Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mume amkatakata mkewe, ajinyonga
Mume amkatakata mkewe, ajinyonga
By Habari Tanzania | Published  09/6/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mary Ngoboko, Mwanza

WATU watatu wamekufa katika matukio tofauti mkoani hapa, likiwamo la mwanaume kujinyonga baada ya kumkatakata mkewe kwa mapanga.

Tukio la kwanza lilitokea juzi katika kijiji cha Mtakuja wilayani Geita mkoani hapa, ambapo mtu alikutwa amejinyonga.

Akizungumzia tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Zelothe Stephen, alimtaja aliyejinyonga kuwa ni Dominick Jackson (36) na kwamba alijinyonga nje ya nyumba yake.

Kamanda Zelothe alisema marehemu alikutwa amejinyonga kwa kamba ya manila juu ya mti.

Alisema chanzo cha kujinyonga kwa mwanaume huyo ni kumtuhumu mkewe Bibi Theresia Ernest (31) kwamba alikuwa akifanya vitendo vya kiasherati.

Pia Kamanda alisema inadaiwa mkewe huyo alikuwa amefungua mashitaka mahakamani ya kudai talaka.

Kamanda Zelothe alisema siku moja kabla ya tukio saa mbili usiku Dominick alimpiga mkewe na kumkatakata kwa mapanga huku amembeba mtoto Sada Dominick (1) ambao walijeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya wilaya ya Sengerema kwa matibabu.

Alisema mwanamke huyo alilazwa katika hospitali hiyo na baadaye alifariki dunia.

Katika tukio lingine lililotokea juzi, mkazi wa Igombe, Ilemela jijini hapa, Bw. Jadiuo Obeid (21), anahofiwa kufa maji baada ya mtumbwi aliokuwa akiutumia kuvua samaki kupigwa na dhoruba na kuzama.

Kamanda Zelothe alisema inadaiwa kuwa siku hiyo, marehemu na wenzake ambao hawajafahamika, walikwenda kuvua samaki na kuzama.

Kamanda alisema wavuvi wengine ambao alikuwa nao walijiokoa kwa kuogelea huku yeye akishindwa kufanya hivyo na kwamba mpaka sasa hajapatikana.

Aidha Kamanda Zelothe alisema Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wa wananchi na vikundi mbalimbali wanaendelea na kumtafuta mvuvi huyo

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.