Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Afrika Kusini yafikiria kupatanisha Kony na Uganda
Afrika Kusini yafikiria kupatanisha Kony na Uganda
By Habari Tanzania | Published  08/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
JUBA na KAMPALA

SERIKALI ya Afrika Kusini inafikiria uwezekano wa kusimamia mazungumzo ya amani kati ya Serikali ya Uganda na waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA) baada ya kupewa ombi hilo na waasi hao.

Naibu wa LRA, Vincent Otti, juzi alisema kuwa anaendelea na msimamo wake kwamba Afrika Kusini iwe mpatanishi wa mazungumzo yenye lengo la kukomesha vita ya miaka 20 ya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mwa Uganda kwa kumpigia simu balozi wa nchi hiyo mjini Kampala.

Otti, alimpigia simu Balozi wa Afrika Kusini nchini hapa, Thandouyife Chiliza saa 10:30 jioni juzi akimtaka awasiliane na serikali ya nchi hiyo iingilie kati katika mazungumzo ya amani yanayoendelea kwenye mji mkuu wa kusini mwa Sudan, Juba.

Chiliza aliliambia gazeti la Daily Monitor siku hiyo kwamba, “LRA wametupigia simu na sasa tunawasiliana na Pretoria (mji mkuu wa Afrika Kusini] juu ya suala hili.”

Mjini Juba, mkuu wa ujumbe wa LRA Martin Ojul, alisema kuwa LRA pia imetuma barua Kampala “ambayo kwa sasa itakuwa imeshawasili Pretoria.”

Hata hivyo, serikali ya Uganda ilieleza kutofurahishwa kwake na uamuzi wa LRA kuwasiliana na Afrika Kusini kusimamia mazungumzo hayo kati ya Kampala na Joseph Kony.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa serikali, Kirunda Kivejinja alisema kuwa itakuwa vigumu kwa Afrika Kusini kuchukua kazi hiyo wakati huu.

“Tayari tumeshazungumzia masuala muhimu katika mazungumzo. Kwa nini LRA wanaleta suala hili leo? Lakini haitakuwa rahisi kumbadili mpatanishi kwa sababu Sudan Kusini ni mpatanishi wa mazungumzo katika hatua hii,” Kivejinja alisema.

Jumatano jioni, Otti, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza, BCC, alisema kuwa waasi wamepiga kura ya kutokuwa na imani na upatanishi wa Dk. Riek Machar, makamu wa rais wa Sudan Kusini, wakihoji juu ya uhalali wake kuegemea upande mmoja na kutaka Afrika Kusini ichukue nafasi.

Hata hivyo, Balolzi Chiliza alisema kuwa serikali yake haijaombwa kuchukua moja kwa moja jukumu la upatanishi zaidi ya kuwa wapatanishi wenza. “Tunavyofahamu si kuchukua jukumu zima bali kusaidia na kuboresha mchakato unaoendelea. Hiyo ni kutokana na mwito na mwaliko tuliopewa na LRA,” Chiliza alisema.

MONITOR


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.