Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CCM njaa kali
CCM njaa kali
By Habari Tanzania | Published  09/4/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

WATUMISHI wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, wameomba kukutana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba ili wamweleze matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake 14, mmoja wa wafanyakazi hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu za kiusalama, alisema unyanyasaji unaofanywa dhidi yao na CCM Mkoa, ni tofauti na dhana halisi ya maisha bora kwa kila Mtanzania inayopigiwa chapuo na Rais Jakaya Kikwete na wasaidizi wake.

Kwa masikitiko makubwa, mtumishi huyo alisema kwamba, kutokana na hadhi na heshima ya chama hicho tawala, imewachukua muda mrefu hadi kuamua kuzungumza bayana mambo hayo, hasa baada ya kuona hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya mkoa aliye tayari kuwasikiliza.

Alisema wakati kima cha chini kwa mfanyakazi ni sh zaidi ya 60,000, tangu waajiriwe wamekuwa wakilipwa sh 40,000 kwa mwezi na hakuna posho ya usafiri wala kutengewa gharama za pango.

Alisema cha kusikitisha ni kwamba, wakati hali ya mambo ikiwa hivyo kwao, viongozi wao wamekuwa katika neema kubwa kwani achilia mbali mishahara minono, usafiri, kupewa mafuta na nyumba, wao wanaambulia kiasi hicho cha sh 40,000 tu.

Wafanyakazi hao wanalalamika kwamba, viongozi wamekuwa wakifaidika zaidi na posho kubwa wanazolipwa na kujipangia safari nyingi za mkoa hadi mkoa, huku wao wakiambulia sh 40,000 tu kwa mwezi mzima, kiasi ambacho wapo wanaopata zaidi ya hicho kwa siku kama posho.

Wengine, walidai, wanajinufaisha wakati wa kampeni kwa kujidai kwenda kupiga debe huku na kule, kumbe ni jinsi ya kujiongezea kipato. Hata kampeni zikiisha, wao huenda mikoa mbalimbali wakijidai wanaimarisha.

“CCM imekuwa ikipiga mbiu kuhusu maisha bora kwa kila Mtanzania. Huu ni wimbo mzuri na mtamu masikioni, hili lilitakiwa lianzie kwetu (CCM) kwani ndio vinara wa mbiu hii, lakini sivyo ilivyo, ni tofauti kabisa,” alisema mfanyakazi huyo.

Alisema kutokana na gharama za maisha, kiasi cha sh 40,000 kwa mwezi ni kidogo mno, kwani kinaishia katika nauli na kula, hivyo akahoji hayo maisha bora kwa Mtanzania yatatoka wapi kama hivyo ndivyo ilivyo ndani ya CCM.

Alisema, wamevumilia, lakini sasa wamechoka na kuamua kusema, si kwa ajili ya kuwakomoa viongozi wao, bali wakubwa wa chama hicho waweze kuelewa nini kinaendelea, kwani pamoja na wao kufikisha malalamiko yao, yamewekwa kabatini na wao kupigwa danadana.

Akitoa mfano hai, alisema Aprili mwaka huu, waliandika barua kuomba kukutana na viongozi ili kufanikisha kilio chao na kuelezwa kikao kingefanyika haraka iwezekanavyo, lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa.

“Tupeleke wapi malalamiko yetu wakati hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kwetu na familia zetu na hakuna anayelijua hili zaidi ya sisi (wafanyakazi) na viongozi wetu? Hivyo tumeamua kutamka bayana ili viongozi wa juu zaidi wasikie,” alisema.

Alisema kwa kiongozi wa CCM anayebisha kuhusu hilo, afike katika ofisi cha chama hicho na kukutana na wafanyakazi na si viongozi, kwani atapewa maneno mazuri na kuona wafanyakazi ni waongo.

Mfanyakazi huyo alisema kwamba, pamoja na kufanyiwa hayo, wangali wakiamini CCM ni chama imara na chenye sera safi, lakini tatizo bado lipo kwa baadhi ya viongozi ambao kwa kutotekeleza sera hizo kwa vitendo, wanakipaka matope chama.

“Hali hii haiishii kutuumiza sisi watumishi, bali pia inakipaka matope chama kilicho mstari wa mbele kupigania haki na maslahi bora kwa Watanzania chini ya kaulimbiu ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’,” alisema.

Baada ya kutafutwa kwa zaidi ya mwezi mmoja na kuahirisha kuonana na Tanzania Daima, hatimaye jana Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Matson Chizii, alisema kwamba malalamiko hayo, kama yapo, hayajafikishwa mezani pake.

Kuhusu kima kidogo cha mshahara, Chizii alisema CCM wana utaratibu nje ya ule wa serikali katika kima cha chini, kwamba wapo watumishi ambao hawajaajiriwa, hivyo hulipwa posho kila mwezi, ambayo hakutaka kutaja ni sh ngapi.

Katibu huyo alisema kwamba, kuhusu walioajiriwa na kima kuwa kidogo, alisema CCM ina taratibu na viwango vyake.

“Hayo malalamiko yao, kwamba wanalipwa chini ya kiwango… ni kiwango kipi? Kiwango cha CCM au cha serikali? Kama ni cha serikali, sisi huko hatupo… tunalipa kulingana na utaratibu wetu,” alijitetea Chizii.

Kuhusu kaulimbiu inayopigiwa debe ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania’ kutotekelezwa katika hili la mishahara, Chizii alisema kila mahali kuna utaratibu wake, na wao (CCM) wanalipwa kuendana na utaratibu waliojiwekea.

Aliahidi kwamba, malalamiko yakifikishwa kwa maandishi ofisini kwake, yatashughulikiwa. Tangu wakati wa kampeni hadi sasa, Kikwete na wasaidizi wake wamekuwa wakisisitiza maisha bora kwa kila Mtanzania, lakini wafanyakazi wa makao makuu wanaona kwamba wema unatakiwa uanzie nyumbani


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.