Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kupanda nauli ni lazima - TABOA
Kupanda nauli ni lazima - TABOA
By Habari Tanzania | Published  05/23/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA), kimesema ni vigumu kuwazuia wasafirishaji kupandisha nauli za mabasi kutokana na mazingira yaliyopo sasa ya kupanda kwa bei ya mafuta, sambamba na gharama za uendeshaji.
 
Mwenyekiti wa TABOA, Mohammed Abdullah, aliyasema hayo jana mjini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa chama hicho kuhusiana na sakata la kupanda kwa nauli za mabasi kunakosababisha na ongezeko la bei ya mafuta.
 
"Tunachosema sisi kama TABOA hatuwezi kuwaambia wasafirishaji wapandishe nauli, lakini pia tunawatetea kwamba wasilazimishwe kuteremsha bei," alisema Abdullah na kuongeza kwamba inafika mahali msafirishaji anaona hawezi kumudu gharama za uendeshaji bila ya kupandisha nauli.
 
Alisema kuendelea kuwabana wasafirishaji kutopandisha nauli kunaweza kuwa madhara kwa kuwa watalazimika kutoa huduma hizo kwa njia za ujanja ujanja, hivyo kuhatarisha maisha ya wasafiri.
 
Kwa mujibu wa Abdullah, bei ya mafuta imekuwa ikipanda siku hadi siku na kwamba kwa mwaka huu pekee, imepanda mara tano licha ya maombi na mapendezo yaliyowasilishwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafirishaji Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kujibiwa kwamba hiyo ni biashara huria.
 
Hivi karibuni SUMATRA ilitoa maelekezo kwa wenye mabasi kutopandisha holela nauli kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta hadi wadau wa sekta hiyo watakapokutana na kujadili suala hilo.
 
Kufuatia tamko hilo, baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo, madereva na makondakta wamekuwa wakilalamikia tamko hilo, kwa madai kwamba halikuzingatia hali halisi ya utoaji wa huduma hiyo.
 
Akifafanua, Abdullah alisema kwa sasa bei ya mafuta imepanda kutoka sh. 800 kwa lita hadi sh. 1,300, ambayo ni sawa na asilimia 62 na kwamba kwa mwaka jana pekee ilipanda mara tisa.
 
Mbali na mafuta, alisema, bei ya speai imekuwa ikipanda kutokana na uamuzi wa serikali kuruhusu biashara huria katika sekta ya nishati ya mafuta na spea.
 
Alisema hiyo imekuwa ikichangiwa na baadhi ya wafanyabiashara kujipangia bei kulingana na mahitaji ya soko na faida zao, bila ya kujali wenye mabasi.
 
"Tuliiambia SUMATRA kukerwa kwetu na upandaji holela wa mafuta na kutoridhishwa na tabia ya kulazimika sisi wasafirishaji kupandisha nauli ovyo kwa abiria kama suluhisho la kufidia gharama za uendeshaji. Lakini majibu yalikuwa hayatoki. Tumebeba mzigo wa hasara kwa muda mrefu tukiwa na subira ya kufanyiwa kazi kwa hoja zetu, ikiwemo ya udhibiti wa mafuta.
 
"Aprili, mwaka huu tulikutana na mkurugenzi mkuu wa SUMATRA na kumlilia kupanda kwa bei ya mafuta, spea na matairi na pia kuuziwa spea na matairi kwa dola za Marekani, licha ya thamani yake kubadilika kila kukicha. Pia hatukupata jibu zaidi ya kuambiwa hii ni biashara huria," alifafanua Abudullah.
 
Alisema kama SUMATRA ingesikiliza kilio chao tangu mafuta yalipofikia sh. 800 kwa lita moja, wangekuwa watetezi wazuri wa wananchi, hasa ikizingatiwa kwamba asilimia 99 ya biashara ya usafirishaji inaendeshwa na wazalendo.
 
Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo ameelezea kutokitambua Chama Cha Huduma ya Wasafiri Tanzania (HUWATA), kuwa ni miongoni mwa vyama vya wasafirishaji.
 
Kutokana na hilo, alisema tamko lililotolewa na chama hicho kuhusiana na suala hilo ni batili, kwa kuwa chama hicho hakitambui matatizo ya sekta hiyo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.