Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Vigogo Bara, Visiwani kukutana Ngurdoto
Vigogo Bara, Visiwani kukutana Ngurdoto
By Habari Tanzania | Published  08/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

VIONGOZI wa ngazi ya juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Mapinduzi Zanzibar, kuanzia kesho watakuwapo Ngurdoto, kilometa 25 nje ya Jiji la Arusha kwa mkutano wa siku tano wa wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa wilaya.

Rais Jakaya Kikwete atafungua na kuwa mwenyekiti wa semina elekezi hiyo itakaojadili utekelezaji wa kazi za serikali ya awamu ya nne. Itamalizika Agosti 26.

Viongozi wengine watakaokuwapo ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein; Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume; Waziri Mkuu, Edward Lowassa; na Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.

Wakuu wa mikoa watakaoshiriki ni pamoja na wa mikoa mitano ya Tanzania Visiwani na wakuu wa wilaya za mikoa hiyo. Tanzania ina mikoa 26.

Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu ambao wizara zao zitatoa mada, pia watashiriki.

Jaji Mkuu, Barnabas Samata; Spika wa Bunge, Samuel Sitta; Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali George Waitara; na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, ni miongoni mwa watakaotoa mada.

Madhumuni ya semina hiyo ni kuwapa nafasi wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa wilaya ya kupata malekezo kuhusu vipaumbele vya awamu ya nne, baada ya rais kukamilisha kupanga safu ya viongozi hao.

Kwa vile shughuli za maendeleo zimepelekwa kwenye halmashauri zilizo chini ya Serikali za Mitaa, viongozi hao wa mikoa ndiyo wasimamizi wa Serikali za Mitaa.

Karibu maandalizi yote yamekwishakamilika kwa ajili ya semina hiyo.

Semina ya aina hiyo imeshafanywa kwa mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu. Ilifanyika hotelini hapo Machi, mwaka huu.

Rais Kikwete tayari amekwishazitembelea karibu wizara zote na kutoa maelekezo ya utendaji kazi.

Waziri Mkuu, Edward Lowassa naye amekuwa akifanya ziara huku na kule kuhimiza utekelezaji.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.