Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  GSB yawafariji Serengeti Boys
GSB yawafariji Serengeti Boys
By Habari Tanzania | Published  08/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Deodatus Mkuchu

LICHA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufuta safari ya timu ya soka ya Tanzania ya vijana wa chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kwenda Uingereza, Kampuni ya Global Scouting (GSB), inatarajiwa kutoa sh 500,000 kwa kila mchezaji na makocha wawili ambao kila mmoja atalamba sh milioni moja.

Uamuzi huyo umekuja siku moja tu tangu Rais wa TFF, Leodegar Tenga kufuta rasmi safari hiyo iliyopaswa kuwa Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kucheza mechi za kirafiki na timu za Chelsea na Watford za England.

Pamoja na kuandaliwa kwa kikosi cha wachezaji 18, safari hiyo ilisitishwa na GSB kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kwa TFF kushughulikia viza, hivyo ili kuepuka hasara, GSB iliamua kusitisha safari siku moja kabla.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwakilishi wa Kampuni ya GSB nchini, Abdul Mteketa, alisema kwamba pamoja na kukwama kwa safari hiyo, GSB imeamua kutoa kiasi hicho kwa wachezaji 18 na makocha waliokuwamo katika safari hiyo.

Mteketa alisema uamuzi huo ni kuwatia moyo wachezaji baada ya kupoteza muda mwingi na ngumu kwa ajili ya safari hiyo, na kwamba kushindikana kwa safari hiyo, si kosa lao, hivyo wanastahili kifuta jasho.

“Vijana wamepoteza muda na nguvu zao kujiandaa kwa safari, hivyo tutatoa kiasi cha sh 500,000 kwa kila mchezaji aliyepaswa kuondoka na makocha wawili watapata sh 1000,000 kila mmoja,” alisema Mteketa.

Ingawa TFF inalalamikia kitendo cha GSB kusitisha safari bila kutoa taarifa, Mteketa bado anashikilia kuwa, kukosekana kwa viza kulichangiwa na TFF wenyewe na kwamba, huenda Tenga anapotoshwa na maofisa wake.

“Tunasisitiza kuvurugika kwa safari ya vijana England kumechangiwa na TFF wenywe, kwa kushindwa kushughulikia mapema viza, kwa bahati mbaya Tenga inaonekana anapotoshwa na watendaji wake,” alisema Mtekete.

Wachezaji waliotakiwa kuwamo katika safari hiyo ni Enock Haule, Hashim Nzota, Homoud Salum, Shaaban Kassim, Zahor Pazi, Muhsin Salim, Yassin Juma, Uliza Ugama, Jacob Peter na Habib Mhina.

Wengine ni Abeid Kissiga, Edward Christopher, Mecky Michael, Musiba Seleman, Lameck Dyton, Hafidh Halfan, John Simbeya na Kigi Makasi Kigi. Makocha ni Rogasian Kaijage na Sylvester Marsh.

Alisema fedha hizo kwa wachezaji na makocha zitatolewa mwishoni mwa mwezi huu na kusisitiza kuwa, ili kuthibitisha kuwa GSB si kampuni ya ubabaishaji, itawaleta makocha maarufu wa England akiwamo Sir Bob Charlton.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.