Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  NIC sasa wanakula mtaji’
NIC sasa wanakula mtaji’
By Habari Tanzania | Published  08/26/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na James Marenga

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC), liko katika hali mbaya kifedha, na kwamba sasa linaendesha shughuli zake kama mfanyabiashara anayekula mtaji.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), Ally Karavina, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam.

Alikuwa akitoa taarifa za mwenendo wa ubinafsishaji wa NIC na ukodishwaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha na Uchumi.

Alisema kwa sasa NIC inaendesha shughuli zake kwa kutegemea ruzuku inayotolewa na serikali ambayo inafikia sh bilioni 52 kwa mwaka.

“Shirika hili limekuwa likijiendesha kwa hasara, njia nyingi ambazo si halali, watendaji wake wakishirikiana na waliokuwa na bima, wamekuwa wakilihujumu shirika hili kwa kupewa fidia kubwa kinyume na taratibu,” alisema Karavina.

Alitoa mfano kwamba gari moja ambalo limekatiwa bima lilipopata ajali lililipiwa bima hata mara sita kwa kutumia nyaraka tofauti.

Mwenyekiti huyo alisema wabunge wamekuwa wakipokea taarifa zisizo sahihi kuhusu ubinafsishaji wa shirika hilo.

Alisema mjadala uliokuwapo kwenye Mkutano wa Nne wa Bunge uliomalizika hivi karibuni, taarifa zake zimekuwa hazina ukweli na zinawachanganya wananchi.

“Shirika hili mpaka sasa halijapata mwekezaji na kilichofanyika ni hatua za awali, zikiwamo kutangaza tenda na kuwapata baadhi ya wawekezaji walionyesha nia ya kulinunua,” alisema.

Alisema taarifa zinazoandikwa kwenye vyombo vya habari na zile zinazozungumzwa kuwa NIC inauzwa kwa bei chee na kutupiwa lawama PSRC, hazina ukweli.

“Huwezi kuuza shirika kama NIC kwa sh bilioni tatu kama inavyoelezwa, na siwezi pia kuuza majengo ya shirika hilo kwa mwekezaji kwa sababu ni mali ya wenye amana, kitakachouzwa ni biashara ya NIC,” alisema.

Alisema jengo kama Life House, lililopo jijini Dar es Salaam haliwezi kuuzwa bila ya kuwa na makubaliano na wenye amana.

Karavina alisema kudumaa kwa NIC kibiashara kunatoka na ushindani wa biashara ya bima uliotokana na kupitishwa kwa sheria inayoruhusu kuwapo mashirika mengine ya bima.

“Mashirika mengi yamekuja na kufanya biashara, awali NIC ilikuwa ndilo shirika pekee lililofanya biashara ya bima, lakini sasa ni biashara ya ushindani,” alisema.

Kamati hiyo ya Bunge iliitaka PSRC kufanya kikao cha pamoja na uongozi wa NIC na wafanyakazi na kutafuta ufumbuzi wa pamoja kuhusu ubinafsishaji wa shirika hilo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.