Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  AFISA MTENDAJI WA KIJIJI (VEO) AKATALIWA NA WAJUMBE WA SERIKALI
AFISA MTENDAJI WA KIJIJI (VEO) AKATALIWA NA WAJUMBE WA SERIKALI
By Prosper Kwigize | Published  08/24/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na. Prosper Kwigize
Kibondo
 
Afisa mtendaji wa kijiji cha nyaruyoba katika kata ya Busagara Zacharia Filbert amekataliwa na wajumbe  wa serikali ya kijiji kwa kile kinachodawa kushindwa kufanya kazi.
 
Kwa mujibu wa muhitasari wa kikao cha serikali ya kijiji  kilichokaa tarehe 21 mwezi huu afisa huyo   amedaiwa kutoshirikiana na viongozi  pamoja na  wananchi katika kuleta maendeleo..
 
Kikao hicho ambacho nakala ya mhitasari wake umepatikana katika mtandao wa www.habaritanzania.com, kimebainisha kuwa kiongozi huyo haendi kabisa sambamba na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya nne ya  ari, nguvu na kasi mpya na amekuwa kikwazo kwa maendeleo ya kijiji cha Nyaruyoba.
 
Aidha Bw, Zacharia anatuhumiwa kwa makosa makuu matatu ambayo ni kutotekeleza maagizo mbalimbali ya vikao vya kijiji, kutotoa taarifa ya mapato na matumizi, na kulewa pombe saa za kazi.
 
Afisa mtendaji huyo anatuhumiwa pia kukusanya ushuru na faini mbalimbali bila kutoa stakabadhi na kwamba pesa zinazotozwa kutokana na faini ya mifugo wanaozagaa huzitumia kwa maslahi binafsi bila taarifa.wala idhini ya serikali ya kijiji.
 
Bw. Zacharia pia anadaiwa kupokea Rushwa ya pombe kutoka kwa wananchi wenye shida na mwananchi asiyetoa hapewi huduma harali za kijiji na wakati mwingine afisa huyo hushiriki kucheza kamali.jambo  ambalo ni kinyume na taratibu za nchi
 
Kikao cha wajumbe wa serikali ya kijiji hicho wamemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Bw Paul Nkulila kumhamisha kituo cha kazi mtendaji huyo na wamependekeza achukuliwe hatua za kinidhamu.
 
Hii ni imekuwa ni desturi kwa wananchi pamoja na wajumbe wa serikali za vijiji wilayani Kibondo kuwakataa watendaji wa vijiji kwa tuhuma za uzembe na uzorotaji wa maendeleo katika vijiji vyao ambapo mwezi uliopita afisa mtendaji wa kijiji cha Kigendeka naye alikataliwa na wananchi na kushushiwa kipigo toka kwa wananchi wenye hasira.kwa madai ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.
 
Jinamizi hili pia limewahi kuwakumba watendaji wa vijiji vya Kigogo na Mukabuye ambao walikataliwa na wananchi mara tu baada ya kuhamishiwa katika vituo vyao na kupelekea kuwepo kwa maandamano makubwa ya wananchi kupinga uhamisho wao kwa kile kinachodaiwa kuwa halmashauri imekuwa na desturi ya kuwahamishia watendaji wabovu katika vituo vingine vya kazi

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.