Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwenyekiti amdunda mbunge
Mwenyekiti amdunda mbunge
By Habari Tanzania | Published  08/30/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi, Jimbo la Jang’ombe, Zanzibar, Omar Said Ameir, amempiga Mbunge wa Mpendae, Issa Kassim Issa (CCM).

Mtafaruku huo wa aina yake ulitokea juzi wakati viongozi hao wakiwa katika kikao cha kujadili mipango ya kuimarisha chama na kutathmini utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2005 – 2010.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema kwamba, mwenyekiti huyo alimshutumu mbunge huyo kuwa uwezo wake katika utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ni mdogo na anasababisha kutofikiwa malengo mengi.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi, Wilaya ya Mjini Unguja, Ramadhan Hamza, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kusema kwamba suala hilo hivi sasa lipo katika orodha ya mambo yatakayojadiliwa na Kamati ya Maadili ya Chama.

Alisema kwamba alipokea ripoti kuhusu mbunge kupigwa, lakini walishindwa kulijadili suala hilo katika kikao chao cha juzi kwa vile lilichelewa kuwasilishwa.

“Tunatarajia ripoti hii kuijadili katika kikao cha maadili kijacho kwa vile tukio hili linakwenda kinyume na maadili ya uongozi,” alisema.

Omar ni miongoni mwa wana CCM waliojitokeza kuchuana katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo jipya, na aliangushwa na Issa.

Kuna madai kwamba wana CCM katika Jimbo la Mpendae wamegawanyika makundi kutokana na “makovu” yaliyojitokeza wakati wa kura za maoni.

Hamza alisema kwamba tatizo hilo limeshaanza kushughulikiwa kwa vile kuendeleza makundi ni kwenda kinyume cha taratibu za chama.

Akizungumzia tukio hilo, Mbunge Issa, alikiri kwamba ni kweli alipigwa, na akasema hana la kusema kwa vile suala hilo sasa linashughulikiwa katika uongozi wa chama chake.

“Kwa sasa suala hili sitaki kulizungumza kwa urefu kwa vile nimeshawakabidhi viongozi chamani na nitakuwa nakwenda kinyume na maadili ya uongozi,” alisema.

Alisema kwamba ameamua kuliwasilisha chamani suala hilo badala ya polisi licha ya kuwa ni la jinai, kwa kuwa anaamini kuna “mkono wa siasa” ndani yake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wazazi amekana kumpiga mbunge huyo.

“Mimi sijampiga bwana, kama ana ushahidi aende mahakamani,” alisema Omar.

Endapo Omar atathibitika kuwa alimpiga mbunge huyo, adhabu yake ni pamoja na kuvuliwa uongozi au kufukuzwa katika chama


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.