Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mchakato ubunge EAC CHADEMA waanza
Mchakato ubunge EAC CHADEMA waanza
By Habari Tanzania | Published  09/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Charles Mullinda

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza utaratibu wa kuteua wanachama wanaotaka kugombea ubunge wa Afrika Mashariki, na sifa za waombaji.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad Slaa, sifa ya kwanza ya mwombaji lazima awe raia wa Tanzania.

Sifa nyingine ni kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania na awe na nia thabiti ya kupenda kuendeleza malengo na madhumuni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa fomu za kuomba kuteuliwa zinapatikana katika ofisi za mkoa na ofisi ya Katibu Mkuu. Inawataka waombaji kuwasilisha maombi yao katika ofisi ya Katibu Mkuu Septemba 30.

Anaelekeza Katibu Mkuu huyo kwenye taarifa yake hiyo kuwa waombaji wanatakiwa kufika kwenye ofisi ya Katibu Mkuu Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano Oktoba 15.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, Kamati Kuu itakutana kuchagua jina moja la mwanachama atakayegombea nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki kupitia CHADEMA.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.