Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mtanzania aliyefia Zambia azikwa
Mtanzania aliyefia Zambia azikwa
By Habari Tanzania | Published  09/5/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Kenneth Mwazembe, Mbozi

MAMIA ya wakazi wa mji wa Vwawa wilayani hapa, juzi walijitokeza kumzika Lucas Msuya, aliyefia mikononi mwa polisi wa Zambia wiki iliyopita.

Akiwasilisha salamu za serikali, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Halima Kihemba, amesema msiba huo si wa familia ya Msuya pekee, bali ni wa Watanzania wote kutokana na mazingira ya kifo chake.

Msuya aliuawa na polisi wa Zambia akiwa kwenye mahabusu ya Kituo cha Polisi Nakonde, nchini Zambia.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi wawe watulivu wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, ametuma salamu za rambirambi na sh 100,000 kwa familia ya marehemu ambazo ziliwasilishwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mbozi, Steven Mtengeti.

Kwenye salamu hizo, Mwema aliwataka kutulia na kuahidi kuwa serikali itahakikisha haki inatendeka.

Mwili huo umechukuliwa kutoka Zambia baada ya wataalamu wa upasuaji kutoka Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu wa Zambia kumaliza kuufanyia uchunguzi.

Kifo cha Lukas Msuya, kimekuwa ukombozi kwa watuhumiwa wengine kwani baada ya kufikia muafaka wa pande mbili hizi, mahabusu Watanzania waliokuwa katika kituo cha Nakonde wameachiwa huru.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.