Mkazi wa Mabatini Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Bw. Manase Robert Mipawa, jana ilikuwa siku yake ya bahati baada ya kujishindia fedha taslimu sh. milioni moja.
Alishinda kitita hicho, katika droo ya kwanza ya shindano kabambe la Nipashe Motomoto, linaloendeshwa na gazeti hili.
Droo hiyo ilifanyika jana katika viwanja vya Magomeni-Kirumba jijini Mwanza.
Ilikuwa ni droo ya kwanza na maalum, kwa ajili ya wasomaji wa Nipashe kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, yenye mikoa ya Mwanza, Mara, Kigoma, Kagera na Shinyanga.
Droo hiyo iliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bw. Charles Linhege.
Mshindi wa pili alikuwa ni Mariam Katemi Raymond wa Makoko mjini Musoma, ambaye alijishindia Sh. 500,000.
Mshindi wa tatu alikuwa John Justine John wa Mahina jijini Mwanza aliyejishindia Sh. 250,000. Mshindi wa nne ni Joseph Kamisa alijinyakulia Sh. 150,000. Pia,washindi kumi walijipatia T-shirt za Nipashe,ambao ni Medard Kapama wa Igoma jijini Mwanza, Emmanuel Mabara wa Buhangija Shinyanga, Daniel Muyala wa Nyakato, Mwanza, Benedict Mkakanzi wa Capri Point Mwanza,ambaye alishinda T-shirt mbili pamoja na Cecilia Charles wa Makoko, Musoma.
Wengine waliojishindia T-shirts ni Moshi Mkombo wa jijini Mwanza, Charles Paul wa Makoko, Musoma, John Justine John wa Mahina, jijini Mwanza pamoja na Pazi Muharami wa Nyakato jijini Mwanza.
Washindi watano waliojipatia kofia za Nipashe ni Wilhald Mkungu wa Bugando jijini Mwanza, Seif Said Mlambalazi wa Kibirizi, Kigoma, Elis Mshango wa Tarime, Zuena Mbegaro wa Makoko, Musoma na Ephasia Malinzi wa Mwisenge, Musoma.
Akizungumza mara baada ya droo hiyo Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya The Guardian Ltd, Bw. Januarius Maganga,aliwashukuru wasomaji wa gazeti la Nipashe kwa kushiriki kwa wingi shindano hili hali inayothibitisha kuwa gazeti hilo linasomwa kwa wingi.