Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kikwete azidi kuwa mwiba
Kikwete azidi kuwa mwiba
By Habari Tanzania | Published  08/25/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na David Frank, Arusha

RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali haiwezi kuwanyang’anya wananchi mamlaka yao na kuwapatia wakuu wa wilaya kwa kuwa kufanya hivyo kutakuwa ni kufisha utamaduni wa misingi ya demokrasia ya utawala bora kwa nchi inayojengwa kwa misingi ya utawala bora na demokrasia.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa semina elekezi ya wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu watendaji, alitoa ufafanuzi huo wakati alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa semina hiyo inayoendelea hapa Ngurdoto.

“Tunajenga utamaduni wa utawala wa kidemokrasia, na hili ni muhimu sana, lazima mlizingatie. Hatuwezi kumkabidhi mtu mmoja awe na sauti kuliko mamlaka ya watu wengine kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa na wananchi,” alisema.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari msaidizi wa rais, Maura Mwingira alisema Rais Kikwete aliongeza kwamba haiwezekani mkuu wa wilaya awe mkubwa kuliko watu wote, kutokana na ukweli kwamba halmashauri ndio mamlaka ya watu.

“DC huwezi kuwa na mamlaka ya kila kitu, huwezi kupewa mamlaka ya veto, hii ni mbaya kwa nchi inayojenga misingi ya utawala bora na utawala wa kidemokrasia," ilisema taarifa ya mwandishi huyo wa rais.

Rais Kikwete alibainisha kwamba inawezekana kabisa kukawa na migongano ya kiutendaji na uhusiano kati ya watendaji wa halmashauri na wawakilishi wa serikali.

Alisema watashughulikia na kuangalia ni kwa namna gani hawa wenye mamlaka ya watu (halmashauri) watakavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na mwakilishi wa serikali kuu (DC).

Aliwataka wakuu hao kuzingatia uhusiano mzuri na watu wote walio chini yao na kuachana na mtizamo wa kuwa wao ni wakubwa. Na kuonya kuwa wakienda na mtizamo huo wa ukubwa hapana shaka kuwa watendaji walio chini yao na wananchi hawatatoa ushirikiano kwao na hatimaye watabaki peke yao.

Baadhi ya wajumbe ambao walichangia mada iliyotolewa na mbunge wa Jimbo la Kwela, Chrisant Mzindakaya, ambaye alitoa mada kuhusu nafasi na majukumu ya wakuu wa mikoa, makatibu tawala na wakuu wa wilaya, walielezea kuwa uwepo uwezekano wa kuwahamisha watendaji wa kata na vijiji ambao baadhi yao utendaji wao si mzuri, wawe chini ya wakuu wa wilaya ili waweze kuwadhibiti.

Katika mada yake, Mzindakaya ambaye amewahi kuwa mkuu wa mkoa kwa miaka 13, naibu waziri miaka 9 na mbunge kwa miaka 40, alikuwa akielezea uzoefu wake katika uongozi wake wa ukuu wa mkoa kwa wajumbe wa semina hiyo.

Aliwataka viongozi hao kuwa viongozi wa mfano kwa kuonyesha njia. “Unawahimiza wananchi walime, ili hali wewe mwenyewe hata kulima nyanya hujui,” alisema na kuwachekesha wajumbe.

Alisisitiza kuwa wakuu wa mikoa na wilaya lazima wawe wabunifu, wawatumie watu walionao wakiwamo wataalamu kutoka vyuo mbalimbali ili waweze kusukuma kwa kasi maendeleo ya wananchi kama alivyowahi kufanya yeye wakati wa enzi zake.

Alisema kuwa moja ya kazi ya mkuu wa mkoa ni kulea wakuu wa wilaya, kujua kalenda zao za kazi na yeye mwenyewe kuwapatia ya kwake na kuwatembelea katika maeneo yao ya kazi na kukagua utekelezaji wa mipango waliyojiwekea.

Mzindakaya alieleza kwa kina namna alivyotumia utundu na ubunifu katika kuifanya mikoa aliyoiongoza kuwa ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara, utumiaji wa zana za kisasa za kilimo, matumizi bora ya rasilimali watu na ushirikishaji na uanzishwaji wa vyama vya kuweka na kukopa.

Mikoa aliyowahi kuongoza ni Morogoro, Kigoma, Mbeya na Rukwa.

Aidha, Mzindakaya aliwataka wakuu wa mikoa kuwatumia vema viongozi wote wanawake walioko katika mikoa yao kwa kile alichosema kuwa wanawake wameonyesha uwezo mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa tu watatumiwa vizuri na kupewa nafasi ya kufanya hivyo.

Katika mada yake hiyo ambayo ilikuwa somo tosha kwa wajumbe hao, alisisitiza kuwa kama hakuna mipango ya kazi na usimamizi kwa watu, basi watu wote wanakuwa ni wavivu. Kauli iliyoungwa mkoni na Rais Jakaya Kikwete.

Aliwataka wakuu hao wa mikoa na wilaya kutobweteka na kusubiri fedha za bajeti, bali kubuni mbinu za kujiongezea mapato katika maeneo yao ya kazi, ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi watendaji wao ili waweze kuchapa kazi na kutoa tija.

Mada nyingine zilizowasilishwa jana ni pamoja na hifadhi na uboreshaji wa mazingira Tanzania, uzingatiaji wa sheria na kanuni katika matumizi ya fedha za serikali na nidhamu ya matumizi ya fedha za serikali


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.