Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ndoa katika umri mdogo hukatiza masomo
Ndoa katika umri mdogo hukatiza masomo
By Habari Tanzania | Published  08/28/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, (TAMWA) kimesema ndoa katika umri mdogo na ubakaji vinachangia wasichana kukatiza masomo na kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Ananilea Nkya alisema ofisini kwake Jijini Dar es Salaama jana kufuatia utafiti uliofanywa na chama chake katika wilaya tano nchini.

Alisema utafiti huo uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 77 ya watu 992 waliohojiwa katika wilaya za Bagamoyo na Rufiji mkoani Pwani na Mvomero, Ulanga na Kilombero mkoani Morogoro walisema kuwa ubakaji na wasichana kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo kunachangia wasichana wengi kukosa elimu na kuenea kwa virusi vya Ukimwi.

Bi. Nkya alisema kwa mujibu wa utafiti huo, jumla ya wasichana 163 wenye umri chini ya miaka 18 walijifungua katika hospitali ya misheni ya Mchukwi, Rufiji kati ya mwaka 2004 na mwezi Juni mwaka huu.

Alisema wengine kati yao walijifungua wakiwa na umri chini ya miaka 11 jambo ambalo linaonyesha kuwa watoto wa kike wanalazimishwa kujiingiza katika vitendo vya kujamiiana wangali wadogo.

Aidha utafiti huo unaonyesha kuwa kati ya wajawazito 215 waliopatiwa ushauri nasaha na kupima katika hospitali ya Utete katika kipindi cha mwanzo wa mwaka huu wengi wao wakiwa ni wasichana wenye umri mdogo, 12 kati yao ambao ni sawa na asilimia sita walikuwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Alisema utafiti pia umeonyesha kuwa kesi 352 zilizofunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Bagamoyo kati ya mwaka jana na Juni mwaka huu, kesi 85 zilikuwa za ubakaji zikiwahusisha wasichana wenye umri wa chini ya miaka 18.

Kwa upande wa Morogoro, alisema utafiti huo umeonyesha kuwa wasichana wawili wanafunzi wa shule ya msingi Wami Dakawa waliripotiwa kubakwa wakati wakienda shule na watuhumiwa walitoroka wakati kesi inaendelea mahakamani.

Alisema baadhi ya wasichana wengi wa mikoa ya Pwani na Morogoro walisema mambo yanayochangia wasichana wengi kuolewa katika umri mdogo ni pamoja na wengi kutochaguliwa kujiunga na shule za sekondari na kutokuwepo kwa vyuo vingi vya ufundi kwa ajili ya kujiendeleza baada ya kumaliza shule ya msingi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.