Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK achafua rekodi kwa waandishi
JK achafua rekodi kwa waandishi
By Habari Tanzania | Published  09/10/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

HAIKUTARAJIWA, lakini ilitokea. Ujirani na uhusiano mwema kati ya Rais Jakaya Kikwete na waandishi wa habari jana uliingia dosari baada ya waandishi kufukuzwa katika ziara yake.

Waandishi hao wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, walikuwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kutembelea Wizara ya Usalama wa Raia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Ilikuwa baada ya Rais Kikwete kutembelea maeneo mbalimbali ya wizara hiyo na kuzindua mfuko wa akiba na mikopo (SACCOS) wa wafanyakazi wa wizara hiyo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Essaka Mugasa, ndiye aliyewagombanisha waandishi na Rais Kikwete, baada ya kutangaza kwa vipaza sauti na kusema: “Waandishi wa habari na wageni toka benki ya CRDB tunaomba muondoke.”

Baada ya kauli hiyo, waandishi walipigwa butwaa na kutoka nje ya ukumbi huku wakiulizana maswali, kuna siri gani katika kikao cha rais na askari, huku wakizungumza kupitia vipaza sauti.

Waandishi wengi walinung’unika na kulalamika, kwamba hawakutendewa haki, lakini hakuna aliyewasikiliza.

“Tunakubali kuondolewa kwenye mkutano huu, lakini hawajatutendea haki kabisa, tumeshirikiana nao tangu asubuhi kwa kutembelea maeneo mbalimbali…, inasikitisha na inakatisha tamaa,” alisema mwandishi mmoja ambaye pia ni mpiga picha.

Rais Kikwete alikuwa anakutana na maofisa wa ngazi za juu, wakuu wa vitengo, na askari wa ngazi za chini ikiwa ni moja ya utaratibu wake aliojiwekea kwa kutembelea wizara mbalimbali.

Hii ni mara ya kwanza kwa waandishi kufukuzwa katika tukio linalomhusu Rais Kikwete, ambaye amekuwa akidaiwa kuwa karibu na waandishi. Kwa sababu hiyo, waandishi wengi walilalamika kwamba ndiye aliyewafukuza, na kwamba kama angetaka angewazuia maofisa wake kutenga waandishi.

Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) tayari kimeingizwa katika ubaguzi wa waandishi wa habari. Wiki chache zilizopita, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwafukuza waandishi katika mkutano mmoja wa ndani aliokuwa anauhutubia mkoani Singida. Baada ya kuwafukuza ukumbini kwa kauli kali, kwa kisingizio kuwa wanapotosha anayosema, aliwaita tena waandishi wa Radio Tanzania na magazeti ya Daily News, Uhuru na Mzalendo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by muungwana)
    Rating
    mgema akisifiwa..........waandishi wengi wahabari wamekuwa wakimsifia sana huyu bwana hata kwa mambo ambayo si sahihi badala ya kumchambua.that is what you get.
     
  • Comment #2 (Posted by Nthelezi Nesaa)
    Rating
    Wapendwa wasomaji wa wavuti huu jiandaeni kupata makala safi kuhusu fungate ya Kikwete na wadanganyika iliyoko jikoni.
    Kwa kuwafukuza waandishi wa habari amefanya vizuri kuwaonyesha sura yake halisi kama mwanasiasa.
    Waandishi kwa njia moja au nyingine wanavuna walichopanda.
    Kama siyo wao isingewezekana huu mgao wa umeme na uteuzi wake wa watu wachafu tunaowajua ungeshupaliwa. Nani afanye hivyo iwapo mdomo yaani waandishi waliamua kumung'unya takrima na kucheza ngoma wasiyoijua.
    Bravo Kikwete kuonyesha kuwa hata nyuma ya malikia kunaweza kuwa na sura katili. Nani alitarajia yaliyokuwa yakitokea kwenye jumba la kifalme la uingereza wakati wa maisha ya Diana?
    uzandiki.
    Kwaheri
    Nthe
    Canada
     
  • Comment #3 (Posted by Nthelezi Nesaa)
    Rating
    Wapendwa wasomaji wa wavuti huu jiandaeni kupata makala safi kuhusu fungate ya Kikwete na wadanganyika iliyoko jikoni.
    Kwa kuwafukuza waandishi wa habari amefanya vizuri kuwaonyesha sura yake halisi kama mwanasiasa.
    Waandishi kwa njia moja au nyingine wanavuna walichopanda.
    Kama siyo wao isingewezekana huu mgao wa umeme na uteuzi wake wa watu wachafu tunaowajua ungeshupaliwa. Nani afanye hivyo iwapo mdomo yaani waandishi waliamua kumung'unya takrima na kucheza ngoma wasiyoijua.
    Bravo Kikwete kuonyesha kuwa hata nyuma ya malikia kunaweza kuwa na sura katili. Nani alitarajia yaliyokuwa yakitokea kwenye jumba la kifalme la uingereza wakati wa maisha ya Diana?
    uzandiki.
    Kwaheri
    Nthe
    Canada
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.