Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Dalali avunjwa mguu
Dalali avunjwa mguu
By Habari Tanzania | Published  09/6/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rocken Hill wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wamempiga na kumvunja mguu dalali wa mahakama mkoani hapa.

Dalali huyo alifika shuleni hapo kuwaonyesha mali na majengo wanunuzi wa shule hiyo, ambayo imepigwa mnada kwa amri ya mahakama, anaripoti Anceth Nyahore wa PST.

Wanafunzi walifikia hatua hiyo kwa kile walichodai kuwa dalali huyo, Bw. Abdallah Subira (47) amekuwa na kiherehere cha kuipiga mnada shule yao.

Shule hiyo ni ya kidato cha kwanza hadi cha nne.

Mahakama wilayani humo iliamuru ipigwe mnada baada ya mmiliki wake,
Bw. George Ngh’wagala, kukabiliwa na madeni ya mamilioni ya shilingi, anayodaiwa na wadeni wake.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Bw. Sirro Nyakoro, alisema kuwa dalali huyo alipigwa na wanafunzi hao Septemba 3, mwaka huu, muda mfupi baada ya kuwepo shuleni hapo.

Dalali huyo alikwenda shuleni hapo, ili kukamilisha zoezi la kuwaonyesha wanunuzi wa sekondari hiyo, iliyopo nje kidogo na mji wa Kahama.

Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa dalali huyo alifika shuleni hapo akiwa na wanunuzi wa shule hiyo wa kampuni ya Inter Fumigation Decoration Company Ltd ya jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kuwaonyesha maeneo na mali za shule hiyo wanunuzi hao, dalali huyo aliondoka shuleni hapo kuelekea mjini Kahama.

Bw. Nyakoro alisema baada ya kufika mjini Kahama, Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari, Bw. Charles Lupimo (37), alimpigia simu dalali huyo akimtaka arudi tena shuleni hapo.

Dalali huyo aliitikia wito huo na mara baada ya kufika shuleni, ghafla wanafunzi waliokuwepo , walimvamia na kuanza kumpiga na kumvunja mguu wake wa kulia, chini kidogo ya kisigino.

Kaimu Kamanda alisema kufuatia vurugu hizo, Polisi inamshikilia Mkuu huyo wa Shule, anayedaiwa kula njama za kumpiga dalali huyo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Hamis)
    Unrated
    Mkuu huyo wa shule anapaswa kuhukUmiwa miezi 6 kwa kuvunja amri halali ya mahakama.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.