Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kaya 179 Songea hazina vyoo
Kaya 179 Songea hazina vyoo
By Habari Tanzania | Published  08/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Albano Midelo, Songea

KAYA 179 katika kata nne za Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Ruvuma hazina vyoo, hali ambayo inahatarisha afya za wananchi hao kupata magonjwa ya mlipuko.

Mratibu wa Huduma ya Afya ya Msingi (HAM) katika Tarafa ya Ruvuma, Abel Mapunda, aliiambia Tanzania Daima juzi kuwa waligundua tatizo hilo katika utafiti walioufanya katika kata hizo kupitia kampeni ya ‘piga kambi’ yenye lengo la kuhamasisha jamii kujenga vyoo na kuvitumia.

Alizitaja kaya ambazo hazina vyoo kuwa ni katika Kata ya Litisha ambako kaya 37 hazina vyoo, sawa na asilimia 13.6, Kata ya Kilaghano kaya 41 hazina vyoo, sawa na asilimia 10.4, Kata ya Maposeni kaya 66 hazina vyoo, sawa na asilimia 13.6 na Kata ya Lilambo kaya 35 hazina vyoo, sawa na asilimia 5.

Mratibu huyo alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo, kampeni ya piga kambi katika kata hizo itaendelea, ili kuhamasisha wananchi kujenga vyoo na kuvitumia, ili kupunguza tatizo la magonjwa ya kuhara, ukiwamo wa kipindupindu katika tarafa hiyo.

Alisisitiza kuwa Tarafa ya Ruvuma kupitia mpango wa kuboresha afya ya msingi umejiwekea malengo ya kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la ugonjwa wa kuhara ifikapo Desemba mwaka huu kupitia kampeni ya piga kambi.

Naye Katibu Tarafa ya Ruvuma, Abdula Mbawala, ameagiza kaya zote katika tarafa hiyo kujenga vyoo na kuvitumia na kwamba kaya yoyote ambayo haitakuwa na choo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.