Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK. AWASHUKURU MADAKTARI KWA KUFANIKISHA MATIBABU YA MTOTO BAKARI HAMISI KATUMBAKU
JK. AWASHUKURU MADAKTARI KWA KUFANIKISHA MATIBABU YA MTOTO BAKARI HAMISI KATUMBAKU
By Habari Tanzania | Published  09/10/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
  • Aahidi kutafuta wafadhili kuisaidia Idara ya Upasuaji Bandia
  • Ampandisha Ndege Bakari Kurudi Tabora
  • Mtoto asema Mungu Atakubariki
 
IKULU
09.09.2006
 
DAR ES SALAAM
 
 
Rais Jakaya Kikwete ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hususani Profesa Atef Amin na Dk. Laurean Rwanyuma kwa kufanikisha upasuaji na matibabu yaliyomrejesha katika hali  yake ya kawaida mtoto Bakari Hamisi Katumbaku.
 
 Kutokana na furaha yake hiyo, na kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.  Rais ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo,  kufanya utafiti wa kina wa gharama za baadhi ya mashine  muhimu zizonahitajika katika Idara ya upasuaji bandia(plastic Surgery) ili awatafute   watu wenye mapenzi mema wagharamie mashine hizo.
 
Alitoa  shukrani hizo na agizo hilo, jana jioni wakati alipomkaribisha mtoto  Bakari Hamisi  Katumbaku Ikulu  kwa lengo la kumujilia hali na kuagana naye baada ya kukamilika kwa matibabu yake. Mtoto huyo alifika Ikulu akifuatana   na Mama yake, Bi Aziza Hamisi Katumbaku, Daktari wake, Laurean Rwanyuma na Muuguzi, Bi Ritha Kitama. Profesa Atef Amin ambaye ni rais wa Misri hakuweza kufika kutoka na majukumu hospitali hapo.
 
Mara Rais alipomuona mtoto Bakari akitembea vizuri kabisa bila dalili zozote za kujikuja au maumivu kama alivyomwona mara ya kwanza kule Sikonge.
 
 Alitamka “ nashukuru sana, umepona kabisa, daktari  nashukuru sana, nilipomwona mara yakwanza Sikonge, hali yake ilikuwa mbaya,  alikuwa akitembea kwa kuinama na akajitahidi kunikimbilia kama watoto wenzie lakini kwa tabu sana. Nikasema mungu akijalia nitakusaidia, Mungu Mkubwa, nimefurahi sana”.
 
Akaongeza “ Nawashakuru sana, ehe, angalia, Bw. Bakari, sasa mambo safi sasa, unatembea kama watoto wenzio, sasa huna mawazo wala uchungu tena,  utakuwa na raha sasa umerudi katika hali ya kawaida, sasa  kasome kweli kweli , ili uje kumsaidi mama,  na sisi tutakuwa tunafuatilia maendeleo yako shuleni akasema rais. Na kuachia tabasamu pana.
 
“ Daktari hebu kafenye tathimini halisi ya ghara za mashine mnazosema zinahitajika sana.Niliteeni gharama halisi za mashine hizo, wapo watu wenye mapenzi mema wanaotaka kupata thawabu kwa Mwenyezi Mungu, watakuwa tayari kugharamia mashine hizo ”alisisitiza rais.
 
 
 
Akitoa shukrani zake kwa Rais, mtoto Bakari ambaye alikumbatiana kwa furaha na Rais kama Baba na Mwana, alisema “Nakushuru sana, Rais, Mungu Akujalie, sina cha kusema nakushuru sana. Nimefurahi sana.
 
Naye Mama wa Bakari yeye alikuwa na haya ya kusema. “ Nakushukuru sana, na kukupongeza kwa kutimiza ahadi yako, haikuwa rahisi kwangu kuamini pale nilipoletewa taarifa kwamba Umeaagiza tuje muhimbili kwa matibabu. Sikutegemea  kama mtoto wangu leo angeweza kutembea  vizuri kama watoto wenzie. Nakushukuru sana Mhe. Rais”.
 
 
Katika maelezo yake kwa Rais kuhusu upasuaji aliyofanyiwa mtoto Bakari aliyeungua  moto wakati akiwa na umri wa miaka sita na kumsababisha maumivu makali yaliyomfanya ashindwe kutembea vizuri, alisema, idara ya upasuaji katika hospitali hiyo, haina mashine muhimu ambazo  zingesaidia sana kuokoa maisha ya Watanzania wengi hususani wale wanaopata ajali za kuungua moto na kupoteza asilimia kubwa ya ngozi zao.
 
Dk Rwanyuma alisema idara hiyo ambayo hadi miaka ya hivi karibuni ilikuwa haina wataalamu wa upasuaji bandia, isipokuwa wale wakutoka nchini misri inahitaji mashine zinazoweza kuotesha ngozi au kuitanua hususani pale mgonjwa anapokuwa amepoteza asilimia zaidi ya 80 ya ngozi yake na hivyo kubakiwa na ngozi kidogo tu ambayo haiwezi kutosha kufunika majeraha yake yote.
 
Aidha alisema kuwa pamoja na kupatikana kwa mashine hizo, pia mafunzo yanahitajika ili kuweza kupata wataalamu wengi zaidi katika idara hiyo, hali aliyosema itasaidia sana katika si tu kuokoa maisha ya watanzania bali pia kurekebisha viungo vyao na kuwafanya watu wenye furaha.
 
 
Rais alisema ni vizuri mashine hiyo ikapatikana ili maisha ya watanzania wengi zaidi yaweze kuokolewa. Na hivyo kusisitiza apewe maelezo kamili ya aina na gharama za  mashine hizo.
 
Rais Kikwete alimweleza daktari huyo kwamba vifaa vya uchunguzi ni muhimu sana na hususani katika hospitali kubwa kama Muhimbili “ wenzetu Ulaya wanatushinda kwa sababu wanavifaa na mitambo ya uchunguzi, kwahiyo nasisi lazima tujielekeze katika kuiwezesha hospitali yetu kupata mashine na mitambo muhimu ya uchunguzi. Lazima na sisi tukimbizane na teknolojia mpya huo ndio uwe moyo wetu. Ili tuweze kuokoa maisha ya watanzania wengi”.
 
Katika kukamilisha furaha yake, Rais aliwaagiza maafisa wake, kuhakikisha kwamba wanampatia usafiri wa ndege, mtoto Bakari na Mama yake, katika safari yake ya kurudi nyumbani.
 
Mwisho.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by zeralucy masanja)
    Rating
    Tunamshukuru Rais wetu kwa moyo wake wa kuweza kusaidia maskini ambao hawajiwezi kutokana na kipato chao kidogo. Tunamwomba Mwenyezi Mungu amjalie katika kazi zake za kila siku na amjalie maisha yake yote pamoja na familia yake. Mwenyezi Mungu amzidishie pale palipopungua.
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.