Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  NHC yazidai wizara mamilioni ya shilingi
NHC yazidai wizara mamilioni ya shilingi
By Habari Tanzania | Published  08/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Hellen Ngoromera

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC), linazidai wizara mbalimbali sh milioni 600 kwa ajili ya upangishaji katika nyumba zake.

Mkurugenzi Mtendaji wa NHC, Martin Madekwe, alibainisha hayo jana wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika katika Makao Makuu ya NHC, Barabara ya Mandela, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Madekwe hakuwa na kumbukumbu ya idadi kamili ya wizara zinazodaiwa na kiasi cha fedha kwa kila wizara.

Akizungumza wakati akizindua bodi hiyo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, aliitaka bodi hiyo kufuatilia madeni hayo ili fedha zitakazopatikana zitumike katika shughuli mbalimbali, ukiwamo ujenzi wa nyumba nyingine za NHC.

“Ni jukumu lenu kufuatilia madeni katika wizara yanayodaiwa ili makusanyo yatumike kwa shughuli mbalimbali za kuinufaisha nchi,” alisema Magufuli.

Sambamba na hilo, Magufuli aliwataka watendaji wa NHC kuendeleza ubia kwa kuyaendeleza majengo ili kuiwezesha miji kukua na kubadilika.

Magufuli aliitaka NHC kutoishia kujenga majengo ya ghorofa moja au tatu, bali ipige hatua kwa kujenga majengo yenye ghorofa nyingi.

“Jengeni ghorofa saba hadi mia moja, tutumie wataalamu wetu tulionao kubadilisha miji yetu,” alisema.

Aliwataka pia kutojenga mijini tu, bali wafike hadi wilayani na mikoa mbalimbali kwa lengo la kuwa na nyumba bora na za kisasa hivyo kuifufua NHC.

Alisema soko la nyumba lipo, linazidi kukua, na kwamba kinachotakiwa ni kujenga nyumba nyingi na za kisasa.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Magufuli aliwataadharisha wananchi wanaotumia udanganyifu kwa kupanga nyumba za NHC wakati hawaishi katika nyumba hizo.

Katika uteuzi huo, Balozi Sulemani Hemed, ameteuliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo mpya. Wajumbe ni Dk. Tumsifu Nkya, Elius Mwakalinga, Andrew Masawe, Mhandisi Consolata Ngimbwa, Blandina Nyoni, Blasi Seleki na William Ngeleja.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.