Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mfanyabiashara kizimbani Dar kwa kukutwa na magogo ya sh. milioni 300
Mfanyabiashara kizimbani Dar kwa kukutwa na magogo ya sh. milioni 300
By Habari Tanzania | Published  05/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARAS wa mjini Dar es Salaam, Yahaya Masare (46) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka sita, likiwemo la kupatikana na mazao ya misitu yenye thamani ya sh. milioni 300.
 
Mwendesha Mashitaka, Charles Kenyela, alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Silvanus Mwangesi, kuwa katika shitaka la kwanza, mshitakiwa katika siku isiyofahamika wala sehemu, alikula njama kutenda kosa na kuidanganya Wizara ya Maliasili na Utalii.
 
Katika shitaka la pili, inadaiwa kwamba Julai 13, 2005 nyakati za kazi katika jiji la Dar es Salaam, alitengeneza hati bandia ya usajili wa mazao ya misitu yenye namba 00032879, ikionyesha imetolewa Julai 13, mwaka jana.
 
Ilidaiwa kuwa hati hiyo ni ya kampuni ya NAHA SAW MILL iliyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, jambo ambalo si kweli.
 
Kenyela alidai kuwa katika shitaka la tatu, mshitakiwa alidaiwa kutenda kosa hilo Mei 8, 2005 nyakati za kazi katika Wizara hiyo, kwa kughushi hati namba 00032879 iliyoonyesha imetolewa na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Aloyce Tango, kwa kampuni ya NAHA SAW MILL, jambo ambalo si kweli.
 
Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa Agosti 5 mwaka jana, jiji la Dar es Salaam, mshitakiwa alighushi hati ya mazao ya misitu yenye namba 00027855 iliyoonyesha kutolewa Septemba 5, 2005, ikiwa na jina la kampuni ya Y.G.F na kutolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii.
 
Shitaka la tano indaiwa kwamba katika tarehe hiyo hiyo, mshitakiwa alighushi hati ya mazao ya misitu yenye namba 00027855 inayodaiwa ilitolewa Julai 13, 2005.
 
Ilidaiwa kuwa, hati hiyo ilionekana ina majina la Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Aloyce Tango, ikionyesha imetolewa na Wizara hiyo, jambo ambalo si kweli.
 
Katika shitaka la sita, mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 7, mwaka huu katika eneo la ‘Merizario Yard’, barabara ya Nyerere, Dar es Salaam. Anadaiwa kukutwa na mbao mita za ujazo 2,500 zenye thamani ya milioni 300 mali ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
 
Mshitakiwa alikana mashitaka yote sita na alirudishwa rumande, baada ya kukosa wadhamini kutokana na kushindwa masharti ya dhamana. Kesi hiyo itatajwa Mei 30 mwaka huu.
 
Upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.