Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Rais Kikwete aenda kusabahi Angola
Rais Kikwete aenda kusabahi Angola
By Habari Tanzania | Published  08/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Shabani Matutu

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuondoka nchini leo kuelekea Angola kwa ziara ya siku mbili.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu mwishoni mwa wiki ilisema kuwa ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake katika nchi jirani na zilizo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) alizokuwa ameanza kuzifanya mapema mwaka huu.

Nchi ambazo Rais hakupata fursa ya kuzitembelea ni Angola, Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Hakwenda Malawi na DRC kwa vile kulikuwa na harakati za kisiasa, ikiwa ni pamoja na matayarisho ya uchaguzi mkuu DRC. Nchi nyingine, marais hawakuwapo kutokana na majukumu mbalimbali

Katika ziara hizo, Rais Kikwete huchukua fursa ya kujitambulisha kisiasa na pia kuelezea nia ya Tanzania kukuza na kufanya biashara kati yake na nchi hizo.

Rais Kikwete amefanya ziara za namna hiyo katika nchi za Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Swaziland na Afrika Kusini.

Pia ameshazuru Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Katika ziara ya Angola, Rais ataongozana na mkewe, Mama Salma; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha - Rose Migiro; na Waziri wa Utalii, Biashara na uwekezaji wa Zanzibar, Samia Suluhu Hassan.

Wengine ni Mbunge wa Ngara, Feethan Banyikwa (CCM); na Mbunge wa Manyoni Magharibi, John Lwaji (CCM).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.