the country. I am afraid some investors (sic) are using TZ as "kopo la chooni". Use it till it rusts / get a hole then ditch it. TZ is not alone in this case, same applies to Angola, Rep.of. Congo, to name a few.
It seems to do with national leadership and conditions and regulations that they set. I have been to some countries, much more developed than TZ, with unbeliavable hard conditions for removing wealth from the country. I have hope in JK as he seems to have nation at heart, however without support from others (you and me) he may not make it. There are too many keen to use non-local resoures for improving their national welfares hence we should not expect miracles to be only on our side. We need build up courage to our leadership, we need to support them to our capacities. On the same line we should maintain local critical outlook and propose tangible solutions without harming our national image. We have working structures, through increasingly open political processes and understanding elements of our government. Destroying national image is same to boring a hole in our boat and nobody who is inside will appreciate you for that.
Comment #55
(Posted by an unknown user) Rating
jamani eeeeeeeeeeeeeeh tuwe wajanja hii filami ni biashara ya GOOD HOPE ni huyo mamanger na si dhani kama kweli anawasaidia watoto he is for buzines. haya wapige na picha kwenye McDonald na TARGET na HEB kuona ni vitoto vingapi vinafanya kazi hata huku USA. mimi naamini dunia nzima watoto wanafanya kazi kutegemeana na mazingira yao, ukienda columbia nahisi utawakuta watot wanalima madawa, UAE wanachimba mafuta, ZNZ wanalima karafuu,Uganda Kahawa,somalia na Darful ni wanajeshi, sasa hizo zote kazi wasitushangae sisi.pia kama kucheza cinema na kuimba ili kupata kipato ni ajira sasa wao mbona nao wanawachezesha watoto na haviendi shule. WAZUNGU ACHENI KUTUZINGUA
Comment #56
(Posted by Mwasakafyuka) Rating
Labour child is illegal no matter what. children should either be in school or at home.parents should go to the mining jobs and not children. severe punishment must be inflicted to children employers.
It is really unfair to learn that around 300 million is collected in every single year from mining activities and yet children and the local citizens in the mining areas are living below 1 dollar a day, this is absurd. it is high time now to get rid of this government,I urge all Tanzanians to show their wrath and disagreement with the current government and remoe it from power, elect those leaders who will not tolerate any kind of exploitation.Bora ukoloni urudi, kuliko kuwa na bogus leaders like the current leaders. watanzania tutaamka lini jamani? tunadanganyika na vitu vidogo sana, viongozi wetu wamejaa porojo, hivi hamuoni kweli? watoto wanatumikishwa, umeme hakuna? barabara hakuna? ajali kila siku,rushwa inaongezeka, kodi kwa wananchi inaongezeka, wezi wa mali ya umma wanaongezeka na jela hawaendi, wanaokwenda jela, ni wamachinga eti wazurulaji, jela waende waliotusaliti na mikataba kama ya IPTL,wanaoajili watoto, wala rushwa nk.WATANZANIA AMKENI, HUO NI USINGIZI GANI JAMANI? Hakuna serikali hapa.
Comment #57
(Posted by Prisca) Rating
What is this my fellow Tanzanian since we have got independence up to now there is a very little changes in our country regardless of the up to date on luxuries.
look at these children they are very young with no care from their parents we us their parents we shouls take action,because if we could not be resiponsible from home who will do to the top stage?our gorvement done nothing up to now.shida ni nyingi sana hasa vijijini tusiangale maendeleo yaliyopo dar es salaam tu tuende na mikoa mingine tujionee has vijijini kila kona ya kijiji kilichoko tanzania maisha ni dunu saaaaaaana.ila viongozi wao huishia wilayani mjini tu hawafiki vijijini kule ndsni ndani.
sasa hao migodini waweza ambiwa kuna wanakijiji wanalala na jnaa huku wengine wakijisombea pesa hali kadhalika hata watu hfa kwa kukosa huduam bora za kujamii ona hii nini nini wkati atu wanasomb mamilioni ya pesa huku mtot akiingia mle bila ha ta kitu cha kuweza kumkinga na hatari je?hakuna watu wazima wanaoweza kufanya shughuli hizo.mimi naomba serikali nayo iwaweke ndani gerezani wale wanaowatumikisha watoto kwani pia wao wanajua wazi kuwa chils labour sio nzuri kwaki kwa kufanya hivyo kma wale wasingekuwa wanawaajiri sidhani kama kuna mtoto angeingia huko chini pia hata eneo hilo la migodo watoto wapigwe marufuku kufika hapo ni hata ri.kwani wnaaingia tamaa hata wanapoona baadhi ya kaizi zinazofanyika hapo nao wanatamani kuzifanya kitu ambacho matokeo yake ndio hayo tunayoyaon.waacheni wenzetu waendelee kuchukua mikanda na bado tukiendelea kulala lala ovyo watachukua hadi picha kuonyesh afamili dunu ya mtanzanania inavyoishi kila siku ona sijui hii itakuwa aibu gani kwa Raisi ikiwa ataendelea kusema tumepigahatua ya maendeo na kuwa tunazalisha 6.....kwamba tuko mbele na wakati kuna familia ya kitanzania inalaa njaaaaa.
Angalieni tunakwenda wapiiiiiiiiii
viongozi wamekaa bure kwenye madaraka.
nipeni mimi nafasi ya viti maalumu muone kazi yangu.
Comment #58
(Posted by Mbongo abroad) Rating
bwana Mwasakafyuka umetoa changamoto hapo juu kwa kweli, ni kweli kabisa tunahitaji mapinduzi ya fikra nchini mwetu, hivi sasa wengi watanzania hatujui siasa zinavyoendeshwa na ndiyo maanake huwezi ona maendeleo ya vitendo, nchi imejaa uozo mtupu, na watanzania wengi tupo kimya kwa sababu naweza sema siasa iliyotawala nchini mwetu tokea tupate uhuru ilikuwa ya kunyamazisha wananchi kuongelea jambo kwa uwazi. hivi sasa wanaotusaidia ni foreign media kuibua issues zilizoshindikana ili walimwengu waone Tanzania ilivyo katiba absolute poverty(siyo ya mali tu hata ya mawazo). hebu tujiulize kwanini tunawapa kura hawa watu wasiokuwa na imani kwa nchi yetu? kuna mikataba mingapi nchini mwetu ni fake? na haya matatizo tumlaumu nani? media yetu wala haijasimama kidete kufichua haya na ndiyo maana hivi sasa tunasaidiwa na wengine. usije ukashangaa jk na timu yake wanailaani hii filamu, ndiyo mbegu za ujamaa hizi. Huu ni ukweli mtupu na lazima serikali itumikie watu waliowaweka madarakani, hapa mtu wa kwanza kupoteza kazi alitakiwa kuwa waziri wa madini na nishati!!.
Comment #59
(Posted by Radyn Nyagaly) Rating
hata kama maisha ni magumu katika familia, lakini kumwashia mtoto kufanya kazi ktk mazingira haya ni kufupisha maisha yake. fikiria kabla ya kumwacha mtoto kuishi hapa na kuendesha maisha kwa kisingizio cha ugumu wa maisha.
Comment #60
(Posted by said) Rating
thearticlecontainsfalseinformation,andits decoy, i can say well done act.
Comment #61
(Posted by Kemunto Ondieki) Rating
Issues of Child labor are a reflection of national economy and management.This film clearly shows how flawed our national leadership is.Lets keep working at holding our politicians accountable on issues of equity on national resources for all people.May the religious members of society be the conscious of the society to awaken us to the needs of children, women and all people to receive a fair share of the nation's resources. Let us all advocate for for basic human rights for all people especially children in the areas of education, health, protection etc.
Let us know our national constitution well to point to, so that if it is not helpful, we could call for revision and ammendment to serve children and all people well and effectively.
May God have mercy on us all!
Comment #62
(Posted by Miah) Rating
Aaah hii sasa zaidi, minofu hatujui imeishia ipi, sasa limekuja lingine, Serikali amka na okoa Taifa la kesho!!!
Comment #63
(Posted by Pauline) Rating
Nimeangalia hiyo cinema, to me it sounds normal, kwani yote tunayafahamu, ila kinachonisikitisha ni hizi NGO as they are also known as Nothing Going On (with them) kutumia baadhi ya matatizo tuliyokuwa nayo kama njia za wao kujipatia fedha. We Tanzanians we should be very carefull with this. Pia nadhani imefikia hatua nasi tukatae kuwa chambo cha kuwezesha watu wengine kujinufaisha na matatizo yetu, kwani huko marekani hakuna matatizo, yapo jamani au matatizo yamekuwa ya bara la afrika tu, we need to be brave wazungu hao si chochote si lolote nao wanatafuta kula tu we need to be very careful.
Mfano mimi binafsi naiona NGO ya Good Hope kama wayeyushaji na wanatumia cinema hii kama njia ya wao kupatia fedha ambazo naiimani wakizipata utasikia wamepeleka mtoto mmoja sekondari na ndio itakuwa hadithi ya mwaka. PIa watanzania sasa inabidi tujiulize je matatizo yetu yatatatuliwa kwa kumuita Jane kutoka Marekani na kutengeneza cinema kupia nothing is going on fulani au ni suala la sisi kama watanzania kukumea kwa kutumia jamii husika, wataalamu tuliokuwa nao katika kutatuwa matatizo tuliokuwao nayo. Merareni si watoto wote wako pale kwasababu wazazi wao hawana uwezo, najua kabisa kuna watoto walioko pale wametoka katika familia zenye uwezo ila wanataka ku win maisha mapema, hao tunwachukkuliaje!!ninachoweza kuwaasa watanzania wenzangu ni kuwa sasa imefikia hatua ambayo inabidi tuwe makini kinyume cha hapo wewe itarekodi mererani wenzio watamrekodi bibi yako kijijini utashangaa tuu kumuona naye new york kwenye cinema iliyoaandaliwa na help age international.
Comment #64
(Posted by lucian) Rating
it's not about the quality of the article,it's about the content,it's about how we should help the children by stopping child labour,why you guys care about the quality of this article? i find this very ridiculous.
i congratulate you for the good work of informing us about what's happening in our country. i live abroad and i depend on habaritanzania to see what's going on back home.
Comment #65
(Posted by shani) Rating
It is disturbing to read this article, Tanzanite Jewellery, the cheapest here in Namibia costs R 1000, but to see that those boys at age 12 in those holes earning 200 shillings, brought tears and anger to my heart. For an industry that earns 300M US Dollars, where is Africa going, will it ever be a better place for Africans!!!!! That 300M US, where is it???? It will be a miracle to find it in Tanzania!!!!!!!
Comment #66
(Posted by Naomy Mrutu) Rating
Hakuna kitu nachukia katika maisha yangu kama mtoto mdogo kutetendewa haki yake,, Tanzania ni nchi masikini lakini si kiasi cha kunyanyasa watoto hivi kwa kuwapa kazi ngumu na kuwalipa pesa ndogo wakati unajua kabisa kabisa kwamba mtoto anatakiwa aende shule na pia unafahamu kabisa kuwa serikali inapinga swala la ajira kwa watoto....watu wa migodini wanaoajiri watoto wanatakiwa wachukuliwe hatua za kisheria...Inauma sana tena sana kuona hali kama hii...je viongozi wako wapi???NGO's ziko wapi???misaada inapelekwa wapi?????
Comment #67
(Posted by Edith Mwita) Rating
It is true kwamba watoto hawatakiwi kutumikishwa na hilo nalipiga vita sana .Lakni hebu tuangalia nani chanzo cha haya yooote ?
Huyo mzungu anayechukua filamu hiyo yeye mwenywe ameenda hapo kwa ajili ya Tanzanite hiyo hiyo.Fatilia utaona !! Wazungu ndio wanapenda kuwafanyisha watu kwenye slavery . Kwa nini sisi watanzania tusingetengeneza hiyo filamu ila mzungu ndio aje atengeneze??? motive yao ni nini??? yeye angetukumbusha lakini kwanini awe msemaji wa nchi yetu ? hiyo ni kutaka kutudhalilisha tu sometimes na wala hwana real huruma ya kweli .Tanzania inadhalilika sana sometimes hata ukiangalia ile Darwins nightmare nayo ilituonyehsa sisi sijui tukoje .
ni kweli watoto wasiajiriwe na sote tukatae lakini ni lazimua mzungu ndio aje aone hayo na sio sisi??? kwani sisi hapa Tanzania hakuna wenye uchungu na watoto?. wazungu wengi hata kuzaa hawataki sasa huruma ya wtoto inatoka wapi? -nao wanataka kula tu kutumia picha zetu -hebu tuweni na akili jamani wale mnaoruhusu wazungu kuchukua filamu jiulize kwanza kabla hujaruhusu mgeni kutuuumbua. mbona ya kwao hata hapa marekani ni mengi hawayasemi??? kwa nini mabo yetu tuanike nje nje na ya kwao mabaya mno ahayonyeshiw umoja wa mataifa ????
Comment #68
(Posted by mkereketwa) Rating
Inasikitisha sana kwamba watoto hawa wanafanyishwa kazi migodini.Je ni jukumu la nani kuhakikisha kwamba tabia hii inakomeshwa?, Ni malezi mabaya, umasikini na utundu wa watoto wetu wa leo, Kwa mfano watoto wengine wanakataa shule na malezi bora nyumbani wanakimbilia mererani.
SASA NINACHOTAKA TU KUKAZIA NI KWAMBA, KWANZA ANAYETENGENEZA HII FILAMU ATATENGENEZA HELA YAKE LAKINI WAKATI HUOHUO BEI YA TANZANITE ITAPUNGUA KUTOKANA KWAMBA WAVAAJI WAKUBWA WA JEWLRY NI WANAWAKE, NA KAMA NIWAJUAVYO WAZUNGU, WAKIONA KITU KAMA HICHO WATZIRA KUNUNUA TANZANITE BILA KUJUA UNDANI WA TATIZO LENYEWE. TUSIHARIBU BIASHARA INAYOLETA MAENDELEO NYUMBANI. SI MNAKUMBUKA WALIPOSEMA KWAMBA KIKUNDI CHA UGAIDI AL-QAIDA WANATUMIA TZNITE KUFANYA KAZI ZAO BEI ZILISHUKA SANA, KWA MAANA HIYO KILA BIASHARA ARUSHA IKASINZIA.NAONA SEREKALI ISINGERUHU FILAMU KAMA HII