Na. Prosper Kwigize
Kibondo
Ushirika wa akiba na mikopo SACCOS wilayani Kibondo mkoani Kigoma umefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni moja baad aya kufungua milango kwa wananchi kujiunga na ushirika huo.
Zaidi ya hisa 217 zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nane zimeuzwa na ushirika wa kuweka na kukopa Saccos wilayani Kibondo katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
Hayo yamebainishwa na katibu wa muda wa Ushirika huo Bw Robert Ntendeli wakati akitoa taarifa katika mkutano wa uchanguzi wa viongozi wa Ushirika huo uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha vijana wilayani Humo.
Bw Ntendeli amesema Ushirika Kibondo hadi sasa una hisa elfu themanini zenye thamani ya shilingi milioni mia nne.
Aidha amebainisha kuwa ili kuepukana na tatizo la Soccos kuhodhiwa na wanachama wachache wameweka kiwango ambacho kila mwanachama anauwezo wa kununua hisa na haruhusiwi kuzidisha hisa mia nne.
Wananchama wa ushirika huo ili weweze kupata mikopo kutoka katika ushirika, anatakiwa awe na hisa isiyopungua mia moja na hamsini ambapo hisa moja inauzwa kwa shiringi elfu tano tu.
Uahirika wa Kibondo ulianzishwa mwezi machi mwaka huo na kupewa usajiri juni 19�mwaka kufuatia kauli mbiu ya serikali kuwahimiza wananchi kuunda na kujiunga katika vyama vya ushirika wa akiba na mikopo ili kupata uwezeshaji toka serikalini na katika mashirika ya fedha.