Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kipenga ubunge EAC chapulizwa
Kipenga ubunge EAC chapulizwa
By Habari Tanzania | Published  09/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Fatma Gaffus, Dodoma

KINYANG’ANYIRO cha kutafuta ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kimeanza, ambapo wenye nia ya kugombea tayari wanajipitisha kwa njia mbalimbali, wakijinadi, bila kueleza nia yao.

Wapo wanaoshiriki kupita kiasi katika hafla, wanaotoa misaada maeneo tofauti, na wengine wanaosema sana katika vyombo vya habari, bila kusahau wanaofanya ziara nyingi, kujiweka karibu na jamii.

Lakini ukweli ni kwamba, kipindi kingine kigumu kwa wanaowania uwakilishi kimewadia, kwani wakati ukomo wa Bunge la EAC unakaribia, taratibu za kupata uwakilishi ndani ya vyama tayari zimeanikwa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama ilivyotarajiwa, wameanza mapema, ambapo katika kikao chake cha Kamati Kuu (CC) kilichomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani hapa, wameamua fomu zianze kutolewa wiki ijayo, Septemba 30 na ziwe zimerejeshwa hadi ifikapo saa 10, Septemba 30, wakitoa wiki mbili hivi kwa wahusika.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kwamba, gharama ya kuchukua fomu ni sh 100,000 na kwamba Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itajadili majina hayo Oktoba 10.

Makamba alisema kwamba Oktoba 12, CC itakaa kuteua wagombea, Oktoba 28 kamati ya wabunge wote wa CCM itakaa kufanya uteuzi wa mwisho na Oktoba 30 majina yatapelekwa kwa Katibu wa Bunge.

Muda wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki unamalizika mwishoni mwa Novemba mwaka huu. Mchakato wa kuwapata wabunge hao ni kupitia vyama vya siasa vyenye wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Related Articles
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.