Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge ashitakiwa na wafanyakazi
Mbunge ashitakiwa na wafanyakazi
By Habari Tanzania | Published  08/17/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Deogratius Temba, SAUT

WAFANYAKAZI 16, wa kampuni binafsi ya ulinzi ya Yono Security ya jijini Dar es Salaam, wanamshitaki mwajiri wao, wakidai wamefukuzwa kazi kinyume cha sheria.

Kampuni hiyo ni miongoni mwa kampuni nyingi zinazomilikiwa na Mbunge wa Njombe Magharibi, Stanley Kevela (CCM).

Wafanyakazi hao wamefungua madai yao kwa Ofisa Kazi Mkoa wa Dar es Salaam, wakidai walifukuzwa kazi Agosti 5, mwaka huu bila kupewa stahili zao.

Kampuni hiyo ilimtuma mhasibu wake aliyejulikana kwa jina moja la Gunda, kwenda kwa Ofisa Kazi kujibu tuhuma hizo.

Mhasibu huyo, kwa niaba ya mkurugenzi wake, alisema kila mfanyakazi atalipwa sh 109,000 kama mafao yao kwa kipindi chote cha miaka mitatu walichofanya kazi. Mshahara wa kila mfanyakazi ni sh 48,000 kwa mwezi.

Wafanyakazi wanalalamika kuwa kiasi cha mafao walichopangiwa kulipwa ni kidogo.

Ofisa Kazi Mkoa ametaka wafanyakazi hao walipwe mishahara yao kuanzia siku walipoachishwa kazi, mapunjo ya mishahara yao, malipo ya muda wa ziada kazini, na malipo ya likizo.

Mkurugenzi huyo ametakiwa afike ofisini kwa Ofisa Kazi Agosti 24, mwaka huu.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.