Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mauaji ya kutisha Musoma
Mauaji ya kutisha Musoma
By Habari Tanzania | Published  08/29/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

MAUAJI ya kutisha yametokea Wilaya ya Musoma mkoani Mara, huku watu wanne wakiuawa, watatu kwa kuchinjwa na mwingine kwa kupigwa mshale.

Katika tukio la kwanza, Watanzania wawili wenye asili ya Kiasia, mtu na mkewe, wameuawa na watu wasiojulikana ndani ya nyumba yao eneo la Majita Road mjini Musoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, David Saibul, alizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana na kuthibitisha taarifa hizo.

Aliyeuawa alitambuliwa kuwa ni Mzee Hirji Bhanji, na mkewe ambao wote walikuwa ni wazee.

Watu waliozungumza na Tanzania Daima walisema mauaji hayo huenda yalifanywa Jumamosi iliyopita, kwani wazee hao hawakuonekana kanisani siku ya Jumapili kama ilivyo kawaida yao.

Hawakuwa na mfanyakazi nyumbani kwao, isipokuwa mlinzi na mbwa wao wawili - Jimmy na Rocky.

“Wameuawa na maiti wamekaa ndani kwa siku kadhaa, kwani baada ya kutowaona kanisani na dukani, ilibidi watu waliowajua waanze kufuatilia.

“Walifika nyumbani na walipoingia, walikuta maiti ya mzee Bhanji na mkewe, hapakuwapo mlinzi, inawezekana alishirikiana na watu wengine kuwaua wazee hao,” alisema Kamanda Saibul.

Alisema dalili za awali zinaonyesha kuwa wauaji hao walipekua kila mahali ndani ya nyumba hiyo baada ya kuwaua wazee hao.

Kamanda hakuwa na takwimu sahihi za mali au fedha zilizoporwa, na kwamba uchunguzi unaendelea.

Katika tukio jingine, mama na mtoto wameuawa katika Kijiji cha Butuguri, Musoma Vijijini.

Habari kutoka kijijini hapo zilisema kuwa watu hao waliuawa kutokana na imani za kishirikina.

“Walifika nyumbani, mtoto alipigwa mshale, akafa, wakachoma nyumba, mama alipojaribu kutoka, alipigwa panga na kutenganisha kiwiliwili,” alisema mwananchi mmoja kutoka Butuguri.

Huu ni mfululizo wa matukio ya mauaji mkoani Mara. Katika siku za karibuni, mauaji ya aina hiyo yametokea sehemu mbalimbali za mkoa wa Mara, ikiwamo Wilaya ya Tarime.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.