Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bemba ashambuliwa, mabalozi 14 waokolewa
Bemba ashambuliwa, mabalozi 14 waokolewa
By Habari Tanzania | Published  08/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
KINSHASA, DR Congo

UMOJA wa Mataifa (UN) juzi uliwaokoa mabalozi 14 kutoka nyumbani kwa Makamu wa Rais, Jean-Pierre Bemba baada ya jumba lake walimokuwa wakikutana naye kupigwa mabomu siku moja baada ya matokeo ya raundi ya kwanza ya uchaguzi kutolewa juzi.

Mabalozi wa kamati ya kimataifa wanaoratibu mchakato wa uchaguzi inayojulikana kwa ufupisho wa Kifaransa kama CIAT, walikuwa wakikutana na Bemba baada ya shambulio hilo.

Wakati hilo likitokea, mapigano kati ya vikosi vinavyomtii Rais Joseph Kabila na vile vya Bemba yaliendelea kwa siku ya tatu mjini hapa jana katika eneo ambalo mabalozi hao waliokolewa.

Chanzo cha habari cha kidiplomasia kilisema: “Kulikuwa na mashambulizi makali ya risasi, pengine mabomu ya mkono, maroketi na bunduki kali na nzito aina ya machine guns.

“Helikopta binafsi ya Bemba iliharibiwa na wanadiplomasia wa CIAT walitafutiwa uficho katika jumba hilo.

“Mashambulizi hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa kabla ya utulivu kurudi.”

Pamoja na mazungumzo kati ya pande mbili zinazopingana kufanyika jana, pia mapigano yaliendelea na kuzua hofu ya kufumuka kwa vita.

Vyanzo vya habari vya kijeshi vya magharibi vilisema kuwa askari wa kikosi cha Republican Guard, kinachomtii Kabila, walihusika na shambulio hilo.

Waziri wa Habari wa DRC, Henri Mova Sakanyi, ambaye yuko karibu na Kabila, aliwatuhumu wafuasi wa Bemba kwa kuanzisha machafuko hayo.

Wanadiplomasia hao walifungiwa katika jumba la Bemba kwa saa kadhaa kabla ya kuhamishwa.

CIAT inawakilisha wanadiplomasia watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN, Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Marekani pamoja na wa Angola, Ubelgiji, Canada, Gabon, Afrika Kusini na Zambia na maofisa wa timu ya waangalizi wa amani wa UN (Monuc), Jumuiya ya Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU).

Mapigano makali kati ya vikosi vya wafuasi wanaomtii Kabila na wale wa Bemba yalianza Jumapili baada ya Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) kutangaza matokeo ya uchaguzi huo wa kihistoria wa urais na wabunge.

Kabila alishinda kwa kupata asilimia 44.8 huku makamu wake na aliyekuwa kiongozi wa waasi Bemba, akishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 20.

Kutokana na Kabila kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 zinazohitajika, uchaguzi wa marudio kati ya wagombea hao utafanyika Oktoba 29, mwaka huu.

AFP


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.