WAKAZI watatu wa Dar es Salaam wameibuka washindi wa sh milioni 2.3 katika bahati nasibu ya kila wiki ya taifa ya Kismati SMS katika droo iliyofanyika Dar es Salaam, jana.
Washindi hao ni Atilo Vahaye aliyejipatia sh milioni 1.8 kupitia namba ya ushindi SR945522; wakati Francis John na Gift Mwaipopo walipata sh 300,000 na sh 200,000 kupitia namba DF947313 na VR222669.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Biashara wa Selcom Gaming, Lengarivo Marti, katika droo nne za kila wiki kwa Agosti pekee, washindi mbalimbali wamepata jumla ya sh milioni 8.6.
Alisema droo kubwa ya mwezi itafanyika keshokutwa ambako washindi watatu watapata sh milioni 25; ikilinganishwa na sh milioni 12 mwezi Julai.
“Zawadi kwa washindi zimekuwa zikiongezeka wiki hadi wiki mpaka mwezi kutokana na ongezeko la ushiriki wa watu wengi,” Marti alisema.
Katika droo kubwa ya mwezi; mshindi wa kwanza atapata sh milioni 12.5; wa pili sh milioni 7.5 na wa tatu atajinyakulia sh milioni tano.
“Ongezeko la ushiriki katika bahati nasibu hii ya Kismati SMS inaonyesha imani waliyo nayo Watanzania juu ya uwazi na zawadi kubwa zitolewazo kwa washindi,” alisema.
Tangu bahati nasibu hiyo ianze rasmi mwishoni mwa mwaka jana, sh zaidi ya milioni 60 zimeshatolewa kwa washindi nchini kote.
Bahati nasibu hiyo ambayo ushiriki wake ni kwa kutuma ujumbe mdogo wenye neno ‘pesa’ kupitia namba 15777, unasimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini